Wafuasi wa Samia Suluhu wangemuiga Hussein Bashe, wasingekuwa wanamwaga damu ya Binadamu

Wafuasi wa Samia Suluhu wangemuiga Hussein Bashe, wasingekuwa wanamwaga damu ya Binadamu

Kwani wanasiasa kuiba hela inamuhitaji awe accounting Officer???
Anaibaje? Hela yoyote isipokuwa yako binafsi huwa ina utaratibu wa kuifikia. Hela ya Serikali Mwanasiasa anaibaje? Wanasiasa wengi wenye hela wananufaika na unafuu wa kukwepa kodi kwenye biashara zao binafsi au unafuu wa kujiingiza kwenye biashara haramu yenye hela ya haraka kwa kutumia kivuli cha unafuu wa Diplomasia na rushwa ili uharamu wao upite. Lakini hela za Serikali zina utaratibu mgumu kiasi cha kuweza kuweza kufika kwa mwanasiasa. siyo rahisi.
 
Ndio maana ake 😄
Screenshot_20261026_065128_Chrome.jpg
 
Watanzania tumezidi roho mbaya. Hapo kajinufaisha vipi? Halima Mdee ana mradi zaidi ya huo, naye unasemaje? Punguza wivu, fanya kazi. Mbunge miaka kibao, Waziri, Mfanyabiashara, kwamba ashindwe kuwa na mifungo, shamba, Mashine ya kulimia na lori la kichina?

Mkuu, usikate tamaa, Tanzania kuna fursa

Bashe hajaanza kufuga leo.. Ameingia kwenye siasa akiwa na kampuni zake nyingi tu. Moja wapo ni hii. Ambapo anapata lita zaidi ya elfu ishirini za maziwa kwa siku

Haiondoshi kuwa wanasiasa wa nchi hii ni wezi nae akiwa mmoja wapo
 
af2ccfe70e0d88984385df44.png




Nembo ya Bashe Dairy Farm Ltd
1a5fc9e08108e753d9822c68.png


Ndani ya Shamba Letu la Kijani: Nishati ya Jua na Kilimo cha Mviringo

Blogu
2026

Ndani ya Shamba Letu la Kijani: Nishati ya Jua na Kilimo cha Mviringo​


Uendelevu katika Shamba la Maziwa la Bashe si zoezi la kuweka chapa — ni jinsi shamba linavyoendeshwa kila siku. Mfumo wa uendeshaji wa nishati ya jua tayari unapunguza utegemezi wetu kwenye dizeli na gridi ya TANESCO, huku bwawa la umwagiliaji la mita 650 × 300 × 11 likitoa kila hekta ya mazao na kila kichwa cha mifugo usalama wa maji mwaka mzima.

Taka za mifugo hubadilishwa kuwa mbolea ya kikaboni na kurudishwa kwenye ekari zetu zaidi ya 300 za mahindi na silage, na hivyo kufunga kitanzi kati ya kundi la ng'ombe wa maziwa na malisho yanayoliendeleza. Kilimo cha alizeti huongeza safu ya pili kwenye mzunguko huo, na kutoa mafuta ya kula huku keki yake ya mafuta ikiwa nyongeza ya chakula chenye protini nyingi.

Kulisha Jumla ya Mgawo Mchanganyiko (TMR), kwa kuchanganya na kupelekwa shambani, huweka mfumo mzima wa lishe sawa — kupunguza upotevu, kuboresha afya ya kundi, na kupunguza gharama kwa kila lita ya maziwa tunayozalisha.

Habari Zaidi​

Bashe Yoghurt Range Yapata Cheti cha Alama ya Kawaida ya TBS

Bashe Yoghurt Range Yapata Cheti cha Alama ya Kawaida ya TBS​

Halali hadi 21 Februari 2027
Kituo cha Uwekezaji Tanzania Chatoa Cheti cha Motisha kwa BDF

Kituo cha Uwekezaji Tanzania Chatoa Cheti cha Motisha kwa BDF​

Kujenga Kufikia Lita 60,000 kwa Siku


Kujenga Kufikia Lita 60,000 kwa Siku​


Safari ya Vizazi Vitatu: Kuanzia 1946 hadi Ekari 3,000


Safari ya Vizazi Vitatu: Kuanzia 1946 hadi Ekari 3,000​

Utofauti wa Spishi Shamba: Ngamia, Nyati, na Zaidi

Utofauti wa Spishi Shamba: Ngamia, Nyati, na Zaidi​

Nembo ya Bashe Dairy Farm Ltd

Shamba la kilimo cha viwanda lenye ukubwa wa ekari 3,000 katika Kijiji cha Kinyamwe, Kata ya Magiri, Uyui-Tabora — limeidhinishwa na TIC na linatii sheria za TBS.

​

 
Kinacho sababisha watu kuteka binadamu ni Umasikini. Yaani Matajiri wanattumia pesa zao kuwapa Masikini ili wamwage damu kumfurahisha tajiri.

Yaani Masikini anapewa hela na tqjiri amuue Maskini mwenzie. Hela anapewa kwa kumwaga damu. Yaani analisha mke na mtoto kwa mali zilizotokana na kumwaga damu.

