Wafuasi wa Samia Suluhu wangemuiga Hussein Bashe, wasingekuwa wanamwaga damu ya Binadamu

Wafuasi wa Samia Suluhu wangemuiga Hussein Bashe, wasingekuwa wanamwaga damu ya Binadamu

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,132
Reaction score
64,416
Kinacho sababisha watu kuteka binadamu, kuua ni Umasikini. Yaani Matajiri wanatumia pesa zao kuwapa Masikini ili wamwage damu za masikini wenzao na hao Masikini wanaoua wenzao, wanajisifu kwa kumwaga damu ya Binadamu fukara mwenzao ili kumfurahisha Mtawala/ tajiri alowatuma.

Yaani masikini anatumia gari ya tajiri kwenda kumuua Mdude nyagali, Deus Soka, Shadrack Chaula, Mawazo.. Akishaua anapita gengeni kununulia dagaa wanaye kwa hela ilitokana na kumwaga damu ya Binadamu mwenzie.

Yaani Masikini anapewa hela na tajiri amuue Maskini mwenzie. Hela anapewa kwa kumwaga damu. Yaani analisha mke na mtoto kwa vijisenti vilivyotokana na kumwaga damu ya mtu.

Wanasiasa wanatumia vyeo vyao na pesa zao kuwatuma masikini wasio na elimu kuua wapinzani wao wa kisiasa ili watawale milele.

Kungekuwa na siasa za haki, mauaji yasingekuwepo.

Watu wangetaka pesa za halali, mauaji yasingekuwepo.

Watu wanataka hela za ufisadi na ukisema wanaiba matokeo yake wanakuua. Hawa wanasiasa wanapambana kupata vyeo na nafasi za juu za uongozi ili wakaibe.

Je, Wangeamua kula kwa Jasho kama anavyofanya Hussein Bashe, Mauaji na utekaji ungekuwepo?

Kutotaka kufanya kazi kwa jasho ndo matokeo ya damu kumwagika Tanzania.

Hongera sana Bashe kwa kuwaonesha hawa Wazanzibari jinsi hela inapatikana pasipo kupoteza uhai wa mtu.
 
Kwa hiyo ule mpango wa BBT ndio lengo lake lilikuwa kujinufaisha yeye na miradi yake binafsi? Th
Watanzania tumezidi roho mbaya. Hapo kajinufaisha vipi? Halima Mdee ana mradi zaidi ya hicho ulichoona kwenye Video., naye unasemaje? Punguza wivu, fanya kazi. Mbunge miaka kibao, Waziri, Mfanyabiashara, kwamba ashindwe kuwa na mifungo, shamba, Mashine ya kulimia na lori la kichina? Hiyo Video ni Intro tu.. Hiyo ni Dibaji wala haijaonesha chochote ushaanza kutoa povu🤣🤣

Mkuu, usikate tamaa, Tanzania kuna fursa

Bashe hajaanza kufuga leo.. Ameingia kwenye siasa akiwa na kampuni zake nyingi tu. Moja wapo ni hii. Ambapo anapata lita zaidi ya elfu ishirini za maziwa kwa siku

 
Watanzania tumezidi roho mbaya. Hapo kajinufaisha vipi? Halima Mdee ana mradi zaidi ya huo, naye unasemaje? Punguza wivu, fanya kazi. Mbunge miaka kibao, Waziri, Mfanyabiashara, kwamba ashindwe kuwa na mifungo, shamba, Mashine ya kulimia na lori la kichina?

Mkuu, usikate tamaa, Tanzania kuna fursa

Bashe hajaanza kufuga leo.. Ameingia kwenye siasa akiwa na kampuni zake nyingi tu. Moja wapo ni hii. Ambapo anapata lita zaidi ya elfu sitini za maziwa kwa siku

Ni vile tu watanzania wengi mpo gizani,hiyo miradi haiendani na kipato cha waziri hata uwe waziri miaka 50 huwezi kuvipata.
Labda uibe ,uzulumu au tayari ulikuwa tajiri kabla ya kuwa Mbunge au Waziri.
 
Hata yeye alikuwa mwizi,hakuna mwanasiasa ambaye sio mwezi katika hii nchi labda wanasiasa wa wakati wa Nyerere
Huyu amerasimisha wizi wake na sasa kaajiri vijana. Sasa fikiria ni wanasiasa wangapi hawastaafu wizi wa hela za serikali na wala hela zao hawawekezi kwenye chochote zaidi ya kununua hisa na bond.
Wanasiasa wezi inabidi warudishe hela kwenye mzunguko kwa kuwekeza kama Bashe ili kuongeza uzalishaji na kuajiri vijana
 
Watanzania tumezidi roho mbaya. Hapo kajinufaisha vipi? Halima Mdee ana mradi zaidi ya huo, naye unasemaje? Punguza wivu, fanya kazi. Mbunge miaka kibao, Waziri, Mfanyabiashara, kwamba ashindwe kuwa na mifungo, shamba, Mashine ya kulimia na lori la kichina?

Mkuu, usikate tamaa, Tanzania kuna fursa

Bashe hajaanza kufuga leo.. Ameingia kwenye siasa akiwa na kampuni zake nyingi tu. Moja wapo ni hii. Ambapo anapata lita zaidi ya elfu ishirini za maziwa kwa siku

60k litres hongera sana Bashe. Ufugaji upo damuni mwake. Anapenda sana mifugo. Nakumbuka ng'ombe wake mmoja alikufa aliomboleza sana.
 
Wewe,ukipata nafasi lazima uitumie yaani mtu yupo level ya uwaziri unataka awe kama wewe
Kumbe hakukuwa na sababu ya kufuta tawala za kimila na kukubali kuunda taifa la Tanganyika na baadaye Tanzania, kwa hiki kinachoendelea kama ni kweli basi Serikali imegeuka kuwa wakala wa genge la mafisadi wanaotumia wadhifa uliopo kisheria kujikusanyia mitaji ya umma kifisadi kwa maslahi binafsi.
 
Ni vile tu watanzania wengi mpo gizani,hiyo miradi haiendani na kipato cha waziri hata uwe waziri miaka 50 huwezi kuvipata.
Labda uibe ,uzulumu au tayari ulikuwa tajiri kabla ya kuwa Mbunge au Waziri.
Kwahiyo bora kwako ni kuua, kuteka na kudhurumu uhai wa watu. Mfano Kampuni hii nimeshare hapa ni ya Familia. Ipo tangu 1946.. Kama mzazi wako hakuwekeza kwaajili yako, waongeze wenzio. Ondoa imani zako za mtu kufanikiwq lazima aibe na kuua.
 
60k litres hongera sana Bashe. Ufugaji upo damuni mwake. Anapenda sana mifugo. Nakumbuka ng'ombe wake mmoja alikufa aliomboleza sana.
Eelfu sitini n Malengo ndani ya miaka 2. Kwa sasa anazalisha elfu ishirini kwa siku
 
Kumbe hakukuwa na sababu ya kufuta tawala za kimila na kukubali kuunda taifa la Tanganyika na baadaye Tanzania, kwa hiki kinachoendelea kama ni kweli basi Serikali imegeuka kuwa wakala wa genge la mafisadi wanaotumia wadhifa uliopo kisheria kujikusanyia mitaji ya umma kifisadi kwa maslahi binafsi.
Utateseka Sana yaani mtu awe Waziri wa kilimo halafu ushangae kuwa na hiyo miradi.

Wewe unawaza ufisadi tu,kama alikopa je,au unadhani anakopeshwa Milioni Hamsini Huyo, level zake anavuta mzigo wa kutosha
 
Back
Top Bottom