Waislamu Waafrika waliosoma madrasa wanaweza kuongea lugha ya kiarabu kwa ufasaha na weledi?

Waislamu Waafrika waliosoma madrasa wanaweza kuongea lugha ya kiarabu kwa ufasaha na weledi?

Hii ni kwenye written tu ? Au mpaka kwenye oral?
Hata kwenye oral maneno yanayosomwa kwenye quran yana utofauti na wanayoongea waarabu japo baadhi ya maneno huingiliana kotekote yapo.
Mfano wa maneno ambayo kote kwenye Quran na kiarabu yapo
1.Kullu-Kila
2.Qul-Sema
3.Mai-maji
4.Twaama-Chakula
5.Fukara-fukara
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Kitu ambacho wakristo wengi hawaelewi.
Busara ya kuacha Qur-an katika lugha yake ya asili ni kuepuka maandiko kupotea, huwezi kufasiri exactly kitu kutoka kwenye lugha moja kwenda kwenye lugha nyingine lazima kuna maana itapotea. Na ndio mana hata Qur-an imebaki kwenye classical Arabic ambayo hakuna anayezungumza kwa sasaivi! Kama ilivyokuwa old English au latin. Ingekuwa rahisi basi ungeona Qur-an imeshafasiriwa kwenda kwenye Modern Standard Arabic lakini la hasha, huwezi kukuta hiko kitu. Eti Qur-an ya kiswahili, au kihaya NEVER. Mwenyezimungu aliapa kukilinda hiki kitabu kitakatifu na kitabaki kama kilivyoshushwa haijalishi itapita miaka mingapi

saivi ukijaribu kuifasiri Qur-an kutoka kwenye classical arabic (lugha iliyokomaa kimsamiati) ukaleta kwenye kiswahili bila kupoteza maana! Haiwezekani
Na hii ndiyo inayofanya bible kupoteza muundo wake kadiri miaka inavyoenda (No hard feelings) hata sisi waislamu tunaamini katika Zaburi, Injili na torati lakini sio hii iliyopinduliwa pinduliwa!

Nimewaeleza hapo juu lakini wala hawataki kuelewa. Wala nia yao hawa watu sio kujifunza. NIA YAO NI KUUKASHIFU UISLAMU
Hiawezekani ukauliza jambo kisha ukafahamishwa halafu unabishana na anayekufahamisha. Ina maana una jibu lako ndio mana unabisha. Sasa umeuliza ya nini kama kila anayekueleza unabishana naye na unataka msimamo wako ndio tuusikie.

HAWA WENZENTU WAMETUMWA KUUCHAFUA UISLAMU NA INAWEZEKANA HATA WAKAWA WAPO KAZINI WANALIPWA KWA HILO

LAKINI KAMWE HAWAWEZI CHOCHOTE WANAHANGAIKA TU
 
Ila huyu mtoa mada namsifu amejitahidi kutumia lugha nzuri kwa kias chake na pia sisi tuwajibu hivi hivi kwa kiungwana tutaelewana tu
 
Hata kwenye oral maneno yanayosomwa kwenye quran yana utofauti na wanayoongea waarabu japo baadhi ya maneno huingiliana kotekote yapo.
Mfano wa maneno ambayo kote kwenye Quran na kiarabu yapo
1.Kullu-Kila
2.Qul-Sema
3.Mai-maji
4.Twaama-Chakula
5.Fukara-fukara
Naam, issue ya kutoonesha irabu ni kwenye written tu
 
Mkuu, huko Madrasa watoto wanafundishwa kwa mfumo wa lugha kama zilivyo lugha nyingine. Kwa maana ya kwamba a b c d & a e i o u.

Wanafundishwa vyema kabisa, ndio maana mwanafunzi bora anayezingatia mafunzo ana uwezo wa kukifahamu Kiarabu kwa ufasaha.
Sio kweli hata kidogo.
 
Hivi ukiwa muislamu uliyesoma dini madrasa automatically unakuwa na uwezo wa kuzungumza Kiarabu kwa ufasaha na weledi? Unaweza kufika uarabuni mkazungumza na mwarabu mkaelewana vizuri au huwa cha kuzungumza nje ya dini ni cha kuombea maji ya kunywa tu?
Huwa naona wengi wanaweza kunukuu Quran kwa kiarabu na pia hata katika kuswali kinatumika kiarabu.

Bro wakija wenyewe mii simo. Maana kuna siku niliwahi kuuliza hapa kama uislam ni chombo au mpango wa waarabu kueneza tamaduni, mila na zao. Walikuwa mbogo. Badala ya kushambulia hoja, wakamshambulia mtoa hoja.
 
