Wafungwa kula mlo mmoja kwa siku na hufanya kazi ngumu, hii ni haki?

Wafungwa kula mlo mmoja kwa siku na hufanya kazi ngumu, hii ni haki?

Napendekeza jela ziondolewe zote mjini. Mjini zibaki mahabusu tu. Wapelekwe sehemu wanazoweza kulima mashamba ya maana. Huko wapewe hata wali nyama, ila wazalishe wenyewe.
 
Kuna haja kubwa hili swala ulilolileta hapa kupewa a special national attention.

Tupaze sauti zetu mpaka zimfikie mama Samia Suluhu Hassan
 
Wangekuwa wote waliopo huko wametenda kosa kweli, ni haki yao kula hivyo, ili wakitoka wasirudie tena kosa
 
Ipo haja ya jela watu waruhisiwe kushiriki mapenzi na wake zao, mfano sabaya unamfunga Miaka 30 bado kesi zingine still ni kijana hana mtoto kwann asipewe haki ya kutungisha mimba Ili akitoka jela akute watoto wake ni wakubwa wamfae uzeeni.
hao watoto watakula mawe siyo
mwanamke yupi yupo tayari kulalwa na mfungwa ?
 
hao watoto watakula mawe siyo
mwanamke yupi yupo tayari kulalwa na mfungwa ?
Mke wa mfungwa atalalwa na nani sasa Ili apate watoto baada ya mke kuruhusiwa kuingia jela kushiriki na mme wake.
Pia makahaba waruhisiwe kuingia jela baada ya kupimwa Ili kupunguza joto
 
View attachment 2143225

Hizi jela zetu zimekuwa sehemu ya mateso na sio sehemu ya kumrekebisha mtu tabia.

Mfano hapa jela ya Mbeya Mjini watu wanafanya kazi asubuhi hadi saa nane mchana, hio kazi wanayofanya ni nzito ambayo mturaiani mtu anaweza kulipwa hela hata ya milo miatu lakini wao wanapewa chakula mara moja tu kwa siku saa tisa mchana, hicho chakula ni ugali maharage ambao haufikii hata nusu sahani, hapo ni mpaka kesho tena.

unyanyasaji wa vipigo ni wa hali ya juu, nakumbuka rais Magufuli alitoa amri Wafungwa wafanyishwe kazi usiku na mchana na wapigwe mateke, wafungwa hawana haki kabisa ya kutoa maoni, mfano wakigoma chakula ni kidogo na wanakula mara moja kwa siku wakifanya mgomo huwa wanapigwa sana.

Pia hakuna haki kwa walio katika ndoa kuwa faragha, mfano kijana wa miaka 27 anafungwa miaka 15, wakati huo bado hana mtoto ila ana mchumba / mke aliemwacha uraiani, hapo ni kwamba hataweza kumtungisha mimba mke wake mpaka kifungo kiishe na muda huo umri wake utakua 40+, kwa hali hii ni wazi kabisa jela inatengeneza mazingira ya mwanamke kumkimbia mme wake, atazalishwa na kuolewa na mwanaume mwengine uraiani kwa sababu jela hakuna haki ya wanandoa. hali hii nayo inapelekea jela ziwe sehemu za kutengeneza mashoga.
Uliza uambiwe! Wafungwa wanapewa chakula cha kuwafanya wasife. Ni mojawapo ya kinga kwa Askari wanaowalinda
 
Mfungwa atungishe mimba, nani atalea huyo mtoto? Wewe uko tayari kutoa binti yako akatungishwe mimba na mfungwa? Kumbafu wewe.
Soma uelewe matusi ni mtu ajapita shule.
Mke wa mfungwa kwann anyimwe haki ya kuzaa na me wake aliyejela?
 
Hilo la wafungwa kulipwa pesa na kuwekwa kwnye ACC zao ni ngumu sn kwa Tanzania.

Kama mahabusu ana kaa week anatoka na kukuta Askari kajimilikisha simu pamoja na viatu vya mtuhumiwa.

Unadhani ya gerezani unapokaa miaka pesa zako itawezekana kubaki salama?

Sent from my M2101K7BG using JamiiForums mobile app

Wanaweza wakaweka utaratibu magereza zikaingia ubia na wawekezaji.
Mwekezaji anatumia nguvu Kazi ya wafungwa kwenye miradi inayomilikiwa na magereza serikali inabakia na suala la usimamizi wa wafungwa na kuhusu macho ya uchumi na uzalishaji usimamiwa na mwekezaji then mfungwa uwekewa pesa yake huku akipata ujuzi akimaliza kifungo upewa mtaji mfano pesa na vifaa apate pa kuanzia maisha.
 
Pia makahaba waruhisiwe kuingia jela baada ya kupimwa Ili kupunguza joto
hapa sawa
Mke wa mfungwa atalalwa na nani sasa Ili apate watoto baada ya mke kuruhusiwa kuingia jela kushiriki na mme wake
ukishakula mvua tu, mke hamu na wewe hana,
hata ule 'ute' hatotoa anajua 'kitega uchumi' wake hayupo
tegemea adai talaka badala yake
 
Soma uelewe matusi ni mtu ajapita shule.
Mke wa mfungwa kwann anyimwe haki ya kuzaa na me wake aliyejela?
Sabaya alifunga lini ndoa? Unataka familia ya huyo binti ibebe mzigo wa kulea mtoto wa mfungwa? Acha kutumia masaburi, tumia akili.
 
Inauma Sana Kila nikifikiria wafungwa wa nchi hii wanavyoteseka,wanatumiwa kisiasa Sana kama nguvu Kazi ya kuwanufaisha wachache,
Hua nikifikiria siku Moja nikija kua kiongozi nibadilishe Mifumo ya kitumwa Kwenye magereza yetu hata wale waliohukumiwa vifungo vya maisha wahisi angalau ladha ya maisha na sio wanaishia kuona maisha kwao hayana thamani kisa mistake walizofanya na kuwafikisha hapo,

Hili swala linahitaji mjadala wa kitaifa kunusuru Hali maana wote humu ni wafungwa watarajiwa,usijione kama haikuhusu Hivi Haya maisha muda wowote historia yako Inaweza geuka Mpaka usiamini kisa maswala madogo madogo tu
Ushakua mfungwa tayari,
Kwani Sabaya aliwahi tegemea Kwa nafasi aliyokua nayo kama atakuja ingia jela?
 
Kuna haja kubwa hili swala ulilolileta hapa kupewa a special national attention.

Tupaze sauti zetu mpaka zimfikie mama Samia Suluhu Hassan

Umepuyanga hapo kwa kumtaja huyo kiumbe uliyemuita mama.
 
Mke wa mfungwa atalalwa na nani sasa Ili apate watoto baada ya mke kuruhusiwa kuingia jela kushiriki na mme wake.
Pia makahaba waruhisiwe kuingia jela baada ya kupimwa Ili kupunguza joto

Hivi jela za wanawake pia hapo umezingatia?
 
achana na kukosea mtaani na jeshi la polisi acheni kubambikiza kesi watu
 
Back
Top Bottom