View attachment 2143225
Hizi jela zetu zimekuwa sehemu ya mateso na sio sehemu ya kumrekebisha mtu tabia.
Mfano hapa jela ya Mbeya Mjini watu wanafanya kazi asubuhi hadi saa nane mchana, chakula ni saa tisa mchana yani chakula ni ugali maharage ambao haufikii hata nusu sahani.
pia unyanyasaji wa vipigo ni wa hali ya juu, nakumbuka rais
Magufuli alitoa amri Wafungwa wafanyishwe kazi usiku na mchana na wapigwe mateke
Pia kwa wale waliooa, wakiingia jela ndoa huwa zinaharibika moja kwa moja, mtu ukiingia jela huwezi kuwa faragha na mke wako mpaka umalize kifungo, ni wanawake wache sana wanaweza kuwa waaminifu katika hi hali.
Hii hali sio hali aisee.