Wahenga wenzangu njoo tukumbushane vipindi vilivyobamba RTD enzi hizoo

Taarifa ya habari ilikuwa na watangazaji maalumu kwa matukio maalum. Nyerere akiteua au akitumbua itasomwa na David Wakati. Kama hayupo ni wakina Jacob Tesha, Juma Ngondae, Abdul Ngarawa au Mgosi Godfrey Mngodo. Na mara nyingi inakuwa saa 2 usiku.

Sent using Jamii Forums mobile app
 


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwendraa af unajua utoto mpaka miaka 17. Ulivyo kapenda sifa unataka kutuambia hiyo miaka tayari ulikuwa unatumia topaz...sifa zitakuua nyonyo

Sent using Jamii Forums mobile app
Nakumbuka kipindi hicho kulikuwa ma nyembe zinaitwa "Perma Sharp" kiwanda kilikuwa pale PUGU ROAD ambayo kwa sasa tunaita NYERERE ROAD, kiwanda hicho kilikuwa kinatazamana na kiwanda cha betri wakati huo kinaitwaNATIONAL, kwa kinaitwa PANASONIC.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wahengaa.. Idhaa ya Taifa ilikuwa inapiga nyimbo za kiswahili tu, idhaa ya biashara ndio ilikuwa inachanganya na miziki ya ki Zaire, hapa Lipua Lipua, Orch Veve, Kiam na nyinginezo, kweli maisha ni safari.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1. Tunakuletea Chakula na Lishe- Ranfred Masako
2. Wananchi Tujifunzeni Ushirika- Ibrahim Chemgege
3. Rushwa- Augustine Buluba
4. Jeshi letu la Polisi- Ramadhan Mhina
5. IDM Mzumbe- Zainabu Mwatawala
6. Bwana Umeme- ???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…