Waislamu nijibuni maswali haya kuhusu Iftari

Waislamu nijibuni maswali haya kuhusu Iftari

Lengo kuu la Iftar ni kuweza kuwasaidia wale wote waislam waliofunga na hawana uwezo wa kupata ama kununua Iftar, lkn tunachokiona ktk karma hizi tulizonazo ni vichekesho Kwa kweli, hivi uliona wapi kisima chenye chemchem kikajazwa maji? Eti unaalika watu wanaojiweza ndiyo wanakuja kwenye Iftar, walengwa waliopaswa kuwepo hatuwaoni kwenye hiyo Iftar, Mimi naweza kusema hao wanaandaa hizo Iftar wengi wao sio Waislam, maana Mwislam hawezi akanda Iftar halafu awaite matajiri tena hawakufunga ili wake kufuturu huu ni ujinga wanapaswa kupewa Elimu, ikumbukwe kwamba Iftar sio sherehe useme uwalike watu wasio na sifa za kualikwa, watu wanapaswa kuisoma dini ili tuondoke katika giza na kuisoma Nuru, Wabillah Tawafique. K
Iftar ya siku hz ni connection na ndio maaana hata mualiko wake ni ki connection connection
 
LENGO la kufuturisha ni nini? Ni kuwapa FUTARI wasiojiweza au NI kulisha wasanii WA kizazi kipya na machawa?

Inakuaje kunaandaliwa FUTARI halafu yanayoongelewa hapo ni mambo ya MPIRA WA miguu? (mpira si Haramu?) au kufuturisha ni kuandaa chakula halafu mnakua mnakula huku mnapiga story zozote zile hata za vitu vya Haramu kama mpo kijiweni?

Mnasema Mziki WA kizazi kipya unaosifia ngono na kucheza uchi NI dhambi, sasa mbona mkialikwa kwenda Kula (kufuturu) na haohao wasanii wanaoimba Mziki WA kidunia mpaka viongozi wenu wanaenda kula? Mnakulaje chakula kinachotokana na pesa za Haramu?

Yani mnaalika watu wenye pesa zao waje wafuturu (SIO wasiojiweza!), na mkiwa huko hamzungumzii mambo ya Imani labda kumrudia Mungu au nini NI watu wanapitisha mambo Yao, Mpira, Sasa au Biashara.

Hongereni Sana wakristo, mfungo wenu umekua SIO wa maonyesho, hapa sasa ndio tunapata picha Dini ipi NI ya ukweli.
Waislam wapo arabuni sio bongo
 
Ametuelekeza Paroko wetu hapo juzi, kuwa Kwaresma ni kujinyima jambo ambalo ni la kawaida ila lisilo la lazima sana kisha fedha za gharama zilizookolewa apewe au anunuliwe mahitaji muhimu mtu mwenye changamoto na muhitaji.

Mfano, ukiamua kuokoa fedha kwa kutokula mlo wa mchana, au kwa kutumia daladala badala ya kujaza mafuta gari yako, au kwa kutoenda matembezi nje (kutoka out), au kwa kutolipia channel za ziada, na vitu vingine vya ziada visivyokuathiri ukivikosa, basi fedha ulizookoa ukawape au ukawanunulie vitu wahitaji (na sio kuwanunulia futari aka kuwafuturisha maana yawezekana sio hitaji lao), basi huko ndiko kunabeba tafsiri ya kufunga.

Ikitokea katika kipindi cha Kwaresma umeokoa sh. 350,000/= mfano, na ukazitumia kumkatia bima ya afya mhitaji mmoja labda na mwanaye, itakayowasaidia matibabu ya mwaka mzima, huko ndiko kufunga Kwaresma.

Mifano ni mingi, lakini akasema kujinyima kwako utakakochagua hakutakiwi kuathiri shughuli zako za uzalishaji, mfano umejinyima mlo wa mchana halafu unaishia kulala kwa kushindwa kuhimili njaa, au umeamua kutoweka mafuta katika gari halafu ndio unachelewa kazini nk, hiyo haitakiwi.
 
Mkuu Uislam una misingi, kanuni na Taratibu zake hayo unayo yaona ni Maonesho ya vyakula na kuonesha ufahari wao wa kula hakuna iftrar hapo lengo la funga ya Radhani ni kumjenga Muumin awe na moyo wa huruma na kusaidia kwa watu wasio na uwezo hata wa kupata mlo mmoja kwa siku aendelee kusaidia sio Ramadhan tu hata baada ya Ramadhan hilo ndio lengo, ni Kujenga Mapenzi baina yetu.
 
