Waislamu wako vizuri kwenye suala la ndoa

Waislamu wanamtambuwa Masiah na wanatambua ndiye atakayehukumu wazima na wafu.

Achana na hawa waislamu maamuma wanaoshinda kwenye vibaraza vya misikiti kutwa mzima hawajui hata Masiah ni nani.
Atakayehukumu Siku ya Malipo ni ALLAH tu. Kwa mujibu wa Uislam. Usitake kumdanganya mwenzio. Ukatumia na vineno sijui maamuma hawamjui Masih ni nani kama kwamba khabari zake ni zenye kufichikana kwa Waislam.

Allah ni Mmoja tu, Peke yake asiye na mshirika yoyote. Amepwekeka Allah na ametakasika na yote wanayomshirikisha nayo washirikina.

Masih ni Mtume wa Allah, na ni miongoni Mitume wakubwa kabisa watano. Alitumwa kwa Wana wa Israel.

Sisi hatutambui kuwa Mtume wa Allah Isa bin Maryam ('Alayhis Salaam) atakuja kuhukumu wazima na wafu. Itikadi hii si ya Waislam, bali unawasingizia
Waislam. Allah ndie atahukumu baina ya waja wake na atawauliza waja wake (hali ya kuwa Yeye Allah ni Mjuzi wa Kila Kitu) ikiwemo Masih (Amani iwe Juu Yake);




(Qur-an 5:116-120)

116. Na pale Mwenyezi Mungu atakapo sema: Ewe Isa bin Maryamu! Ati wewe uliwaambia watu: Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa ni miungu badala ya Mwenyezi Mungu? (Na Isa) atasema: Subhanaka, Wewe umetakasika! Hainifalii mimi kusema ambayo si haki yangu. Ikiwa nilisema basi bila ya shaka umekwisha yajua. Wewe unayajua yaliyo ndani ya nafsi yangu, lakini mimi siyajui yaliyo katika nafsi yako. Hakika Wewe ndiye Mjuzi mkubwa wa yaliyo fichikana. 116


117. Sikuwaambia lolote ila uliyo niamrisha, nayo ni: Muabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi. Na mimi nilikuwa shahidi juu yao nilipo kuwa nao. Na ulipo nifisha ukawa Wewe ndiye Muangalizi juu yao. Na Wewe ni shahidi juu ya kila kitu. 117


118. Ukiwaadhibu basi hao ni waja wako. Na ukiwasamehe basi Wewe ndiye Mwenye nguvu na Mwenye hikima. 118


119. Mwenyezi Mungu atasema: Hii ndiyo Siku ambayo wasemao kweli utawafaa ukweli wao. Wao watapata Bustani zipitazo mito kati yake. Humo watadumu milele. Mwenyezi Mungu amewawia radhi, nao wawe radhi naye. Huku ndiko kufuzu kukubwa. 119

120. Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi na vilivyomo. Naye ni Muweza wa kila kitu. 120
 
Waislamu wanamtambuwa Masiah na wanatambua ndiye atakayehukumu wazima na wafu.

Achana na hawa waislamu maamuma wanaoshinda kwenye vibaraza vya misikiti kutwa mzima hawajui hata Masiah ni nani.
Acha kuisemea dini yetu wakati yko wala hauijui vzr
 
Yani unasoma unainjoy kabisa maneno yamenyooka kabisa. Raha tupu. Quran is the best of all books.
 
Huezi kua muslim kama humuamin Christ, karibu katika uislam na utaendelea kumuamini Christ zaid ya huko ulipo
 
Mwenyez mung katuletea uislamu na qur-ani kitabuchake ndo muongozo katik dunia.
 
Msisingizie dini bwana. Hayo ni mapenzi yenu wenyewe. Unaweza kuoa simple tuu ukiwa mkristo bila shida yoyote. Tatizo wengi wetu tunafanya harusi ndio muhimu baadala ya ndoa kiwa muhimu.
Binti atakubali?
ME hawatakagi mambo mengi, tatizo lipo kwa KE
 
Laana tuliyopewa wanadam ni Kwamba Mwanaume utatafuta Kwa jasho Mwanamke atazaa Kwa uchungu. Sasa tumegeuza utaratibu ndo shida tunayoipata. Wenzetu wapemba wanafuata Ili kwenye maisha ndoa zinadumu watoto wanazaliwa wakutosha. Mataifa yote Matajiri ni population. Sasa tunashindwa kuzaliana sababu Mwanamke naye yupo kwenye Shughuli za kiuchumi. Wapemba mbeleni watakuwa powerful society.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…