Kulingana Na Biblia tukiacha Quran (Tuliipumzisha)..
Chuki ya Nguruwe Inatoka Huko..Mnyama aliyeandikwa Ni chukizo kwenu Unamzungumziaje?
1. Mambo ya Walawi 11:7-8
"Nguruwe, kwa kuwa ana kwato, tena kwato zake zimegawanyika katikati, lakini hacheui; yeye ni najisi kwenu. Nyama yao msile, wala mizoga yao msiiguse; hao ni najisi kwenu."
2. Kumbukumbu la Torati 14:8
"Na nguruwe, kwa kuwa ana kwato lakini hacheui, yeye ni najisi kwenu; msile nyama yao, wala msiiguse mizoga yao."
3. Isaya 65:2-4
"Nimeinyosha mikono yangu mchana kutwa kwa watu waasi, waendao katika njia isiyo njema, wakifuata mawazo yao wenyewe... watu wale wanaokaa katika makaburi, na kulala katika mahali palipofichika; wale walao nyama ya nguruwe, na supu ya vitu vichukizao vi katika vyombo vyao."
4. Isaya 66:17
"Wale wajitakasao na kujisafisha katika bustani, wakimfuata mmoja aliye katikati yao, wakila nyama ya nguruwe yenye machukizo, na panya, wataangamizwa pamoja, asema Bwana."
Torati ilijumuisha mambo mengi ya desturi na maagizo ya Mungu, ndiyo maana Kristo Masiha aliyependezwa na Baba kuliko manabii wote, alikuja kuikamilisha.
Sikuja kutangua/kuifuta torati bali kuikamilisha:
1. Mat: 5: 43-46
Imeandikwa wapendeni marafiki zenu, wachukieni maadui zenu, mimi nawaambia wapendeni maadui zenu kwa maana mkiwapenda tu marafiki zenu na kuwachukia maadui zenu mnatofautiana na nini na wake wasiomjua Mungu?
2. Math 5:38.
Imeandikwa jino kwa jino, jicho kwa jicho, lakini mimi nawaambieni usimlipizie kisasi mtu mbaya.
NB: Utimilifu wa kila amri ya torati upo katika Kristo Yesu, aliyrkuja kuikamilisha kwenye mapungufu yote.
Ukitaka kujua kuhusu vyakula, sikiliza mtimilifu wa torati ananena nini juu ya chakula.
MATHAYO 15
1Kisha Mafarisayo na waalimu wa sheria wakafika kutoka Yerusalemu, wakamwendea Yesu, wakamwuliza, 2“Kwa nini wanafunzi wako hawajali mapokeo tuliyopokea kwa wazee wetu? 3Yesu akawajibu, “Kwa nini nanyi hamjali sheria ya Mungu ila mnapendelea mapokeo yenu wenyewe?
7Enyi wanafiki! Isaya alitabiri sawa kabisa juu yenu:
8‘Mungu asema: Watu hawa huniheshimu kwa maneno tu,
lakini mioyoni mwao wako mbali nami.
9Kuniabudu kwao hakufai, maana mambo wanayofundisha ni maagizo ya binadamu tu.
(Marko 7:14-23)
10Yesu aliuita ule umati wa watu, akawaambia, “Sikilizeni, mkaelewe! 11Kitu kinachomtia mtu unajisi si kile kiingiacho kinywani, bali kile kitokacho kinywani. Hicho ndicho kimtiacho mtu unajisi.”
12Kisha wanafunzi wakamwendea, wakamwambia, “Je, unajua kwamba Mafarisayo walichukizwa waliposikia maneno yako?” 13Lakini yeye akawajibu, “Kila mmea ambao Baba yangu aliye mbinguni hakupanda, utangolewa. 14Waacheni wenyewe! Wao ni vipofu, viongozi wa vipofu; na kipofu akimwongoza kipofu, wote wawili hutumbukia shimoni.” 15Petro akasema, “Tufafanulie huo mfano.” 16Yesu akasema, “Hata nyinyi hamwelewi? 17Je, hamwelewi kwamba kila kinachoingia kinywani huenda tumboni na baadaye hutolewa nje chooni? 18Lakini mambo yatokayo kinywani hutoka moyoni, na hayo ndiyo yanayomtia mtu unajisi. 19Maana moyoni hutoka mawazo ya uuaji, uzinzi, uasherati, wizi, ushahidi wa uongo na kashfa.