Nimewaeleza hapo juu lakini wala hawataki kuelewa. Wala nia yao hawa watu sio kujifunza. NIA YAO NI KUUKASHIFU UISLAMU
Hiawezekani ukauliza jambo kisha ukafahamishwa halafu unabishana na anayekufahamisha. Ina maana una jibu lako ndio mana unabisha. Sasa umeuliza ya nini kama kila anayekueleza unabishana naye na unataka msimamo wako ndio tuusikie.

HAWA WENZENTU WAMETUMWA KUUCHAFUA UISLAMU NA INAWEZEKANA HATA WAKAWA WAPO KAZINI WANALIPWA KWA HILO

LAKINI KAMWE HAWAWEZI CHOCHOTE WANAHANGAIKA TU
Majadiliano hukuza uelewa mkuu, deep questioning, deep answering huko ulaya na amerika wengi wanabadili dini baada ya majadiliano. Kikubwa lugha ya kiungwana tu itumike
 
Nimejaribu kufatilia huu mjadala toka mwanzo sijaona jibu la mwislamu yeyote kutoa jibu fasaha kuhusu lugha iliyoandikwa kwenye korani inaonekana wengi wenu ni wale fata mkumbo au umezaliwa ktk familia ya kiislamu lakini ukuwai kudadisi masuala ya dini yako uliyoirithi toka kwa wazazi wako.
Nilijaribu kuwauliza marafiki zangu waisalamu kwenye kijiwe cha kahawa .
Kuna ustaadh mmoja hivi anajua sana masuala ya dini anatokea msikiti maarufu kwa jina la ngamia mburahati.
Alinijibu kwamba Korani imeandikwa kwa kutumia lugha ambayo ipo ktk jamii fulani kwenye kijiji na hadi leo hii hiyo jamii hipo na wanazungumza hiyo lugha, tufanye hapa wangechukua mfano lugha ya( kizanaki) ingetumbukizwa kwenye korani ingekosa irabu a,ei,o,u
Majibu yashatolewa kote unless tu hujasoma, Mkuu mngoni ametoa Majibu mazuri tu.

Quran inatokana na Fus'ha classical Arabic ya wakati huo, kama huyo sheikh alivyokwambia ila kuifanya iwe rahisi kusomeka na hata wasio kuwa waarabu yakatumika maandishi rahisi kuyasoma yakawekwa irabu na viashiria vingine kMa hapa uvute, hapa ukaze etc.

So ni rahisi kusoma Quran hata kama sio mwarabu, binafsi naweza kusoma Quran ila Kiarabu mpaka nikaze sana na maneno mengi yatanishinda.

Hili ni shairi la kiswahili ambalo lime tumia Lugha ya kiarabu cha kwenye Quran kuandika

img_1_1733303988004~2.jpg

Unaona hivyo mistari vimepita juu na chini? Hizo ni irabu na alama nyengine kukusaidia kusoma,

Ila kiarabu chenyewe kinakua kama hivi
images (6).png

So kiarabu cha Quran hata wewe ukipigwa msasa wiki tu unaweza kuanza kusoma, ila kiarabu chenyewe inabidi ukae darasani kujifunza.
 
Nimewaeleza hapo juu lakini wala hawataki kuelewa. Wala nia yao hawa watu sio kujifunza. NIA YAO NI KUUKASHIFU UISLAMU
Hiawezekani ukauliza jambo kisha ukafahamishwa halafu unabishana na anayekufahamisha. Ina maana una jibu lako ndio mana unabisha. Sasa umeuliza ya nini kama kila anayekueleza unabishana naye na unataka msimamo wako ndio tuusikie.

HAWA WENZENTU WAMETUMWA KUUCHAFUA UISLAMU NA INAWEZEKANA HATA WAKAWA WAPO KAZINI WANALIPWA KWA HILO

LAKINI KAMWE HAWAWEZI CHOCHOTE WANAHANGAIKA TU
Mpaka hapa hakuna tena maana ya kushiriki kwenye huu mdahalo, ni wazi kuwa mtoa mada ana majibu yake anayoyahitaji. Anauliza swali anajibiwa anabisha sasa mbona uulize wakati majibu yako inayo??
 
Hapa ndio hua wananichanganya kwamba kuran imeandikwa kwakiarabu ila kiarabu ni lugha tofaut na kuran, yan unaweza kuijua koran nzima kuisoma nakuitafsiri ila ukashindwa kukijua kiarabu
 
Kwenye shule za Kiislamu kiarabu kinafundishwa kama (Arabic language) na somo la dini (Islamic knowledge)
Kwa kuna umuhimu kujua kiarabu ili uelewe zaidi Quran
 
Hivi ukiwa muislamu uliyesoma dini madrasa automatically unakuwa na uwezo wa kuzungumza Kiarabu kwa ufasaha na weledi? Unaweza kufika uarabuni mkazungumza na mwarabu mkaelewana vizuri au huwa cha kuzungumza nje ya dini ni cha kuombea maji ya kunywa tu?
Huwa naona wengi wanaweza kunukuu Quran kwa kiarabu na pia hata katika kuswali kinatumika kiarabu.

