Wahitimu wengi wanajutia kusoma chuo kikuu. Mzazi mwandalie mwanao Mtaji. Zama zimebadilika

Watu wapewe passport watafute fursa nchi nyingine
Ila sasa suala jingine linakuja ni elimu yetu hii 🥴 mtu mhitimu wa chuo ila kujieleza hata kwa kiswahili anashindwa
Leo umeweka comment mujarabu kabisa
Safi sana mkuu
Hapo kwenye passport muhimu saaana saaanaa
Kujieleza kutakuja hukohuko mbele
Nakuhakikishia ,mtu aliefika chuo kikuu akienda nje huko akakaa mwezi tu anaongea kimalkia fresh tu
Ila Sasa passport kupatikana inaonekana Kama anasa
Serikali ya ccm imejaa laana
 

Kenya wana export sana wafanyakazi majuu.. ila bongo tumelala tu
 
Wazazi wetu nao wanamchango mkubwa sana wa kuzorotesha maendeleo ya watoto wao. Wanachojua wao ni akishakusomesha amemaliza anakusukumia duniani ukatangetange utafute cha kufanya. Anasahau kuwa si kila mtu anajiweza kuanza mwenyewe matokeo yake wengine wanakuwa walevi wa pombe hadi kuharibikiwa, wanakuwa watumiaji wa dawa za kulevya na kadhalika yote ni kufeli kwa wazazi katika kuwasiliana na vijana wayajue matarajio yao.

Ni vema wazazi kusikilizana na vijana. Kuna muda inaweza kuwa ni swala la mtaji, kuna muda ni swala la social support tu ile ya encouragement na kadhalika.
 
Bora uache kuchangia tu, inakuwaje mtu unatupa kazi ya kusoma vitu unakosea neno baada ya neno? Yani ukiandika hupati muda wa kurudia kusoma kidogo ndio upost?
 
Bora uache kuchangia tu, inakuwaje mtu unatupa kazi ya kusoma vitu unakosea neno baada ya neno? Yani ukiandika hupati muda wa kurudia kusoma kidogo ndio upost?
Sina. Naona niache tu kwa kuwa napoteza muda hamna faida nayopata kuandika humu.
 
Mimi sijawahi kujuta kusoma chuo .... Kwakwel nakimbiza sana mtaaan had wanasema freemason...
 
Mnaolalamika kuhusu elimu ni wapumbavu mno. Ingekuwa elimu haina maana basi kina Dewji, GSM, na matajiri wengine wasingewapeleka watoto shule. Kama unajuta kwenda chuo basi wewe hata maisha ya kawaida tayari umefeli.
 
Si umuachishe shule sasa akaanze biashara azoee mapema
 
Ww kama haijakukimboa usiwe general kwamba wote haijawakomboa ni mindset yako ilipinda ikakataa kubadili mtazamo tangu unasoma had sa iz haikusaidii
Unazungumzia hii Elimu yetu ya kibongo?? Ama ya kule ulaya mkuu.
 
Si rahisi wazazi wa Kitanzania kuelewa,kutambua kuwa mambo yamebadilika hivyo ni vyema nao kubadilika.

Ni taifa la namna gani tunalo andaa ? Hatujafika hata mapinduzi makubwa ya kiteknolojia & kiviwanda lakini hali mbaya namna hii ? Inasikitisha
Tungekuwa tumefanya mapinduzi ya viwanda shida isingekuwa kubwa hivi
 
Watu wapewe passport watafute fursa nchi nyingine
Ila sasa suala jingine linakuja ni elimu yetu hii 🥴 mtu mhitimu wa chuo ila kujieleza hata kwa kiswahili anashindwa
Ww ndo huwez kujieleza acha kupotosha yaani morning speech, debate za secondary bado presentations chuo bado kuna platform nyingi chuoni za kutoa speech ushindwe kujieleza?

Makosa yako usifikiri na wengine wapo kama ww
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…