Wanasiasa wanatumia vyeo vyao na pesa zao kuwatuma masikini wasio na elimu kuua wapinzani wao wa kisiasa ili watawale milele.

Kungekuwa na siasa za haki, mauaji yasingekuwepo.

Watu wangetaka pesa za halali, mauaji yasingekuwepo.

Watu wanataka hela za ufisadi na ukisema wanaiba matokeo yake wanakuua. Hawa wanasiasa wanapambana kupata vyeo na nafasi za juu za uongozi ili wakaibe.

Je, Wangeamua kula kwa Jasho kama anavyofanya Hussein Bashe, Mauaji na utekaji ungekuwepo?

Kutotaka kufanya kazi kwa jasho ndo matokeo ya damu kumwagika Tanzania.

Hongera sana Bashe kwa kuwaonesha hawa Wazanzibari jinsi hela inapatikana pasipo kupoteza uhai wa mtu.
View attachment 3698736
Shamba limeanzishwa 1960s
 
Amejinufaishaje? kwani yeye ndio alikuwa mhasibu wa BBT? Nani alikuambia Waziri ni Accounting Officer? Maskini siku zote ana roho ya umaskini na mawazo yake ni ya kimaskini?
Taratibu Ramses Il ili kuanzisha mradi mkubwa kama huo inahitaji mchakato mrefu wa usajili kwenye mamlaka mbali mbali za udhibiti na usimamizi, kwa nafasi yake kama Waziri wa Kilimo kuanzisha mpango kitaifa uliofeli unapoonekana kuwa na mafanikio kwenye makampuni yake binafsi wewe huoni kuwa tunapaswa kuhoji? Wewe kama unaona ni sawa, ni maoni yako wewe ila mimi ninayelipa kodi zote za Serikali kwa wakati ni haki yangu kuhoji, hii kauli ya mawazo ya kimasikini ni ya kijima sana,nakushauri uachane nayo maana haina tofauti na ile ya "Aliyeko juu mngoje chini" ni kauli za uswahilini hizo. Kijana unatakiwa uwe na ujasili wa kuhoji.
 
Kwahiyo bora kwako ni kuua, kuteka na kudhurumu uhai wa watu. Mfano Kampuni hii nimeshare hapa ni ya Familia. Ipo tangu 1946.. Kama mzazi wako hakuwekeza kwaajili yako, waongeze wenzio. Ondoa imani zako za mtu kufanikiwq lazima aibe na kuua.
Kwa hiyo hicho ki-clip tayari umechotwa akili?

Kabla ya uwaziri alikuonesha chochote kuhusu hiyo kampuni ya familia? Si alikuwa muajiriwa wa Rostam Dar huyo?

Tuhuma zooote kuanzia vibali vya kuagiza sukari na BBT zinasafishwa na video mtu kuwa shamba?

Hii nchi ujinga umetamalaki kwelikweli.
 
Kinacho sababisha watu kuteka binadamu ni Umasikini. Yaani Matajiri wanattumia pesa zao kuwapa Masikini ili wamwage damu kumfurahisha tajiri.

Yaani Masikini anapewa hela na tqjiri amuue Maskini mwenzie. Hela anapewa kwa kumwaga damu. Yaani analisha mke na mtoto kwa mali zilizotokana na kumwaga damu.

Wanasiasa wanatumia vyeo vyao na pesa zao kuwatuma masikini wasio na elimu kuua wapinzani wao wa kisiasa ili watawale milele.

Kungekuwa na siasa za haki, mauaji yasingekuwepo.

Watu wangetaka pesa za halali, mauaji yasingekuwepo.

Watu wanataka hela za ufisadi na ukisema wanaiba matokeo yake wanakuua. Hawa wanasiasa wanapambana kupata vyeo na nafasi za juu za uongozi ili wakaibe.

Je, Wangeamua kula kwa Jasho kama anavyofanya Hussein Bashe, Mauaji na utekaji ungekuwepo?

Kutotaka kufanya kazi kwa jasho ndo matokeo ya damu kumwagika Tanzania.

Hongera sana Bashe kwa kuwaonesha hawa Wazanzibari jinsi hela inapatikana pasipo kupoteza uhai wa mtu.
View attachment 3698736
hongera sana saba Bashe ni mfano mzuri sana wa viongozi kwa vitendo
 
Kwa hiyo hicho ki-clip tayari umechotwa akili?

Kabla ya uwaziri alikuonesha chochote kuhusu hiyo kampuni ya familia? Si alikuwa muajiriwa wa Rostam Dar huyo?

Tuhuma zooote kuanzia vibali vya kuagiza sukari na BBT zinasafishwa na video mtu kuwa shamba?

Hii nchi ujinga umetamalaki kwelikweli.
Ulishaonja bidhaa zake? Kwanza hiyo Video ni Intro tu.. Punguza presha.. Kutembelea shamba lake ni bure. Usichoke kujifunza.

