Baljurashi
JF-Expert Member
- Dec 30, 2017
- 1,628
- 2,720
Atakayehukumu Siku ya Malipo ni ALLAH tu. Kwa mujibu wa Uislam. Usitake kumdanganya mwenzio. Ukatumia na vineno sijui maamuma hawamjui Masih ni nani kama kwamba khabari zake ni zenye kufichikana kwa Waislam.Waislamu wanamtambuwa Masiah na wanatambua ndiye atakayehukumu wazima na wafu.
Achana na hawa waislamu maamuma wanaoshinda kwenye vibaraza vya misikiti kutwa mzima hawajui hata Masiah ni nani.
Allah ni Mmoja tu, Peke yake asiye na mshirika yoyote. Amepwekeka Allah na ametakasika na yote wanayomshirikisha nayo washirikina.
Masih ni Mtume wa Allah, na ni miongoni Mitume wakubwa kabisa watano. Alitumwa kwa Wana wa Israel.
Sisi hatutambui kuwa Mtume wa Allah Isa bin Maryam ('Alayhis Salaam) atakuja kuhukumu wazima na wafu. Itikadi hii si ya Waislam, bali unawasingizia
Waislam. Allah ndie atahukumu baina ya waja wake na atawauliza waja wake (hali ya kuwa Yeye Allah ni Mjuzi wa Kila Kitu) ikiwemo Masih (Amani iwe Juu Yake);
(Qur-an 5:116-120)
116. Na pale Mwenyezi Mungu atakapo sema: Ewe Isa bin Maryamu! Ati wewe uliwaambia watu: Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa ni miungu badala ya Mwenyezi Mungu? (Na Isa) atasema: Subhanaka, Wewe umetakasika! Hainifalii mimi kusema ambayo si haki yangu. Ikiwa nilisema basi bila ya shaka umekwisha yajua. Wewe unayajua yaliyo ndani ya nafsi yangu, lakini mimi siyajui yaliyo katika nafsi yako. Hakika Wewe ndiye Mjuzi mkubwa wa yaliyo fichikana. 116
117. Sikuwaambia lolote ila uliyo niamrisha, nayo ni: Muabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi. Na mimi nilikuwa shahidi juu yao nilipo kuwa nao. Na ulipo nifisha ukawa Wewe ndiye Muangalizi juu yao. Na Wewe ni shahidi juu ya kila kitu. 117
118. Ukiwaadhibu basi hao ni waja wako. Na ukiwasamehe basi Wewe ndiye Mwenye nguvu na Mwenye hikima. 118
119. Mwenyezi Mungu atasema: Hii ndiyo Siku ambayo wasemao kweli utawafaa ukweli wao. Wao watapata Bustani zipitazo mito kati yake. Humo watadumu milele. Mwenyezi Mungu amewawia radhi, nao wawe radhi naye. Huku ndiko kufuzu kukubwa. 119
120. Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi na vilivyomo. Naye ni Muweza wa kila kitu. 120