PreGE2025 Waislamu walikuwa mbele kumng'oa Mkoloni, Wakristu kwa kiasi kikubwa ndio watakaoing'oa CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Ni dhahiri bila chembe ya shaka, Waislamu walikuwa msitari wa mbele kumng'oa mkoloni. Hilo halina ubishi, maana Tangu enzi za vita vya mababu zetu dhidi ya wakoloni, struggle nyingi zilifanyika kwenye ukanda wenye waislamu wengi, kuanzia kwa Mkwawa, Abushiri huko Pangani, Kinjekitile Ngwale huko Kilwa wote hao walikuwa Waislamu (Anayetaka elimu ataelimishwa).

Harakati za Uhuru nazo kwa kiwango kikubwa zilikomaa zaidi katika mikoa ya waislamu wengi, kuanzia kwa vyama vya AA, kuja TAA hadi TANU, Majority ya waliounga mkono struggle hizo walikuwa ni Waislamu.

Baada ya Uhuru Nyerere aligundua kuwa nguvu mojawapo inayoweza kumsumbua kutawala ni Waislamu, kwa hiyo akawatengenezea chombo chini ya Usalama wa Taifa kiitwacho BAKWATA, chombo hiki kazi yake ni kuhubiri amani, na kukataza movement yoyote ya waislamu kuraise up.

Kitu kimoja ambacho Nyerere alisahau au aliacha kwa makusudi ni kuliacha Kanisa kuoperate nchini kwa Autonomy, bila kuingiliwa organisations zake na mipango yake. Kitabu cha Sivalon cha Kanisa Katoliki na siasa za Tanzania kilitoa mwanga namna ambavyo kanisa lilikuwa likishirikiana na serikali. Nyerere mwenyewe amewahi kutamka kuwa "I have given the church, a good chance to operate in Tanzania". Matokeo ya sera za Nyerere za kuwacontrol waislamu kupitia BAKWATA na Kuliacha Kanisa Kuthrive, leo hii limetengeneza Power Kubwa sana ya kimtandao na waumini wengi kiasi kwamba Likiamua jambo dhidi ya serikali kwa dhati ya kuliamua basi serikali ya bongo haina namna zaidi ya kukaa chini kuzungumza nalo ama kwa siri au kwa dhahiri (Huwa kuna mikutano mingi tu serikali huwa inafanya na maaskofu kimyakimya).

Sasa Kanisa linataka haki nchini, limechoshwa na propaganda za Amani. Linataka amani ya kweli itamalaki kupitia Haki. Polepole limeanza kupaza sauti. Kwa bahati mbaya Kanisa si BAKWATA, Kanisa si tawi la Serikali, Halitabiriki, linaweza kuiunga mkono serikali waziwazi au likaamua kuigomea, na serikali haina uwezo kulifanya lolote!.

Na bahati nzuri kanisa limejijengea heshima kwa:
1. Kumchenjia Magufuli alivyokuwa anakandamiza demokrasia, kumbuka ule waraka wa demokrasia uliomchanganya Magufuli, hivyo hii inaondoa dhana kuwa Kanisa linabaugua mtawala wa kumkosoa kwa misingi ya dini yake.

2. Waraka wa Covid, uliotaka serikali iache kufanya mambo kama waganga wa kienyeki huku wananchi wakiwa hatarini

3. Hata maaskofu kama Niwemugizi, Bagonza, Saba na wengineo walisimama kiume na kutoa kauli kuwa mambo hayako sawa

Alivyokuja huyu mama na kuanza kuingia mikataba ya kimangungo kwa kuuza bandari yetu kanisa lilisimama na kukataa. Hata hivyo halikuamua kuwapeleka mamilioni barabarani kwenda Ikulu ili "kuleta misa" ya kuombea busara kwenye matumizibya rasilimali zetu. Uwezo huo linao lakini halijaamua tu.

