Waislamu Waafrika waliosoma madrasa wanaweza kuongea lugha ya kiarabu kwa ufasaha na weledi?

Waislamu Waafrika waliosoma madrasa wanaweza kuongea lugha ya kiarabu kwa ufasaha na weledi?

Ukiwa madrasa kuna somo maalum la lugha ya kiarabu, ukikaa vizuri hapo unatoka unaizungumza vizuri tu na ukiwa mzembe utaishia kujua quran tu lakini lugha itakupiga chenga.
Ni kweli Kuna watu nimeishi nao wanaongea vizuri kabisa bila shida.
 
Mbona mnarudia rudia maswali tumeshawajibu mtu anaweza akajua Quran na tafsiri yake ila asielewe kiarabu sio dhambi na haimuondolei chochote kwenye dini ila wale wanaobobea kwenye kiarabu wana X factor kwenye kutafsiri maneno mengi kwenye Quran, Quran imeshushwa kwa kiarabu ila kiarabu si Quran ni lugha pana zaidi.
Ilishushwa na nani hiyo qura'an!
 
Ni kweli Kuna watu nimeishi nao wanaongea vizuri kabisa bila shida.

Hao ni asilimia ngapi ya umma wa waislam wa Tanzania 🇹🇿 au nje ya ulimwengu wa kiarabu? Wataalam wa lugha wanasema lugha yoyote ikiwa inatumika kwa ajili ya kujifunzia, na nje ya mazingira ya kujifunzia haitumiki kuzungumzwa. Basi watumiaji wake watakuwa katika hali ya kutokuwa fasaha katika lugha hiyo. Hivyo kuna uwezekano mkubwa sana ya kuwa na asilimia kubwa sana ya waislam nje ya ulimwengu wa kiarabu kutoweza kuelewa na kuongea kiarabu kwa ufasaha. Ndiyo maana Yoda akawa anasema waislam wakikutana watasalimiana kwa kiarabu, lkn baada ya salaam wataendelea mazungumzo kwa lugha ya kiswahili.
 
Thibitisha hili. Wakina nani hao ? Unafikiri ni kama Ukristo ambao mnaliona taifa ovu la Israeli ni taifa teule na watu wake ?

Hili limesemwa wapi katika Uislamu ? Tuwekee andiko.

Kwako wewe ambaye huujui Uislamu na Uarabu kadhalika ni ngumu kwako, ila ni rahisi sana.

Kwanini mnayajadili mambo ambayo hamna elimu nayo ? Unaweza pia ukaongea hayo unayosema maneno ya Kiarabu swala yako pia ikawa batili. Sala ya Muislamu ina nguzo zake na masharti kadhalika.
Ile oktoba 7 ulikuwa utukufu ule?watumwa bhana!
 
Kiarabu ni lugha na uislam ni dini, kujua lugha ya kiarabu kunaweza kukurahisishia kujua uislam,,,unaweza ukaujua uislam kwa ufasaha lakini usijue kuongea kiarabu.. Na mwisho kabisa sio waarabu wote duniani ni waislam.....wapo waarabu ambao ni wakristo.
 
Pia kuna Biblia ya kiarabu. Huwezi kuisoma na kuielewa kama hujui lugha ya kiarabu.

Hakuna somo maalum la kuisoma biblia hiyo. Usipojua kiarabu tafuta version ya lugha unayoelewa - Neno liendelee.
 
Hivi ukiwa muislamu uliyesoma dini madrasa automatically unakuwa na uwezo wa kuzungumza Kiarabu kwa ufasaha na weledi? Unaweza kufika uarabuni mkazungumza na mwarabu mkaelewana vizuri au huwa cha kuzungumza nje ya dini ni cha kuombea maji ya kunywa tu?
Huwa naona wengi wanaweza kunukuu Quran kwa kiarabu na pia hata katika kuswali kinatumika kiarabu.
Hapana Quran sio kiarabu
 
Kiarabu ni lugha na uislam ni dini, kujua lugha ya kiarabu kunaweza kukurahisishia kujua uislam,,,unaweza ukaujua uislam kwa ufasaha lakini usijue kuongea kiarabu.. Na mwisho kabisa sio waarabu wote duniani ni waislam.....wapo waarabu ambao ni wakristo.

