Waislamu bila kujali ni Wasunn,Wahabi,Washia,Wahamadia ni walewale! Wote wanatumia Quran ile ile na Sunna za mtume yule yule.
Ni hatari kwa ulimwengu huu.
Nipo Grupu la mashia,suni, masalafi na wahhabi
Hao jamaa Wana chuki sio ya nchi hii Tena wao kwa wao ,nimegundua Wana chukua
Soma hii ya 👇👇
KWANINI MAWAHABI HAWAPENDI KUNASIBISHWA NA JINA LA SHEKH WAO SHEKH MUHAMMAD BIN ABDILWAHAAB ?
Wapo wanaosema haifai kuwaita Mawahabi au Wahabiya kwasababu ni jina la Allaah.
Madai haya sio ya kweli kwasababu, kwanza Allaah ni AL WAHAAB. Kwahiyo hata mtu akiitwa Wahab sio tatizo kisheria.
Pili kuna dhehebu katika Ahli sunna linaitwa Dhwaahiriyah ambapo Allaah anaitwa AL DHWAAHIR. Lakini hakuna Shekh wa Kiwahabi aliekataza matumizi ya jina hili.
Wapo wanaosema kwanini wasiitwe Muhammadiya kwasababu jina la kwanza la Shekh ni Muhammad na la pili ndio Abdulwahaab.
Hoja hii sio sahihi kwasababu, hata majina ya wafuasi wa maimamu wetu wanne wa Fiqhi hawaitwi kwa majina ya kwanza ya maimamu hawa.
Hanafiyah
Hanbaliyah
Maalikiyah
Shaafiyah
Majina yote hayo sio majina ya kwanza ya maimamu wetu wa nne.
Naomba tusaidiane kutafuta sababu kwanini Mawahabi hawapendi kuitwa kwa jina hili.
Kwa mtazamo naona baadhi ya matukio ya Kihistoria ya Shekh Muhammad bin Abdilwahaab, yanawafanya wafuasi wake wasijiamini kwa jina la Shekh wao.
Shekh Ibn Baz anasema, daawah ya Shekh Muhammad bin Abdilwahaab imeelezwa wazi katika vitabu vyake. Moja ya kitabu alichokitaja hapo ni Al Duraru Saniyya Fi Ajwibat Al Najdiyya
Sasa katika kitabu hicho Shekh Muhammad bin Abdilwahaab amenukuliwa akisema maneno haya
(وأنا أخبركم عن نفسي والله الذي لا إله إلا هو، لقد طلبت العلم، واعتقد من عرفني أن لي معرفة، وأنا ذلك الوقت، لا أعرف معنى لا إله إلا الله، ولا أعرف دين الإسلام، قبل هذا الخير الذي من الله به؛ وكذلك مشايخي، ما منهم رجل عرف ذلك.فمن زعم من علماء العارض أنه عرف معنى لا إله إلا الله، أو عرف معنى الإسلام قبل هذا الوقت، أو زعم من مشايخه أن أحدا عرف ذلك، فقد كذب وافترى، ولبس على الناس، ومدح نفسه بما ليس فيه).
الدرر السنية في الأجوبة النجدية51/10
"Na mimi nawapa habari kuhusu nafsi yangu, naapa kwa jina la Allaah ambae hakuna apasae kuabudiwa kwa haki ila yeye, hakika nimetafuta elimu na nikaitakidi nina maarifa. Na mimi katika wakati huo nilikuwa sijui maana ya Laa ilaaha illa Allaah, wala nilikuwa sijui Uislamu, kabla ya kheri hii ambayo Allaah amenineemesha Na hivyo hivyo Mashekh wangu hakuna katika wao mtu aliekuwa anajua hayo (Maana ya Laa ilaaha illa Allaah na Uislamu). Na atakae dai miongoni mwa wanazuoni kwamba anajua maana ya Laa ilaaha illa Allaah au anajua maana ya Uislamu kabla ya wakati huu, au akadai miongoni mwa Mashekhe zake kwamba yupo yoyote anajua hilo (maana ya Laa ilaaha illa Allaah) basi atakuwa amezua na akawadanganya watu na amejisifu kuwa na elimu ambayo hakuwa nayo"
Kitabu: Al Duraru Saniyya Fil Ajwibat Al Najdiyya Juzuu ya 10 ukurasa wa 51.
Kwahiyo Shekh anaamini yeye ndio alikuja kuwafundisha Uislamu na maana ya Laa ilaaha illa Allaah, waislamu wote katika zama zake.
Na mtazamo huu ndio wameurithi Mawahabi wote, wanaamini waislamu wengi wamepotea isipokuwa wao.