Wajaluo wakimbeba John Hanning Speke kumpeleka lilipo Ziwa Victoria ili aligundue

Wajaluo wakimbeba John Hanning Speke kumpeleka lilipo Ziwa Victoria ili aligundue

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2021
Posts
1,117
Reaction score
3,153
Wajaluo wakimbeba John Hanning Speke kumpeleka lilipo Ziwa Victoria ili aligundue.
IMG-20240329-WA0332.jpg
 
Wajaluo wakimbeba John Hanning Speke kumpeleka lilipo Ziwa Victoria ili aligundue.View attachment 2948913
Ndugu zangu,
Nina kitabu nimeandika miaka miwili iliyopita.

Baada ya kusoma hii post ya Speke nimeona niweke kipande kifupi katika yale ambayo nami yamenifikirisha na nikayaandika katika kitabu cha maisha ya Rajabu Ibrahim Kirama:

''Msimamo wa Bruno Gutmann wa kuwaheshimu Wachagga katika maandiko yake akiwaonesha kama watu waliostaarabika ulimletea upinzani mkubwa kwao Ujerumani na katika duru ya wasomi wa enzi zile.

Haikuyumkinika kwao kuwa lile bara ambalo wao waliliita, “Dark Continent”, yaani “Bara la Kiza”, liwe na watu waliostaarabika.

Inasikitisha sana kuwa hawa Wamishionari hawakueleza uhusiano wao na wale Waafrika ambao wao waliwategemea kwa mengi katika safari zao. Hii ndiyo hali iliyopo katika historia nzima ya Wachagga.

Ingekuwa kama si kwa Susi na Chuma kubeba mwili wa David Livingstone kuufikisha Bagamoyo huenda watu hawa ambao walikuwa karibu sana na Livingstone wasingefahamika.

Chuma anafahamika kwa jina moja tu lakini kwa bahati nzuri mwenzake kabahatika kujulikana kwa majina yake mawili - Abdallah Susi.

Inafahamika kuwa Johannes Rebmann alifikishwa kuuona Mlima Kilimanjaro kwa msaada wa Wakikuyu lakini katika historia hii hakuna hata jina moja la Mkikuyu waliyoongozana nae katika safari hiyo limetajwa.

Baada ya hawa Wamishionari kufika Uchagga wakaiandika historia ya Wachagga historia hii ambayo haikuwa imeandikwa popote.

Historia yote, Wazungu waliipokea kutoka katika kumbukumbu ambazo zilikuwa zimehifadhiwa katika vichwa vya watu.

Iwe iwavyo Johann Krapf alipofika Usambaa mwaka wa 1848, nchi ambayo haikuwa mbali na Uchaggani kwa Chifu Kimweri, alimkuta Kimweri katika mahakama yake Vuga.

Alikuwa akihukumu mashauri ya raia zake huku akisoma na kuandika kwa herufi za Kiarabu na amevaa kanzu, juba na amepiga kilemba kama kile wanachofunga Waarabu wa Omani.

Watoto wake pia walikuwa wanajua kusoma na kuandika.

Na bila shaka raia zake pia walikuwa wanajua kusoma na kuandika.

Chifu Kimweri alikuwa na uhusiano mzuri na sultani wa Zanzibar.

Krapf akiwa mmishionari aliyekuja kueneza Injili bila shaka hasad iliingia katika nafsi yake kwa kushuhudia, kwa macho yake, kuwa kama ni suala la kumjua Mungu, Mwenyezi Mungu alikuwa anafahamika na kuabudiwa si pwani ya Bahari ya Hindi alikoingilia kuja Afrika ya Mashariki bali hata bara.''

Inachekesha kuwa Speke abebwe na wananchi wampeleke kwenda kulivumbua ziwa Victoria kama Wakikuyu walivyowapeleka Krapf na Rebmann kwenda kuuvumbua Mlima Kilimanjaro.

1711797656371.png
 
Muafrika kuwa mpole hii sio kawaidaView attachment 2950303

Hata kumpondaponda mkasepa zenu hii akili waliikosa?
Watu weusi ni jamii dhaifu kuliko jamii zingine zote duniani

Ni dhaifu zaidi kiakili, kiubunifu na kimbinu ndio maana popote walipo wao ndio Watumwa...hata hapa nchini Watu weusi ni watumwa kwa Wahindi mpaka leo hii
 
Back
Top Bottom