Masamila
JF-Expert Member
- Jun 22, 2014
- 6,490
- 7,422
Yuko jirani yangu hapa Kimara B alikwenda kurushia kanisa la walokole usiku wa manane kisa wanampigia makelele hawezi kulala. Asubuhi polisi wakaja kumbeba, utani utani kaja mtu mmoja kumuwekea dhamana , policcm wakasema wanataka wadhamini wawili, kisa mchungaji aliwapa ubani. Ilikua ijumaa, kufumba na kufumbua mshikaji Yuko gerezani.
Amesema kule kula kwa foleni, ugali na Maharage, siku ya kwanza walimpa Maharage 17 siku ya pili 14. Kujisaidia haja kubwa unasimamiwa na kijana mdogo na unaambiwa UFANYE haraka.
Kulala ndio ishu, maana mnakabana Kama mihogo na joto hili. Vidirisha viko juu kabisa haviingizi hewa.
Ameapa hata Kama walokole watapiga mziki mpaka saa Tisa usiku. Hatowagusa.
Ahhahahha Dah