Hapana hii inategemea. Madrasa zetu nyingi hazitilii mkazo katika kujifunza lugha ya Kiarabu. Zile ambazo zinafundisha Kiarabu hazifundishi kwa undani sana.

Ila ukitaka uijue Dini ya Kiislamu vizuri lazima usome Kiarabu na ukijue. Hii inataka muda na juhudi kubwa.

Qur'an ni muujiza ndio maana mtu yoyote ambaye hakijui Kiarabu anaweza kuihifadhi Qur'an na akaisoma kwa ufasaha, hata akiwa hajui maana yake. Kwa vitabu vingine hili ni muhali.
 
Kwanza Kiarabu ni lugha kama zilivyo Kiswahili, Kiingereza n.k
Kiarabu sio Kiislam bali ni lugha iliyotumika kushushiwa Quran.

Hivyo basi, wapo wanaokielewa Kiarabu vyema kabisa na binafsi nina ndugu wenye uwezo wa kuzungumza Kiarabu kwa ufasaha na ni kweli walijifunza hukohuko Madrasa na wengine walipata nafasi ya kuongeza maarifa huko Arabuni.

Hao ni asilimia ngapi ya jamii ya watanzania?
Pia unadhani mazingira ya lugha (linguistic environment) ya kiarabu hapa Tanzania 🇹🇿 yanamsaidia mtu wa kawaida kuielewa lugha hiyo inavyopaswa?
Au ni kukalili yale maneno ya kwenye swala tano ndiyo kuna mfanya mtu aonekane anajua kiarabu?
Ninachojua kiarabu kina maneno mengi sana zaidi ya yale mnayoyatumia kwenye swala 5 na adhana.
 
Yani wewe mmatumbi huoni aibu kusema kiarabu ni lugha yako? Huu ni utumwa wa kiakili wa viwango vya juu sana.

Kiarabu ni lugha yetu sisi Waislamu na tunajivunia sana.

Sababu kama unataka kuijua dini ya Kiislamu vizuri ni lazima ujifunze lugha ya Kiarabu.

Lakini, kingine hakuna lugha ambayo imehudumiwa na kuhifadhiwa vizuri sana kuzidi lugha ya Kiarabu. Hapa tuweke mapenzi pembeni.
 
Quran imeandikwa kiarabu ila kiarabu si Quran maandishi ya kiarabu yanatofautiana na ya kwenye Quran kwa kuwa huwa hayana irabu(aeiou) kwa hyo anaesoma Quran tupu hawez kusoma kiarabu unless amesoma kiarabu ama kwa lugha nyingine kiarabu kinasomwa kwa kujua maana na muundo wa maneno.

Hapo tujiulize swali. Je kiarabu cha awali/zamani pia kiliandikwa bila irabu (vowels; a, e, i, o & u)?

Maoni yangu ni kuwa lugha iliyoandikwa kwenye kuruwan kuna kipindi itakufa. Hakutakuwa na lugha inayofanana nayo. Hiyo ni kwa sababu kila lugha maneno yake mengi tu huzaliwa, hukua na kufa. Sasa kama lugha ya kuruwan haiendani na sheria hii ya lugha, basi itapitwa na wakati. Katika maana ya kuwa itaendelea kitumia maneno ya zamani ambayo hayapo tena katika lahaja za kisasa za lugha ya kiarabu.
 
Wakiristo waliosoma Magomeni Mwakinya St Joseph secondary school wakienda ulaya wanaongea kidhungu? Au ndio hello hello

Ukitumia msingi huo huo. Je mswahili aliyesomeshwa kiarabu madrasa pekee, ataweza kuongea kiarabu na muarabu wa Oman? Achilia mbali muarabu wa Zanzibar.
CC: Yoda
 
Si ilishushwa kwa mtume na watu wanaoongea lugha hiyo. Sasa ulitegemea iwe ya kiswahili. Vitabu vyote vya dini viliandikwa kwa lugha zao . Kilichotakiwa ni viongozi kufanya juhudi za kufundisha Quran kwa lugha zinazotumiwa na watu mbalimbali
Lugha Hutambulisha jamii.
Kama Quran ilishushwa ikiwa na ujumbe wa kiarabu Maana yake walengwa walikuwa ni waarabu.
 
Back
Top Bottom