sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Hizi jela zetu zimekuwa sehemu ya mateso na sio sehemu ya kumrekebisha mtu tabia.
Mfano hapa jela ya Mbeya Mjini watu wanafanya kazi asubuhi hadi saa nane mchana, hio kazi wanayofanya ni nzito ambayo uraiani anastahili malipo ya chini iwe kumudu milo miatu lakini wao wanapewa chakula mara moja tu saa tisa mchana, hicho chakula ni ugali maharage ambao haufikii hata nusu sahani, hapo ni mpaka kesho tena.
Unyanyasaji ni wa hali ya juu wafungwa ni kama watumwa kipindi cha ukoloni, nakumbuka hapa Mbeya kuna sehemu ya makaburi kulikuwa kuna nyasi ndefu ilibidi zifyekwe ila kulikuwa na nyoka wengi hio sehemu, ilibidi wafungwa ndio wafyeke (ukikataa unatembezewa kipigo kzito), pia nakumbuka rais Magufuli alitilia mkazo Wafungwa wawe wanapigwa mateke.
Pia hakuna haki kwa wafungwa wenye ndoa kukutana faragha, mfano kijana wa miaka 27 akifungwa miaka 30, ni kwamba katika hii miaka 30 hataruhusiwa kukutana kimapenzi na mke wake na hataweza kuwa na watoto, na hata akiamua kuwa na watoto baada ya kifungo, tayari umri utakuwa umeenda sana hata watoto watamwita babu. hapa ndipo ndoa huwa zinavunjika, binti anamkimbia mme wake kwasababu ya huu unyanyasaji.