Sasa, kwa sasa Baada ya Serikali kufanikiwa kuwazima Waislamu kupitia sheria za Ugaidi, Kuwatia ndani na kuwashughulikia Masheikh influential, Kuvamia misikiti na kusimika maimamu wanaowataka kupitia operation maalum za usalama wa Taifa, Na kuwaweka kwenye payrol baadhi ya masheikh, Serikali imefanikiwa kudhibiti mwamko na nguvu za Waislamu. Waislamu wa leo siyo sawa na Waislamu wa Mwembechai mwaka 1998, Wale walikuwa breed nyingine kabisa. Wa sasa wamethibitiwa!.

Ila Kanisa lipo Strong, Kama kuna Taasisi itakayoharakisha CCM kudondoka ni taasisi ya Kanisa (TEC). Ugumu wa kudeal na Kanisa ni kuwa kuna waumini wao wengi ktk mifumo ya nchi na serikali, ni vigumu nyakati zote kuwa loyal kwa mifumo kandamizi ya kiutawala huku wakiendelea kuwa members wa taasisi za dini zinazowanyooshea vidole, lazima crack ktk dhamiri zao itakuwepo. Uwezo wa kiorganizesheni wa Kanisa kufikia mtu wa chini, Loyalty ya waumini kwa viongozi wa dini, Lakini kikubwa zaidi ni Waumini, hawa ni nguvu ambayo Kanisa ikisema iitumie kukataa mambo ya kiuonevu ya CCM, basi CCM haina chance.

Ukombozi wa Kwanza wa nchi hii kwa kiasi kikubwa uliungwa mkono na umma wa waislamu kwanza na zaidi, Ila ninaona ukombozi wa pili wa nchi hii utaletwa na Kanisa!
SIYO KWELI KUWA WAISLAMU WALIKUWA MBELE KUWANGOA WAKOLONI LABDA UWAJUI WAISLAMU VIZURI ?NIULIZENI MIMI KAMA MNABISHA WAISLAMU NI MAANDAZI TU
 
Historia za kutunga na za kibwege hizo .

Waislam walikuwepo tangu karne ya Saba Afrika mashariki lakini hapakuwa na kitu kinaitwa siasa wala Elimu ya siasa wala mtu mweusi kutawala nchi zaidi ya machifu wa kimila waliokua wanatawala makabila na koo tuu tena kwa kurithi .

Hakuna Mahali kabla ya ukristo kufika ambao palikua na vyama vya siasa vilivyosajiliwa au kuruhusiwa kugombea nafasi ya Sultani popote .

Baada ya Ukristo kuja ndio walifundisha watu na kuwapatia watu ya kujitawala wenyewe .Wakafundisha madaktari ili wajitibu na kuwatibu ndugu zao , Wanawafundisha walimu wa kufundisha wanafunzi n.k. Wakristo chini ya mifumo ya Kirumi waka waandaa watu kuwa wanajeshi ,Mapolisi na PGO ,Mahakama na majaji , Bendera na majengo ya watawala . Wakawafundisha namna ya kuunda vyama na mifumo ya kisiasa ya kufanya chaguzi . Hapo Waislam wakapata fursa ya kuunda vyama vya kidini kama Tanzania Muslims Association kupigania maslahi ya waislam tu badala ya maslahi ya Jamii nzima .
Wakristo chini ya Kanisa Katoliki walishauriwa kuwa wasiunde vyama vya kidini kwa sababu wataganyika .
Nyerere akiwa ameandaliwa vyema kuwakomboa watanzania wote bila kujali dini alipiga kampeni za kuunganisha vyama vyote na watanzania wote kudai uhuru.
Waislam wakiwa bado wanawaza kunufaisha dini yao walidhani kuwa baada ya uhuru wataendelea na harakati za kudai haki zao kama waislam badala ya Watanzania na binadam ambao ni sawa na wenye mahitaji sawa.

