Wahitimu wengi wanajutia kusoma chuo kikuu. Mzazi mwandalie mwanao Mtaji. Zama zimebadilika

Wahitimu wengi wanajutia kusoma chuo kikuu. Mzazi mwandalie mwanao Mtaji. Zama zimebadilika

Nenda hospitali mkuuu. Eti unashika vyeti unafurahia hata kama havijakusaidia kupata ajira. Umesema mwenyewe mkuu kuwa unafurahia usinibadilishie kibao.
Sio tyuuh kufurahia, kuna muda navifuata niliko hifadhi navitazamaa afu naachia tabasamu mwanana,

Niko swafiiiii, poleeee yenu mnaolalama kwa kukosa ajira, sie wengine sio shda zetu.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kutokana na tulipianzia mjadala na jinsi ulivyoeleza hapa. Hio freedom of thought lazima ukaipate chuo kikuu ? Maana vyuo vyenyewe vinachagua tuvitu tuchache twa kumfundisha mtu. Kama ishu ni kupata mawanda mapana, elimu ya hivyo si imejaa mitandaoni ni kujipa muda na bando unasoma unachokitaka.
Wewe unaposema unaenda kupata freedom of thought akusaidie nini ? Naona umekwepa kujibu maswali yangu, inawezaje kuniaminisha kuwa una hio freedom of thought wakati unaepa maswali ?
Kwanza kabisa, mimi sijasema kuwa nina hiyo freedom of thought.

Pili, sikwepi maswali. Changamoto niliyonayo ni muda.

Swali lako la awali uliuliza maana ya freedom of thought na uhusiano wake na money creation.

Sasa hivi unauliza umuhimu wa kwenda chuo ili hali elimu iko mitandani.

Haya ndio baadhi ya maswali yako kama sikosei.

Mimi sina majibu sahihi sana, what am going to write down here is just an attempt to view your quiz in diverse perspectives.

Uhusiano kati ya elimu na money creation.

Elimu ni knowledge, and it is not power, The applied knowledge is the real power.

Kinachofundishwa mashuleni na vyuoni(ambacho mara nyingi hakihusiani na money creation) ni knowledge tu.

Ni logics. Ni IQ.

Money creation does not neccessarily depend on your IQ level but depends mostly on your Emotional intelligency, kitu ambacho hakipewi kipaumbele sana mashuleni.

So dont be surprised to find a broke proffesor and a very rich illiterate man.

Kuna kauli mbiu kwamba EDUCATION FOR LIBERATION, Liberation of what?

Of thought! Ni ukombozi wa fikra. Ni sawa na kula tunda la mti wa kati halafu ukajua mabaya na mema.

Alexander The Great alipofika katika kijiji cha Corinth alipokuwa anakaa Diogenes, mwanafalsafa wa kale wa Uyunani alimkuta amekaa kuota jua huku amezungukwa na mbwa zake.

Alexander The Great alimuuliza Diogenes, what can i do for you?

Haraka Diogenes alimwambia, Move aside you are blocking the sun!

Diogenes ndiye mwalimu wa Crates, aliyemfundisha Zeno, mwanzilishi wa falsafa ya ustoa (Stoicism)

Kwa hiyo utaona kwamba Diogenes alikuwa ni intellectual aliyeishi maisha ya ufukara kwa sababu he was not interested in wealth creation.

To be an intellectual or enlightened does not go hand in hand with becoming rich, the aim of education is to get wisdom, na ndio maana logo ya chuo kikuu cha DSM wanasema WISDOM IS FREEDOM, Hekima ni Uhuru and hence, kuwa na hekima sio lazima upate utajiri, hata kama Mfalme Selemani alipata. Kuna watu wengi wenye hekima na hawaoni kama utajiri ni wa muhimu hivyo.

Lengo la kusoma siyo utajiri. Na ninakubaliana falsafa ya Robert Kiyosaki, IF YOU WANT TO BE RICH, DONT GO TO SCHOOL.

Ni kweli elimu mitandaoni ipo, but, ili unufaike nayo, ni lazima uwe umesoma. Illiterate au darasa la 7, hawezi kunufaika na elimu ya mitandaoni.

Let me stop here for now!
And that was an attempt to discuss some of your questions.
 
Habari wadau.

Wazazi wengi tunasomesha watoto kwa kujibana, Tena shule za gharama. Tunakopa huku na huku tuwalipie ada. Nawakumbusha tu tukumbuke na kuwaandalia mitaji ya biashara wakimaliza kusoma.

Graduates wengi ambao wazazi wao hawajawapa mitaji wamekuwa wazururaji tu mitaani, walevi wenye msongo mkubwa wa mawazo.

Graduates ambao wapo vizuri ni wale ambao kwao wamepewa mitaji. Na wale wenye vipaji kama wasanii kina Bilnass.

Hizi ni comments za graduates wanaojutia kwenda chuo kikuu. Maoni haya wametoa baada ya graduates mmoja kulalamika degree yake haijamlipa. Bali ilimpotezea muda tu na kumpa ego ya kujiona class ya juu.


