Wafugaji wa kuku wa nyama na mayai wasiosajiliwa kuchukuliwa hatua

Ni hela tu inatafutwa hapo. Haluna kingine
 
Madhara ya kuongozwa na kichaa ndio haya Mkuu.
 
Kila mtu atafikiwa ni suala la muda tu.
One world order, lazima tuwe kwenye mfumo! kuna siku itafika huwezi kuuza wala kununua endapo huna namba ya utambulisho. wafanyakazi hivi sasa lazima wawe na TIN number, ili kupata mshahara. sasa wewe unayefuga kware utatambulikananje kama hujajisajili?😎🀣
 
Kwa sababu msipojisajiri. Kuna watu wabaya wanaweza kutokea ndani au nje ya jamii wakatuuzia kuku ambao sio salama kwa afya. Tuko kwenye vita ya kiuchumi ambayo huwezi jua adui anakuja kwa style gani. Kwa hiyo we tulia kama ulivo serikali ulikulinde.
Ndo hivo hivo tulifika kwenye conclusion kwamba NGOs zisajiliwe kwa sababu kilikua na NGOs ambazo zilikua zina malengo evil juu ya hili taifa.

So relax brother. This goverment fights a lot of battles in silence na wananchi hawawezi kujua kwa sababu wanasikiliza sana western media kuliko kufatilia ukweli
 
Ni kweli tunahitaji barabara na madaraja lakini sio kwa mtindo huu
 
10 tenaa...!! Watasajilii mpaka wafugaaa mbwaaa
 
Safi sana.Tunaanza na wanaosafirisha kuku kwenye bodaboda na vipikapu watuonyeshe vibali vyao kwa kuwa ilishatangazwa wasafirisha vitoweo wapate leseni. Kisha tunauliza watuonyeshe manda yao ya kufugia na Vibali vyao. Kama hawana tuntaifisha kuku. Hatuachi mpaka kuku wapotee mjini na wapande bei. Tuige kufuata sheria bila shuruti kama wapinzani walivyofanya wakati wa uchaguzi. Tano tena.
 
Hii taarifa iliyoandikwa kwenye magazeti inaweza kuwa ya kitambo lakini nadhani ninjambo linalotakiwa kujadiliwa kwa kina. Mimi nilifikiri wanaotakiwa kuwekewa kipaumbele cha kusajiliwa ni wale wanaotoa huduma kwenye tasnia ya ufugaji kuku. Hao ni pamoja na:

Matabibu wa mifugo,
Animal production specialists,
Wauza pembejeo, et cetera

Aidha, maelezo haya pia yame exclude wafugaji wa kuku wa asili, ambao, takwimu zinaonesha kuwa ni wengi zaidi ya kundi lengwa na hivyo ndio wenye mchango mkubwa
 
Like seriously KUKU?

Mbona sasa badala ya kupunguza umasikini instead mnaweka sheria zinazoongeza umasikini?

Nani anatunga hizi sheria kandamizi juu ya hawa masikini?

Kuna trailer ya far cry 6 ipo YouTube ina ujumbe mzito sana.
Kwamba nchi ni kama grenade iliyochomolewa pini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…