Nyerere akaunda Bakwata na KKKT kwaAjili ya kuunganisha nguvu pamoja na kujenga taifa.

Waislam kwa muda mrefu wakawa bado wanawaza ubinafsi wa kidini badala ya haki sawa kama binadamu.
Mwinyi alipokuja akaja na hulka na tabia za waZanzibar kuimarisha utawala wake kupitia uungwaji mkono na baadhi ya waislam, wenye misimamo mikali ndio zinaanzishwa harakati za kupigania maslahi ya kiislam na kuwa na vurugu za mara kwa mara huku wanafunzi wa kiislam wakiwa wamejitenga mashuleni na kuvaa un8fom tofauti.
Good lesson.
 
Naona imeshageuka sasa ushindani wa kidini. Here are facts.
0. Nadhani mtu akiandika neno "etc" unaelewa maana yake
1. Miaka ya 1950's kwenda 1960's wakati huo kanisa likiwa na less than 100 years nchini mikoa mingi ya Tanganyika ya interior, Pagans walikuwa wengi kuliko wakiristo
2. Sensa ya 1954 Waislamu walikuwa majority Tanganyika wakifuatiwa na Pagans, Wakiristo walikuwa namba 3
3. Sijasema kulikuwa na zero christians katika movement za uhuru lakini walikuwa wachache kulinganisha na waislamu
4. Church ya Tanganyika haikuwa interested kukemea maovu ya Wakoloni. Nipe waraka mmoja wa Kanisa ktk miaka hiyo ukikemea colonial policies Tanganyika.
5. Jiulize Adam Sapi Mkwawa uislamu wake ni wa kusilimu au kazaliwa ndani ya familia ya kiislamu?

Najua, hii mada ni ngumu kidogo,ila ni fact kuwa Waislamu walikuwa front zaidi kukubali agenda ya uhuru kuiunga mkono na kushriki ipasavyo, hii haimaanishi hakuna wakirsto waliounga mkono agenda hiyo
Wimbo tu wa Taifa unajieleza kuwa ni nani waliopigania uhuru.Wimbo wa Taifa ndiyo jibu.
 
Ni dhahiri bila chembe ya shaka, Waislamu walikuwa msitari wa mbele kumng'oa mkoloni. Hilo halina ubishi, maana Tangu enzi za vita vya mababu zetu dhidi ya wakoloni, struggle nyingi zilifanyika kwenye ukanda wenye waislamu wengi, kuanzia kwa Mkwawa, Abushiri huko Pangani, Kinjekitile Ngwale huko Kilwa wote hao walikuwa Waislamu (Anayetaka elimu ataelimishwa).

Harakati za Uhuru nazo kwa kiwango kikubwa zilikomaa zaidi katika mikoa ya waislamu wengi, kuanzia kwa vyama vya AA, kuja TAA hadi TANU, Majority ya waliounga mkono struggle hizo walikuwa ni Waislamu.

Baada ya Uhuru Nyerere aligundua kuwa nguvu mojawapo inayoweza kumsumbua kutawala ni Waislamu, kwa hiyo akawatengenezea chombo chini ya Usalama wa Taifa kiitwacho BAKWATA, chombo hiki kazi yake ni kuhubiri amani, na kukataza movement yoyote ya waislamu kuraise up.

Kitu kimoja ambacho Nyerere alisahau au aliacha kwa makusudi ni kuliacha Kanisa kuoperate nchini kwa Autonomy, bila kuingiliwa organisations zake na mipango yake. Kitabu cha Sivalon cha Kanisa Katoliki na siasa za Tanzania kilitoa mwanga namna ambavyo kanisa lilikuwa likishirikiana na serikali. Nyerere mwenyewe amewahi kutamka kuwa "I have given the church, a good chance to operate in Tanzania". Matokeo ya sera za Nyerere za kuwacontrol waislamu kupitia BAKWATA na Kuliacha Kanisa Kuthrive, leo hii limetengeneza Power Kubwa sana ya kimtandao na waumini wengi kiasi kwamba Likiamua jambo dhidi ya serikali kwa dhati ya kuliamua basi serikali ya bongo haina namna zaidi ya kukaa chini kuzungumza nalo ama kwa siri au kwa dhahiri (Huwa kuna mikutano mingi tu serikali huwa inafanya na maaskofu kimyakimya).

