Waimba kwaya wanaokata miuno na kunengua kanisani wanamsifu Mungu kweli?

Without a video,this post is nuthin'
 
Heshima huanzia kwenye mavazi,mtu hawezi kwenda kwenye Nyumba ya ibada na mavazi yasiyo na staha,

Unakuta mtu ana vaa kiheshima akienda ukweni ila akienda kwenye Nyumba ya ibada ana vaa kihasara! Haya ni maajabu nayo.
 
Yote haya ikiwemo dansi za kukata viuno zimeingizwa makanisani Ili kuwapotosha watu. Viongozi wa dini nao wanaogopa kuongea ukweli juu ya mavazi yasiyostaha kuogopa kuwakwaza waumini watawakimbia sadaka zitapungua. Sketi fupi, suruari, jeans, t shirt, ndala, skuna, car wash, tracksuit,pajama,kofia,nguo za mapicha sio mavazi ya kuvaa ibadani, watu wanachanganya mavazi ya disco, beach , michezo na mavazi ya ibadani.
Hongera waislamu kanzu na baibui ni vazi la ibada.
Mungu anaangalia roho na sio mwili ni fundisho la uongo kabisa na hii ni Kazi ya freemason waipenyeza kwa watumishi wao kupitia mitume na manabii feki Ili kuliangusha kanisa
 
Ahahaha

Nielekeze mahali lilipo ilo kanisa nikapate upako
 
Waache wamtukuze Bwana Mungu kwa vinubi na vinanda na hata kutikisa miili yao.Mbona mnawahukumu hivyo.Let them be!
 
mbona ile nyimbo ya "Tumeuona mkono wake Bwana" inapigwa kila club au mkono wa dj ndo mkono wa bwana?
 
Mungu anapenda uwe na energy na furaha ndio anatenda vema
 
Mungu anaangalia moyo wako na matendo yako na sio mavazi, angekua anaangalia mavazi basi magaidi wote wangeenda mbinguni maana huwa wanajifunika mpaka uso na macho

Tujitahidi kutenda matendo mema na kuweka mioyo yetu safi, unaweza kuvaa gauni refu panaaa kama gunia halafu usiku ni pakashume unaeruka na ungo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…