View attachment 3044026


View attachment 3044029


View attachment 3044032


View attachment 3044035

View attachment 3044029

View attachment 3044047


View attachment 3044048


View attachment 3044050

View attachment 3044050View attachment 3044137View attachment 3044136View attachment 3044135View attachment 3044134View attachment 3044133View attachment 3044132View attachment 3044131
Huo upuuzi niliisha acha,wanangu Primary anasoma English medium na Secondary wanasoma za kata.Pesa zao wa kulipia elimu isiyokuwa na future nawanunulia Viwanja na mashamba na mpaka sasa nina Viwanja zaidi ya kumi na naendelea kununua.Wakifika Chuo wasome Business Management na wasipofika watauza ardhi yao kupata mitaji.
Wazazi wanaumia sana kutusomesha kwa gharama alafu mwisho wa siku hola,watu wanapeana ajira kwa connection,niliapa sitaki watoto wangu wapitie msoto wa kukosa ajira kama Baba yao na kuishi maisha ya kuungau ga!!
 
Tatizo sio mtoto kupewa mitaji

Moja tuige wahindi,waarabu wapemba,wakinga na wachaga

Mzazi aanzishe biashara .Mtoto ashirikishwe kwenye biashara toka mdogo akimaliza elimu yeyote iwe msingi,sekondari au chuo level yeyote anaingia moja kwa moja kwenye biashara za familia

Pili kusoma ni uwekezaji kama uwekezaji mwingine wowote lazima kuangalia soko la ajira kimataifa.Kabla kusoma jiulize hii course ina soko kimataifa? Hasa nchi zilizoendelea.Ukisomea course ambayo soko la ndani tu shida ni upotezaji hela za uwekezaji wa kulipa ada .

Haitakiwi mtu kusoma kama mwehu ooh awe na digrii tu .Na sehemu nzuri ya kuanzia ni je hiyo digrii ina demand nje ya Tanzania?

Tatu unaangalia je Hiyo digrii nasoma kama vigezo hivyo viwili haipo je naweza kujiajiri mwenyewe hata kama ajira hamna?

Nne vigezo vyote vitatu kama havienei ni je yaweza saidia business za familia kusonga mbele? Mfano mzazi ana shule au hospitali au mabasi au malori au duka mtoto kwenda kusoma mfano Business administration marketing, uhasibu ,Logistics and Transport management nk course related to family business anakuwa yuko sahihi ili akasimamie na kukuza family business

Tatizo wengi husoma kama wehu tu hakai chini kuwaza future yake anataka iweje kabla kuwekeza kichwa chake kusoma digrii

Anasoma hana future vision ni kuwa come what may .I don't care.Matokeo mwishoni kelele kibao nina digrii na sijui pa kuipeleka

Mzazi husikiliza mtoto hajakosea kitu asilaumiwe anaamini mtoto anachotaka kusoma kajipanga hiyo future yake

Akiona tofauti hata yeye atashangaa kama mtoto anavyoshangaa kuwa ana digrii na hajui kwa kuipeleka
 
Ndio maana kila siku huwaga nawaambia msitumie mamilioni kusomesha watoto shule za ENGLISH mediums.
Huelewi kitu wewe shule nzuri hufundisha career path za English medium kwa watoto ndio maana wakiijua husoma sana ili wafaulu sana kuelekea mwelekeo wa career path waliofunzwa English medium ndio maana English medium hufaulisha sana sababu watoto wanakuwa inspired kwenye career path kuwa ukitaka kufikia huko unataka piga kitabu sana ufaulu masomo mojs mbili tatu nne nk

Hiyo huduma haipatikani shule za kayumba za kubeba vidumu na mifagio kwenda navyo shule
 
mbona Sijaona hapo aliyesoma engineering wala medicine ? Ninauliza tu ili kupata ufahamu
Hao wako vizuri tunakoelekea kuzuri na tatizo hili la ajira la waliomaliza digrii kukosa ajira litafikia tamati mbeleni

Watu mbeleni kabla kusoma chochote watakaa chini kutafakari kwanza nasoma ili iweje na future nataka kuwa nani na kuangalia options zote kabla kulipa ada ili akienda soma anajua kilichompeleka kusoma sio tu kutafuta karatasi la digrii aonekane kuwa naye anayo wakati akimaliza hiyo digrii hajui pa kuipeleka

Watasoma wale tu wanaojielewa kuwa akimaliza digrii ataipeleka wapi
 
MATOKEO YA UTITIRI WA VYUO!!!!!!Haya yote hayakuwepo chuo kikuu kilipokuwa kimoja au viwili Udsm na SUA. Shida imekuja baada ya kuletwa utitiri wa vyuo, kulikuwa na haja gani ya kuongeza vyuo vikuu wakati soko la ajira ni dogo, unazalisha mazao mengi kuliko walaji wachache, mazao yanaoza, university wangeenda wachache tu the best of the best wengine waishie form 4 certificate au diploma tu, hadi degree imeshuka thamani na heshima hadi degree zilizokuwa zikiheshimika sana zinadharaulika Sheria na Udaktari, watu wenye IQ za kawaida wanasoma, kuwa na PHD siku hz kawaida sana imekuwa.
 
Hao wako vizuri tunakoelekea kuzuri na tatizo hili la ajira la waliomaliza digrii kukosa ajira
Watu mbeleni kabla kusoma chochote watakaa chini kutafakari kwanza nasoma ili iweje na future nataka kuwa nani na kuangalia options zote kabla kulipa ada ili akienda soma anajua kilichompeleka kusoma sio tu kutafuta karatasi la digrii aonekane kuwa naye anayo wakati akimaliza hiyo digrii hajui pa kuipeleka

Watasoma wale tu wanaojielewa kuwa akimaliza digrii ataipeleka wapi
Well said mkuu nimepata kitu
 
Back
Top Bottom