Sasa Kanisa linataka haki nchini, limechoshwa na propaganda za Amani. Linataka amani ya kweli itamalaki kupitia Haki. Polepole limeanza kupaza sauti. Kwa bahati mbaya Kanisa si BAKWATA, Kanisa si tawi la Serikali, Halitabiriki, linaweza kuiunga mkono serikali waziwazi au likaamua kuigomea, na serikali haina uwezo kulifanya lolote!.

Na bahati nzuri kanisa limejijengea heshima kwa:
1. Kumchenjia Magufuli alivyokuwa anakandamiza demokrasia, kumbuka ule waraka wa demokrasia uliomchanganya Magufuli, hivyo hii inaondoa dhana kuwa Kanisa linabaugua mtawala wa kumkosoa kwa misingi ya dini yake.

2. Waraka wa Covid, uliotaka serikali iache kufanya mambo kama waganga wa kienyeki huku wananchi wakiwa hatarini

3. Hata maaskofu kama Niwemugizi, Bagonza, Saba na wengineo walisimama kiume na kutoa kauli kuwa mambo hayako sawa

Alivyokuja huyu mama na kuanza kuingia mikataba ya kimangungo kwa kuuza bandari yetu kanisa lilisimama na kukataa. Hata hivyo halikuamua kuwapeleka mamilioni barabarani kwenda Ikulu ili "kuleta misa" ya kuombea busara kwenye matumizibya rasilimali zetu. Uwezo huo linao lakini halijaamua tu.

Sasa, kwa sasa Baada ya Serikali kufanikiwa kuwazima Waislamu kupitia sheria za Ugaidi, Kuwatia ndani na kuwashughulikia Masheikh influential, Kuvamia misikiti na kusimika maimamu wanaowataka kupitia operation maalum za usalama wa Taifa, Na kuwaweka kwenye payrol baadhi ya masheikh, Serikali imefanikiwa kudhibiti mwamko na nguvu za Waislamu. Waislamu wa leo siyo sawa na Waislamu wa Mwembechai mwaka 1998, Wale walikuwa breed nyingine kabisa. Wa sasa wamethibitiwa!.

Ila Kanisa lipo Strong, Kama kuna Taasisi itakayoharakisha CCM kudondoka ni taasisi ya Kanisa (TEC). Ugumu wa kudeal na Kanisa ni kuwa kuna waumini wao wengi ktk mifumo ya nchi na serikali, ni vigumu nyakati zote kuwa loyal kwa mifumo kandamizi ya kiutawala huku wakiendelea kuwa members wa taasisi za dini zinazowanyooshea vidole, lazima crack ktk dhamiri zao itakuwepo. Uwezo wa kiorganizesheni wa Kanisa kufikia mtu wa chini, Loyalty ya waumini kwa viongozi wa dini, Lakini kikubwa zaidi ni Waumini, hawa ni nguvu ambayo Kanisa ikisema iitumie kukataa mambo ya kiuonevu ya CCM, basi CCM haina chance.

Ukombozi wa Kwanza wa nchi hii kwa kiasi kikubwa uliungwa mkono na umma wa waislamu kwanza na zaidi, Ila ninaona ukombozi wa pili wa nchi hii utaletwa na Kanisa!
Sema Nyerere alilipendelea kanisa Katoliki lililomlea. Alilishughulikia vilivyo kanisa Anglicana kwa kumhofia mwingereza kurejea kupitia kanisa hilo.
 
