Waislamu nijibuni maswali haya kuhusu Iftari

Iftar ya siku hz ni connection na ndio maaana hata mualiko wake ni ki connection connection
 
Kuhusu dini tafadhali zingatia kuwa Technology inaisogelea Dini kwa kasi sana.
 
Waislam wapo arabuni sio bongo
 
Ametuelekeza Paroko wetu hapo juzi, kuwa Kwaresma ni kujinyima jambo ambalo ni la kawaida ila lisilo la lazima sana kisha fedha za gharama zilizookolewa apewe au anunuliwe mahitaji muhimu mtu mwenye changamoto na muhitaji.

Mfano, ukiamua kuokoa fedha kwa kutokula mlo wa mchana, au kwa kutumia daladala badala ya kujaza mafuta gari yako, au kwa kutoenda matembezi nje (kutoka out), au kwa kutolipia channel za ziada, na vitu vingine vya ziada visivyokuathiri ukivikosa, basi fedha ulizookoa ukawape au ukawanunulie vitu wahitaji (na sio kuwanunulia futari aka kuwafuturisha maana yawezekana sio hitaji lao), basi huko ndiko kunabeba tafsiri ya kufunga.

Ikitokea katika kipindi cha Kwaresma umeokoa sh. 350,000/= mfano, na ukazitumia kumkatia bima ya afya mhitaji mmoja labda na mwanaye, itakayowasaidia matibabu ya mwaka mzima, huko ndiko kufunga Kwaresma.

Mifano ni mingi, lakini akasema kujinyima kwako utakakochagua hakutakiwi kuathiri shughuli zako za uzalishaji, mfano umejinyima mlo wa mchana halafu unaishia kulala kwa kushindwa kuhimili njaa, au umeamua kutoweka mafuta katika gari halafu ndio unachelewa kazini nk, hiyo haitakiwi.
 
Ibada zinageuzwa kua Anasa, Futari iliyobora ni Tende hayo mengine ni dinner tu tunajipangia kufanya Israfu
Kwa nini tende ndio futari iliyo bora??
 
Mkuu Uislam una misingi, kanuni na Taratibu zake hayo unayo yaona ni Maonesho ya vyakula na kuonesha ufahari wao wa kula hakuna iftrar hapo lengo la funga ya Radhani ni kumjenga Muumin awe na moyo wa huruma na kusaidia kwa watu wasio na uwezo hata wa kupata mlo mmoja kwa siku aendelee kusaidia sio Ramadhan tu hata baada ya Ramadhan hilo ndio lengo, ni Kujenga Mapenzi baina yetu.
 
Umeandika kwa uchungu sana huku ukilia na kububujikwa na machozi.
 
Kwa hiyo unataka niweke hapa invoice ya ofisi tuliyomlipa caterer baada ya kuandaa futari kwa maelekezo ya kiongozi wangu.
Na unataka kusema Rais anavyofuturisha waislamu anatumia fedha zake za mfukoni kwake.
Misingi ya kiislamu inakiukwa kwani dhama nzima ya kuandaa futari ni mtu mwenye uwezo wake anaamua kuwakarimu waislamu wenzake waliofunga wasiokuwa na uwezo waweze kufuturu baada ya kufunga.
Sasa fikiria futari inaandaliwa na mkristo wanaalikwa kufuturu matajiri wakristo na waislamu wengine hata hawajafunga hapo ni ukiukwaji mkubwa wa misingi ya uislamu kuhusu iftar .
Mimi nimefunga kwaresma sili chakula mchana ,situmii pombe, sitaki kukasirika kipindi hiki na pia ninasali na kusoma vitabu vya dini muda mwingi zaidi
 
Umeongea ukweli ninaoujua mimi .
Much respect kwako mkuu
 
Ndio unafiki wenyewe huo.
 
Umehoji kitu kizuri sana… kufuturisha kuliko elekezwa c uko unako kuona kutoka kwa jamaa zetu wapenda sifa,,, makundi yaliyo tajwa yko wazi kwa lugha rahisi futulisha wenye mahitaji,, unayo yaona kutoka kwa wapenda sifa za kukutana kwa munasaba wa iftar ni wahuni tu…muone mwinyi rais wa znz anavyo futurisha au Ally kiba pia..Achana na izi za sifa za mjini buda.
 
Hio ni kama dinner tu au gathering ya watu wenye kariba moja ambayo fursa imepatikana katika mwezi huu wa Ramadhani
Ila wapo baadhi katika hao tangia day 1, daily wanalisha maskini wasiojiweza sema hawafanyi hio mikusanyiko nao tu
 
Weka huo ushahidi,maana hizo ni tuhuma na nimatumizi mabaya ya fedha za umma.ukifanya hivyo wahusika wataitwa hapa,waone ili wachukue hatua stahiki,na hilo ni moja ya faida ya jukwaa hili!
 
Umeandika kwa uchungu sana huku ukilia na kububujikwa na machozi.
Shida iko mahali,kuna baadhi ya watu wanataka wawapangie watu maisha,yaani mtu anataka watu waishi anavyotaka yeye,hata kama maisha ya hao watu hayampunguzii wala kumuongezea chochote,hii sio kwenye masuala ya imani tu,hata kwenye maisha ya kawaida.yaani mtu hujiona yeye yuko sahihi juu ya wote,na mawazo na matamanio yake ndio anataka watu wayaishi!
Mtu anasumbuliwa hadi na vyakula vya watu,ni tatizo hilo!
Hii ni dunia ya uhuru wa kila kitu,kiimani kibiashara n.k.
Kila mtu afuate njia yake kama hakuna sheria anayovunja.
Ndio maana wahenga waliuliza,"pilipili usiyoila yakuwashia nini?"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…