Waimba kwaya wanaokata miuno na kunengua kanisani wanamsifu Mungu kweli?

Kweli magugu yanaota katitati ya nganooo safi
 
Kwani viuno vimeumbwa na nani?
 
Wewe nikikupa pensi nyanya utavaa? Najua hutavaa kwa sababu sio vazi la mwanaume
 
Wewe nikikupa pensi nyanya utavaa? Najua hutavaa kwa sababu sio vazi la mwanaume


Mahala ambapo Neno limeweka wazi kuhusu nini kifanyike ni vyema tukatii badala ya kujaribu kutafuta excuses mbalimbali.

Imeandikwa; “ utii ni bora kuliko sadaka “

Hicho ulichoandika ndicho mojawapo ya excuse ambayo wengi hupenda kutafuta kujifichia humo!

Wengine watakwambia kuna suruari za kike na kiume lakini yote ni kutafuta excuse coz kwenye jamii tuliyonayo vazi la Mwanaume linajukana ni lipi hata mtoto Mdogo anafahamu.!

Halafu wengine tukajadili mambo haya hupata makasiriko ni kawaida sana kuona watu wa namna hiyo!
 
Unakuta mtu amevaa kama yuko night club [emoji848][emoji848][emoji848]

Na ni kwa bahari isiyo nzuri kwenye mahubiri ya siku hizi wahakemei kuhusu mavazi ya kihuni!

Wewe vaa utakavyo hata kama utaonekana kama aendaye night club ni Sawa hakuna wa kukukemea ilimradi uende na sadaka yako tu [emoji108][emoji108]

Mahubiri ambayo yameshika kasi na hufundishwa mara kwa mara siku hizi ni kuhusu utoaji sadaka!

Ya Utaua na ufalme badae!
 
Siyo siku hizi,walokole 1998 huko nilikokua,beat ya bongoman wanavisha injili Kisha wananengua jukwaani
 
Je haikuandikwa nabii alicheza mpaka mavazi yakamvuka? Na sherehe ilichukua siku 7 au wewe una bible yako ilio tofauti na ninayo isoma Mimi?. Acha mabo ya wajenzi huru Ile ni office kama office zingine zilivyo au hujui makampuni ya ujenzi ya wageni yalio jaa hapa Tz?.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Popote milipo mkizungumzia habari za uzima wa mbinguni basi tambueni na mimi nipo, ikiwa mpo 2 au zaidi nami nitakuea katikati yenu. Kucheza kwa mtumishi wa Mungu mbele ya waabudu tafsiri yake ni kumtukuza mungu na kuirejesha sifa zake.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Mungu akubariki sana.

Uzi umejibiwa kiitifaki na kwa mifano mbali mbali.

Mwenye macho na ashuhudie Roho Mtakatifu awaambia Mataifa kupitia Jackwillpower.
 
Ni sawa kabisa na inapendeza sana
 
“tena Walawi waimbaji, wote pia, yaani Asafu, na Hemani, na Yeduthuni, na wana wao, na ndugu zao, hali wamevaa kitani safi, wenye matoazi na vinanda na vinubi, wamesimama upande wa mashariki wa madhabahu, na pamoja nao makuhani mia na ishirini wakipiga panda😉

— 2 Mambo ya Nyakati 5:12 (Biblia Takatifu)



Ufunuo wa Yohana 15 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
² Tena nikaona kitu kama mfano wa bahari ya kioo iliyochangamana na moto, na wale wenye kushinda, watokao kwa yule mnyama, na sanamu yake, na kwa hesabu ya jina lake, walikuwa wamesimama kando-kando ya hiyo bahari ya kioo, wenye vinubi vya Mungu.
³ Nao wauimba wimbo wa Musa, mtumwa wa Mungu, na wimbo wa Mwana-Kondoo, wakisema, Ni makuu, na ya ajabu, matendo yako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi; Ni za haki, na za kweli, njia zako, Ee Mfalme wa mataifa.
 
Wasabato walidecide kwamba wasicheze kabisa. Kongole kwao.

Na madhehebu mwengine waliomua kucheza wacheze wanavyojisikia. Msikae mnapangia watu jinsi ya kucheza.
 
kucheza kuna kipimo?

Tupe kipimo basi
 
ATHARI ZA KUCHEZA MBELE ZA MUNGU.

1. DHARAU [emoji116]

2 SAMWELI 6:16.
Ikawa, sanduku la BWANA lilipoingia mji wa Daudi Mikali, binti Sauli, akachungulia dirishani, akamwona mfalme Daudi akiruka-ruka na kucheza mbele za BWANA; akamdharau moyoni mwake.

2. KUONEKANA MPUMBAVU (BARADHULI) [emoji116]

2 SAMWELI 6:20.
Ndipo Daudi akarudi ili awabarikie watu wa nyumbani mwake. Na Mikali, binti Sauli, akatoka nje aende kumlaki Daudi, naye akasema, Mfalme wa Israeli alikuwa mtukufu leo namna gani, akijifunua mwili wake mbele ya vijakazi vya watumishi wake, mfano wa watu baradhuli mmojawapo, ajifunuavyo mwili wake mbele ya watu, asipokuwa na haya!

3. NI UPUUZI NA MUNGU ATAADHIBU "AMOSI 5." [emoji116]

AMOSI 6:5.
Ninyi mnaoimba nyimbo za upuzi pamoja na sauti ya vinanda, na kujifanyizia vinanda vya namna nyingi, kama vile Daudi.
 
Wasabato walidecide kwamba wasicheze kabisa. Kongole kwao.

Na madhehebu mwengine waliomua kucheza wacheze wanavyojisikia. Msikae mnapangia watu jinsi ya kucheza.
Wasabato hawajiamulia bali ni maagizo ya Mungu kupitia Biblia.

SOMA UJUMBE WOTE NO 49.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…