Lengo la kufuturisha ni kufuturisha,haijarishi una mfuturisha nani,kikubwa umefuturisha!

Kwanini uwaite binadamu wenzio chawa? Kwani kupenda walichoamua kukipenda ni kosa ila ulichopenda wewe ndio sawa?

Kwani wakati wa futari inawalazimu waongelee nini? Mpira kama mchezo si haramu kuucheza,kuuongelea hata kuutazama!

Kwa hiyo ulitaka mtu akialikwa asiende kisa aliyemualika ni msanii? Huhisi kama kwenda kwao kunaweza kuwa sababu ya huyo msanii kufikiria kubadilika? Maana hata muhamad alilelewa na hakuwatenga wasiomuamini,hata yesu alikula na kupakwa mafuta na kahaba.kwanini wewe unataka wawatenge hao unaohisi ni wadhambi?

Aliyekwambia wasiojiweza hawafuturishwi ni nani? Umetembelea vituo vingapi vya watoto yatima,wazee,magereza na nyumba za masikini wakakwambia hawana futari?

Umefanya jambo jema kuwapongeza wakristo,maana unafunga na una uhakika kuwa wanafunga na wanafanya kwa usahihi yote uliyokandia upande mwingine! Basi shikilia imani yako achana na imani isiyokuhusu!
Umeandika kwa uchungu sana huku ukilia na kububujikwa na machozi.
 
Thibitisha kuwa wanatumia fedha za serikali,kwani wao hawana pesa zao mpaka useme wanatumia pesa za serikali? Kufuturisha sio kujenga barabara au hospital kwamba inakubidi uwe bilionea ndio ufanye hivyo.hata wewe unaweza futurisha uwapendao!

Kuwazushia watu wanaojumuika na watu kwa upendo wao ili kujenga mahusiano mazuri na watu bila kuwa na hata robo ya ushahidi kama sio chuki na kuchafuana tu ni nini?

Unaposema misingi ya dini ya kiislam inachezewa unataka kusema wewe unaijua zaidi misingi hiyo kuliko wenye dini yao?
Kuna dini inayozuia watu kujumuika pamoja wakiwa na jambo lao jema?

Unapozungumzia kasoro unamaanisha nini? Kwani wewe unayefunga kwaresma umekamilika kiasi cha kuona kasoro za waliofunga ramadhani?
Kuna roho flani inakusumbua,ndio maana huoni uzuri kwenye mambo mema! Shika imani yako waache na imani yao!

halafu hata yesu ameshauri juu ya hiyo tabia,akasema kabla ya kuhangaika na boriti jichoni kwa mwenzio anza kwanza na banzi lako jichoni mwako! Jichunguze hii ni kwaresma,je umefunga? Unatengeneza na mungu wako? Je unatengeneza na jamii yako? Ukifanya hivyo utakosa muda wa kuhangaika na yasiyo kuhusu! Na roho yako itakuwa na amani.

Nimekuuliza hata yesu alilisha watu hadharani wakala hadi wakasazaje,na yeye alikuwa anaichezea dini?
Alijumuika na watu nyumbani kwa zakayo,aliwapenda wakosefu,hadi kupakwa mafuta na kahaba je,na yesu alikuwa anafanya show off kama ulivosema?

Halafu uwe una jibu hoja
Kwa hiyo unataka niweke hapa invoice ya ofisi tuliyomlipa caterer baada ya kuandaa futari kwa maelekezo ya kiongozi wangu.
Na unataka kusema Rais anavyofuturisha waislamu anatumia fedha zake za mfukoni kwake.
Misingi ya kiislamu inakiukwa kwani dhama nzima ya kuandaa futari ni mtu mwenye uwezo wake anaamua kuwakarimu waislamu wenzake waliofunga wasiokuwa na uwezo waweze kufuturu baada ya kufunga.
Sasa fikiria futari inaandaliwa na mkristo wanaalikwa kufuturu matajiri wakristo na waislamu wengine hata hawajafunga hapo ni ukiukwaji mkubwa wa misingi ya uislamu kuhusu iftar .
Mimi nimefunga kwaresma sili chakula mchana ,situmii pombe, sitaki kukasirika kipindi hiki na pia ninasali na kusoma vitabu vya dini muda mwingi zaidi
 
Mkuu Uislam una misingi, kanuni na Taratibu zake hayo unayo yaona ni Maonesho ya vyakula na kuonesha ufahari wao wa kula hakuna iftrar hapo lengo la funga ya Radhani ni kumjenga Muumin awe na moyo wa huruma na kusaidia kwa watu wasio na uwezo hata wa kupata mlo mmoja kwa siku aendelee kusaidia sio Ramadhan tu hata baada ya Ramadhan hilo ndio lengo, ni Kujenga Mapenzi baina yetu.
Umeongea ukweli ninaoujua mimi .
Much respect kwako mkuu
 
LENGO la kufuturisha ni nini? Ni kuwapa FUTARI wasiojiweza au NI kulisha wasanii WA kizazi kipya na machawa?

