Wahuni waiba engine ya lori lililotumbukia Mto Wami

Wahuni waiba engine ya lori lililotumbukia Mto Wami

Watafanyaje yao huku tukio zima likirekodiwa tangia wapewe amri na mkuu wao?

Wa kwanza kuhisiwa kama ni hujuma ni ile timu ya kwanza iliyodai jambo hilo haliwezekani, kumbe linawezekana tena kiurahisi kabisa!

Ndiyo maana wakatoa mkadirio wa mbali kuvuruga ushahidi.

Nilistaajabu sana kwa kada hiyo ya uokoaji kutoa tathimini yao ya kizembe zembe kama hiyo, nikawa najiuliza maswali yasiyo majibu!

Hata kama injini na kebeni viling'oka kwenye msukosuko vingelikutwa jirani na hilo chesesi, maana maiti ilikwama humo na ikaopolewa!

Vyombo vinavyohusika vikifuatilia kuanzia staff waliopo hapo idara ya maji, wakiwemo wavuvi ukweli utajulikana tu na kuna watu wataibeba hiyo kashifa.
Pia walisema hawawezi kulitoa hilo lori sababu ya uzito wakidai lina mizigo,

Chakushangaza JWTZ walivyolitoa hawajakuta mzigo wowote.
 
Kwahiyo lile lori lililotumbukia Mto Wami ndio injini na kichwa chake mamba watu wamekula ama[emoji848]
 
Kila nikisikia habari hizi, natamani kuona picha zake...

Mwenye picha naomba utupie basi..
 
1. Siyo ajari. ni ajali. Kuandika ''ajari'' waachie watoto wa darasa la kwanza wanaojifunza kuandika.
2. Ku-fail kwa breki kunasababishwa na ubovu wa gari. Kuendesha gari bovu ni uzembe.
3. Gari lilikuwa bovu kabisa. Wahusika walitakiwa ku-face sheria na siyo kuonewa huruma.
4. Kusema kuwa ''kama lilikuwa bovu toka lilipotoka hadi linapata ajari (ajali) lilipita wapi?''inaonyesha kiwango cha IQ yako.
Kama wee mwenye IQ, kubwa ndio mwenye mawazo hayo ya kufikia conclusion, kwenye mambo ambayo yanahitaji uchunguzi kwanza kubaini hasa tatizo ni nini, nasema bora nibaki na IQ, yangu hii ndogo lakini yenye utambuzi.
 
kama wana wameweza kufua ile engine na kuondoka nayo..basi tuna vijana wanavipaji vya ajabu hapa nchini....na pengine hao wana hata vifaa vya kuzamia hawana..na maji yalivyo machafu sasa..hatari sana

Hakuna engine iko huko huko chini
 
Hiyo injini na cabin zilichomoka. Hili naweza kulisema nikiwa na uhakika kabisa. Vilichomoka kwa sababu lori liligonga nyuma ya gari jingine na kuanguka urefu mkubwa. Pia ubovu wa lori unachangia. Injini na cabin vinaweza kuja kuonekana baadae sana, baada ya maji kupungua kabisa. Pale ni sehemu iliyo busy muda wote na siyo rahisi watu kupata muda wa kuzama ndani ya maji mpaka wafungue injini na kuitoa. BTW huyu mama alitakiwa alishtakiwe kwa kuweka gari bovu barabarani. Huu mlori wake unaonekana ulikuwa mbovu kabisa na uliungwa ungwa na na mafundi wa uchochoroni ndiyo maana breki zilifeli na injini kuchomoka kwa urahisi.
Maiti ya dereva iliopolewa ndani ya cabin, vipi kuhusu hilo?
 
Mkuu, ebu kwa akili ya kawaida jaribu kifikiria uzito wa Geabox na Engine. Kisha jiulize Cabin mbona haijatoka na chassis??

Kisha nikujibu tu kwamba bolts zinazo kamata Engine mauntain ni nne pekee zenye unene wa 16 millimeters.

Gearbox inaunganishwa na bolts 10 zenye unene wa 10 millimeters kutoka kwenye flyn wheel pamoja na pressure, inayo ungana na bell housing ya aluminum.
Sasa.....

Ile impact ya force plus weight kutoka kule juu darajani ingeweza kuhimili kuto kusambaa kwa gari lile...??
Binadamu anao uwezo mkubwa wa kufanya jambo lisilowezekana kwa urahisi akidhamilia.Hiyo engine,cabin vimeibiwa na watu,amini nakwambia.
Ile team ya mwanzo iliyodai kushindwa kulitoa hilo gari,wezi wametokea humo.
 
Back
Top Bottom