Nyerere aliwabana zaidi Walokole, hakuwapa nafasi ya kustawi nchini. Walikuja kuinuka kipindi cha Mwinyi alipowatengenezea mazingira mazuri ya kuanzisha makanisa yao ya born again.
 
CHADEMA ipi imeshindwa, ile ya Mbowe iliyogeuzwa kuwa tawi la CCM?
Sasa elewa kwamba hii siyo kazi ya CHADEMA tena pekee; hii ni kazi itakayofanywa na waTanzania wenyewe. Kuingiza mambo ya kidini humo ni kutafuta njia za kuwagawanya tu waTanzania wasitimize adhma ya kuikomboa nchi yao toka kwa wakoloni hawa wapya.

Kunyimwa HAKI ya wananchi kuwachagua viongozi wanao wataka wao haliwahusu wakristo au waislaam; ni swala la waTanzania wote.
Well Said!
 
Mmomonyoko wa maadili unalibomoa Taifa kwa kasi kubwa,

Huko ndiko viongozi wa dini wanapaswa kujikita, wakifanikiwa huko mbona huku kwingine itakuwa rahisi tu.

Mambo ya siasa waachiwe wanasiasa wenyewe wayatatue kwa njia za kisiasa, ambazo zipo na zinafahamika.
Haya maneno ya "mmomonyoko wa maadili", yamekuwepo toka enzi na enzi; hili siyo jambo jipya. Kila jamii kihistoria imekuwa ikizungumzia "mmomomyoko wa maadili wayajuwavyo wao katika enzi zao.

Sasa jiulize , ni "maadili" gani yanayo himiza kunyima watu HAKI zao kuwachagua viongozi wao?
Tunaimbiwa nyimbo za AMANI, kama vitisho vya kuwatia hofu watu wasidai HAKI; halafu tunaambiwa watu wanakosa "maadili", hayo ni maadili ya namna gani.

Tusimung'unye maneno hapa na kutoa visingizio visivyo kuwa na ukweli; kilichopo sasa ndani ya nchi hii ni UDINI. CCM inatetewa na BAKWATA; ambao nao wanataka dini isiingie kwenye siasa!

CCM inapofanya kila hila kunyima HAKI na viongozi wa dini wakitoa maoni juu ya hilo inakuwa ni kuingiza DINI kwenye siasa?
Kwa nini sote tusiwe waTanzania kwanza, na kudai HAKI itendeke bila kujali ni kiongozi wa dini gani anayefanya hila za kunyima waTanzania HAKI zao za kuwachagua viongozi wanao wataka wenyewe. Kwa nini uovu huo tuutetee kwa sababu tu unafanywa na mtawala wa dini yetu?

Mkuu 'Stroke', sasa tuache udanganyifu na visingizio vingine vyote, tatizo letu ndani ya nchi hii ni UDINI, na ni lazima watu walitambue hilo waziwazi. Tuache kufunika jambo lililo wazi.
 
Nyerere aliwabana zaidi Walokole, hakuwapa nafasi ya kustawi nchini. Walikuja kuinuka kipindi cha Mwinyi alipowatengenezea mazingira mazuri ya kuanzisha makanisa yao ya born again.
'Elements' zile zile za mwanzo ulizo anza nazo huko nyuma naona zimerudi kwa kasi sana wakati huu. Wakati wa Nyerere ulokole pote duniani ulikuwa haujapamba moto kama ulivyokuja kujitokeza baadae; sasa wewe hapa unasema ulibanwa na Nyerere, aliubana vipi?
 
Amekuchukiza kabisa kwa kusema Waislam ndo waliopigania uhuru wa nchi hii!
Ni wapi niliposema "amenichukiza"?
Hao waliopigania uhuru hawakuwa waTanganyika? Uislamu wao au ukristo wao una maana gani katika mapambano ya kupata uhuru?
watu wa aina yenu mnaokazania udini kazi yenu ni kuleta mifarakanyo tu katika taifa hili.
 