Inakuaje kunaandaliwa FUTARI halafu yanayoongelewa hapo ni mambo ya MPIRA WA miguu? (mpira si Haramu?) au kufuturisha ni kuandaa chakula halafu mnakua mnakula huku mnapiga story zozote zile hata za vitu vya Haramu kama mpo kijiweni?

Mnasema Mziki WA kizazi kipya unaosifia ngono na kucheza uchi NI dhambi, sasa mbona mkialikwa kwenda Kula (kufuturu) na haohao wasanii wanaoimba Mziki WA kidunia mpaka viongozi wenu wanaenda kula? Mnakulaje chakula kinachotokana na pesa za Haramu?

Yani mnaalika watu wenye pesa zao waje wafuturu (SIO wasiojiweza!), na mkiwa huko hamzungumzii mambo ya Imani labda kumrudia Mungu au nini NI watu wanapitisha mambo Yao, Mpira, Sasa au Biashara.

Hongereni Sana wakristo, mfungo wenu umekua SIO wa maonyesho, hapa sasa ndio tunapata picha Dini ipi NI ya ukweli.
Ndio unafiki wenyewe huo.
 
Umehoji kitu kizuri sana… kufuturisha kuliko elekezwa c uko unako kuona kutoka kwa jamaa zetu wapenda sifa,,, makundi yaliyo tajwa yko wazi kwa lugha rahisi futulisha wenye mahitaji,, unayo yaona kutoka kwa wapenda sifa za kukutana kwa munasaba wa iftar ni wahuni tu…muone mwinyi rais wa znz anavyo futurisha au Ally kiba pia..Achana na izi za sifa za mjini buda.
 
Hio ni kama dinner tu au gathering ya watu wenye kariba moja ambayo fursa imepatikana katika mwezi huu wa Ramadhani
Ila wapo baadhi katika hao tangia day 1, daily wanalisha maskini wasiojiweza sema hawafanyi hio mikusanyiko nao tu
 
Kwa hiyo unataka niweke hapa invoice ya ofisi tuliyomlipa caterer baada ya kuandaa futari kwa maelekezo ya kiongozi wangu.
Na unataka kusema Rais anavyofuturisha waislamu anatumia fedha zake za mfukoni kwake.
Misingi ya kiislamu inakiukwa kwani dhama nzima ya kuandaa futari ni mtu mwenye uwezo wake anaamua kuwakarimu waislamu wenzake waliofunga wasiokuwa na uwezo waweze kufuturu baada ya kufunga.
Sasa fikiria futari inaandaliwa na mkristo wanaalikwa kufuturu matajiri wakristo na waislamu wengine hata hawajafunga hapo ni ukiukwaji mkubwa wa misingi ya uislamu kuhusu iftar .
Mimi nimefunga kwaresma sili chakula mchana ,situmii pombe, sitaki kukasirika kipindi hiki na pia ninasali na kusoma vitabu vya dini muda mwingi zaidi
Weka huo ushahidi,maana hizo ni tuhuma na nimatumizi mabaya ya fedha za umma.ukifanya hivyo wahusika wataitwa hapa,waone ili wachukue hatua stahiki,na hilo ni moja ya faida ya jukwaa hili!
 
Umeandika kwa uchungu sana huku ukilia na kububujikwa na machozi.
Shida iko mahali,kuna baadhi ya watu wanataka wawapangie watu maisha,yaani mtu anataka watu waishi anavyotaka yeye,hata kama maisha ya hao watu hayampunguzii wala kumuongezea chochote,hii sio kwenye masuala ya imani tu,hata kwenye maisha ya kawaida.yaani mtu hujiona yeye yuko sahihi juu ya wote,na mawazo na matamanio yake ndio anataka watu wayaishi!
Mtu anasumbuliwa hadi na vyakula vya watu,ni tatizo hilo!
Hii ni dunia ya uhuru wa kila kitu,kiimani kibiashara n.k.
Kila mtu afuate njia yake kama hakuna sheria anayovunja.
Ndio maana wahenga waliuliza,"pilipili usiyoila yakuwashia nini?"
 
Back
Top Bottom