 
Taratibu Ramses Il ili kuanzisha mradi mkubwa kama huo inahitaji mchakato mrefu wa usajili kwenye mamlaka mbali mbali za udhibiti na usimamizi, kwa nafasi yake kama Waziri wa Kilimo kuanzisha mpango kitaifa uliofeli unapoonekana kuwa na mafanikio kwenye makampuni yake binafsi wewe huoni kuwa tunapaswa kuhoji? Wewe kama unaona ni sawa, ni maoni yako wewe ila mimi ninayelipa kodi zote za Serikali kwa wakati ni haki yangu kuhoji, hii kauli ya mawazo ya kimasikini ni ya kijima sana,nakushauri uachane nayo maana haina tofauti na ile ya "Aliyeko juu mngoje chini" ni kauli za uswahilini hizo. Kijana unatakiwa uwe na ujasili wa kuhoji.
Alianza kufuga kabla hata ya kuwa mbunge , alianza 2008 ubunge kaupata 2015 ,uwaziri wa kilimo kaupata 2021 kwa hiyo BBT imemkuta yupo vizuri ,pia ni mjasiria mali mzuri
 
Nimewahi kuona projects zake, mwenzetu yupo mbali sana kwenye uwekezaji wa Kilimo

Ana kampuni ya kusindika maziwa, yupo kwenye pembejeo, ananunua na kuuza mazao n.k
 
Nasikia ana kituo cha mafuta pia.

Ila sema kuhusu kugombania madaraka hii hali kila mwanasiasa hasa hawa vijana wanayo.

Mana ule mtanange wa bashe na mashiri.....adi mashiri alinyoosha mikono mwenyewe
 
Alianza kufuga kabla hata ya kuwa mbunge , alianza 2008 ubunge kaupata 2015 ,uwaziri wa kilimo kaupata 2021 kwa hiyo BBT imemkuta yupo vizuri ,pia ni mjasiria mali mzuri
Sikatai kwani nafahamu wazazi wake walikuwa wafanyabiashara tangu miaka ya sitini huko, hivyo mtaji ulikuwepo, hata kama amefanya maboresho na kufanya biashara kuwa ya kisasa, swali ni kwa nini BBT aliyoinadi kwa nguvu kubwa tena kitaifa haikufanikiwa?
 
Ujue bora uibiwe na mwenye akili kama huyu angalau wananchi wa huko watapata hata ajira.
Sasa watu wanaiba wanannua magari na majumba ya billions of money tena hata sio bongo.
Magari yamepaki tu hata muda wa kuyaendesha hawana inatia hasira sana.
Jengeni hata viwanda basi mpunguze hawa panya road mitaani!
 
Kinacho sababisha watu kuteka binadamu, kuua ni Umasikini. Yaani Matajiri wanatumia pesa zao kuwapa Masikini ili wamwage damu za masikini wenzao na hao Masikini wanaoua wenzao, wanajisifu kwa kumwaga damu ya Binadamu fukara mwenzao ili kumfurahisha Mtawala/ tajiri alowatuma.

Yaani masikini anatumia gari ya tajiri kwenda kumuua Mdude nyagali, Deus Soka, Shadrack Chaula, Mawazo.. Akishaua anapita gengeni kununulia dagaa wanaye kwa hela ilitokana na kumwaga damu ya Binadamu mwenzie.

Yaani Masikini anapewa hela na tajiri amuue Maskini mwenzie. Hela anapewa kwa kumwaga damu. Yaani analisha mke na mtoto kwa vijisenti vilivyotokana na kumwaga damu ya mtu.

Wanasiasa wanatumia vyeo vyao na pesa zao kuwatuma masikini wasio na elimu kuua wapinzani wao wa kisiasa ili watawale milele.

Kungekuwa na siasa za haki, mauaji yasingekuwepo.

Watu wangetaka pesa za halali, mauaji yasingekuwepo.

Watu wanataka hela za ufisadi na ukisema wanaiba matokeo yake wanakuua. Hawa wanasiasa wanapambana kupata vyeo na nafasi za juu za uongozi ili wakaibe.

Je, Wangeamua kula kwa Jasho kama anavyofanya Hussein Bashe, Mauaji na utekaji ungekuwepo?

Kutotaka kufanya kazi kwa jasho ndo matokeo ya damu kumwagika Tanzania.

Hongera sana Bashe kwa kuwaonesha hawa Wazanzibari jinsi hela inapatikana pasipo kupoteza uhai wa mtu.
View attachment 3698736
Angepanda nyasi, hayo mahindi yangefaa kwa matumizi mengine, hatumpangii lakini uhalisia ndio hivyo kwenye umasikini uliotopea kulisha ng'ombe mahindi ni kukosa umakini na hii miradi wameanzisha kwa pesa zetu kwenye ile miradi iliyotakiwa wapewa watu masikini wamejipa wao, nani hajui Bashe na wenzake kuwa wamejipendelea.
 
Alivyokua kwenye system mlikua mnamuandama sasa hivi Bashe Shujaa😂😂😂
Hakuna binadamu asiye semwa.. Maisha ndovyo yalivyo na huwezi kumkataza mtu kusema. Acha kila mtu aseme anachofikiria
 
Back
Top Bottom