Mkuu hii ni hakika na kweli.
Sasa kazi ipo kwa wala nguruwe,kuleta uhuru wa pili
 
'Elements' zile zile za mwanzo ulizo anza nazo huko nyuma naona zimerudi kwa kasi sana wakati huu. Wakati wa Nyerere ulokole pote duniani ulikuwa haujapamba moto kama ulivyokuja kujitokeza baadae; sasa wewe hapa unasema ulibanwa na Nyerere, aliubana vipi?

Ukijua chanzo cha Mgogoro wa pioneers wa makanisa ya kilokole ya akina Moses Kulola na wenzie kilichoanza miaka ya 1980's mpaka kugawanyika utafunguka macho sana.
It seems wabongo wengi wako gizani na operesheni za serikaki ktk makundi haya ya dini.
 
Ni wapi niliposema "amenichukiza"?
Hao waliopigania uhuru hawakuwa waTanganyika? Uislamu wao au ukristo wao una maana gani katika mapambano ya kupata uhuru?
watu wa aina yenu mnaokazania udini kazi yenu ni kuleta mifarakanyo tu katika taifa hili.
Najua hili la kutajwa Waislamu walipigania uhuru wa nchi hii linakuchukiza sana!
 
"Unajuwa" Kwani wewe nani?
kama kuna kinacho nichukiza ni watu wa aina yako mnaoweka dini kuwa mbele ya u-Tanzania wenu. Watu wa aina yenu siyo wengi.
 
Ukijua chanzo cha Mgogoro wa pioneers wa makanisa ya kilokole ya akina Moses Kulola na wenzie kilichoanza miaka ya 1980's mpaka kugawanyika utafunguka macho sana.
It seems wabongo wengi wako gizani na operesheni za serikaki ktk makundi haya ya dini.
Haya ya udini na kurundika watu kwenye makundi dhidi ya u-Tanzania wetu sote hayanipi mwamko wowote wa kuyashabikia.
 
Ni wapi niliposema "amenichukiza"?
Hao waliopigania uhuru hawakuwa waTanganyika? Uislamu wao au ukristo wao una maana gani katika mapambano ya kupata uhuru?
watu wa aina yenu mnaokazania udini kazi yenu ni kuleta mifarakanyo tu katika taifa hili.

Ninatambua unapenda umoja wa kitaifa lakini hilo haliondoi ukweli kuwa kuna demographies. Na watu wanaweza kuwa grouped kwa jinsia zao, Age zao (watoto, vijana , wazee etc), Dini zao, Vipato vyao, Elimu zao, Mirengo yao ya kisiasa (uliberali, conservatism etc).

Na demography zote hizo zina aina ya vitu vinavyozifanya zitick. Hata wanasiasa wakienda mikoa ya waislamu wengi wakitaka kuconvince watu kwa kutumia scriptures watamquote mtume, wakienda kwenda kwenye audience ya wakiristo wengi usishangae wakimquote Yesu zaidi.

Hadi miaka ya 1960's Sensa ya Kikoloni ilikuwa inataja demographies za watu ikiwemo dini zao. Kwa hiyo inajulikana wazi ni mikoa gani ilikuwa na watu wa aina gani.

Again, Najua unapenda Umoja wa Kitaifa, hutaki movenent ziangaliwe kwa jicho la dini, Lakini facts are facts.

Je nikisema kuwa CUF ilikuwa ikiungwa mkono na Waislamu zaidi nitakosea?
 
"Unajuwa" Kwani wewe nani?
kama kuna kinacho nichukiza ni watu wa aina yako mnaoweka dini kuwa mbele ya u-Tanzania wenu. Watu wa aina yenu siyo wengi.
Nakujua siku nyingi unachukia sana Waislamu na Uislamu. Utafanyaje sasa mana Uislamu upo sana tu. Jutahidi kuvumilia hata kama una chuki
 
Back
Top Bottom