Yote hayo tunaelewa. Issue ambayo yunahitaji ufafanuzi ni kwamba kwa nini ibada zenu ziwe kwa lugha ya kiarabu pekee. Kwa nini adhana iitwe kwa kiarabu na si kwa lugha yetu ya taifa kiswahili?
Tukisema wa uislam ni chombo au mpango wa waarabu wa kueneza tamaduni, mila na desturi zao tutakuwa tunakosea?
 
Ibada ya sala katika uislam inatumia lugha ya kiarabu ili kufanya ifanane popote duniani,,utakavyosali Tanzania ndio hivyo hivyo utakavyosali nchi yoyote duniani,,,nje ya sala lugha yoyote inaruhusiwa.
 
Na wale mawakili kile kilatini chao wanaweza kuongea kwa mawasiliaño au ni swaga tu?
 
Ibada ya sala katika uislam inatumia lugha ya kiarabu ili kufanya ifanane popote duniani,,utakavyosali Tanzania ndio hivyo hivyo utakavyosali nchi yoyote duniani,,,nje ya sala lugha yoyote inaruhusiwa.

Kknachotakiwa kufanana ni maudhui au lugha. Unataka kusema maudhui ya kiarabu yaliomo kwenye kuruwan na yanayotumiwa na waislam hayawezi kutafsiriwa katika lugha yoyote ile. Au kwa lugha rahisi, maudhui yaliyo kwenye Newton's third law of motion ya kiingereza yanaweza kuwa tofauti na yale yanayoandikwa kwa kirusi, kijerumani au kichina?
 
Kknachotakiwa kufanana ni maudhui au lugha. Unataka kusema maudhui ya kiarabu yaliomo kwenye kuruwan na yanayotumiwa na waislam hayawezi kutafsiriwa katika lugha yoyote ile. Au kwa lugha rahisi, maudhui yaliyo kwenye Newton's third law ya kiingereza yanaweza kuwa tofauti na yale yanayoandikwa kwa kirusi, kijerumani au kichina?
Brother jiridhishe tu kuwa huo ndo utaratibu uliowekwa na uislam na wenyewe wako comfortable nao hilo ndo la msingi kama ambavyo baadhi ya manabii wananena kwa lugha ambazo hazieleweki lakini kwa kuwa walengwa wameridhika nao sisi hatujishughulishi na wala haituhusu.
 
Kwanza Kiarabu ni lugha kama zilivyo Kiswahili, Kiingereza n.k
Kiarabu sio Kiislam bali ni lugha iliyotumika kushushiwa Quran.

Hivyo basi, wapo wanaokielewa Kiarabu vyema kabisa na binafsi nina ndugu wenye uwezo wa kuzungumza Kiarabu kwa ufasaha na ni kweli walijifunza hukohuko Madrasa na wengine walipata nafasi ya kuongeza maarifa huko Arabuni.
Huyu muongo muongo
 
Kknachotakiwa kufanana ni maudhui au lugha. Unataka kusema maudhui ya kiarabu yaliomo kwenye kuruwan na yanayotumiwa na waislam hayawezi kutafsiriwa katika lugha yoyote ile. Au kwa lugha rahisi, maudhui yaliyo kwenye Newton's third law of motion ya kiingereza yanaweza kuwa tofauti na yale yanayoandikwa kwa kirusi, kijerumani au kichina?
Kutafsiri Quran kwenye lugha nyingine haina shida,,,sala ya kiislam sio kusoma Quran peke yake kuna dua zingine ambazo zinatakiwa zitamkwe kiarabu katika sala na uzijue maana yake katika lugha yako.....Hilo lisikusumbue sana kwa sababu ndio uislam ulivyoelekeza na we we amini katika dini yako ilivyoelekeza.
 
Back
Top Bottom