Wajaluo wakimbeba John Hanning Speke kumpeleka lilipo Ziwa Victoria ili aligundue

Ungeenda shule usingekuwa na maswali kama haya. Nakusaidia tu kwa kifupi historia imesahishwa mara nyingi sana.
Historia Ipi wewe mmatumbi umesahihisha? Nipe mfano mmoja tu. Ulienda kukaririshwa hukupata kuelimika. Vinginevo hata lawama hii usingetoa kama ungeelimika japo kwa theluthi
 
1712043223162.png
 
Dude at this juncture i am done with you. You can't engage in any scholary discourse coherently. You are all over the place clinging to whatever your fingertips can hold onto.
What makes you think I can engage in a constructive conversation with an Uncle Tom? Go eat di*k.
 
Hata kuwatesa watu kwa kuwafanya wakubebe hivyo ni Ubaya na Ukatili
Wammeba kwa hiari Yao na sio kulazimishwa,niliongeana mtu alisem zamani ulikuwa usafiri huo unalipia.
So mzungu ni abiria kama wengine ambao hawakuwa na technology ya picha
 
Ndugu zangu,
Nina kitabu nimeandika miaka miwili iliyopita.

Baada ya kusoma hii post ya Speke nimeona niweke kipande kifupi katika yale ambayo nami yamenifikirisha na nikayaandika katika kitabu cha maisha ya Rajabu Ibrahim Kirama:

''Msimamo wa Bruno Gutmann wa kuwaheshimu Wachagga katika maandiko yake akiwaonesha kama watu waliostaarabika ulimletea upinzani mkubwa kwao Ujerumani na katika duru ya wasomi wa enzi zile.

Haikuyumkinika kwao kuwa lile bara ambalo wao waliliita, “Dark Continent”, yaani “Bara la Kiza”, liwe na watu waliostaarabika.

Inasikitisha sana kuwa hawa Wamishionari hawakueleza uhusiano wao na wale Waafrika ambao wao waliwategemea kwa mengi katika safari zao. Hii ndiyo hali iliyopo katika historia nzima ya Wachagga.

Ingekuwa kama si kwa Susi na Chuma kubeba mwili wa David Livingstone kuufikisha Bagamoyo huenda watu hawa ambao walikuwa karibu sana na Livingstone wasingefahamika.

Chuma anafahamika kwa jina moja tu lakini kwa bahati nzuri mwenzake kabahatika kujulikana kwa majina yake mawili - Abdallah Susi.

Inafahamika kuwa Johannes Rebmann alifikishwa kuuona Mlima Kilimanjaro kwa msaada wa Wakikuyu lakini katika historia hii hakuna hata jina moja la Mkikuyu waliyoongozana nae katika safari hiyo limetajwa.

Baada ya hawa Wamishionari kufika Uchagga wakaiandika historia ya Wachagga historia hii ambayo haikuwa imeandikwa popote.

Historia yote, Wazungu waliipokea kutoka katika kumbukumbu ambazo zilikuwa zimehifadhiwa katika vichwa vya watu.

Iwe iwavyo Johann Krapf alipofika Usambaa mwaka wa 1848, nchi ambayo haikuwa mbali na Uchaggani kwa Chifu Kimweri, alimkuta Kimweri katika mahakama yake Vuga.

Alikuwa akihukumu mashauri ya raia zake huku akisoma na kuandika kwa herufi za Kiarabu na amevaa kanzu, juba na amepiga kilemba kama kile wanachofunga Waarabu wa Omani.

Watoto wake pia walikuwa wanajua kusoma na kuandika.

Na bila shaka raia zake pia walikuwa wanajua kusoma na kuandika.

Chifu Kimweri alikuwa na uhusiano mzuri na sultani wa Zanzibar.

Krapf akiwa mmishionari aliyekuja kueneza Injili bila shaka hasad iliingia katika nafsi yake kwa kushuhudia, kwa macho yake, kuwa kama ni suala la kumjua Mungu, Mwenyezi Mungu alikuwa anafahamika na kuabudiwa si pwani ya Bahari ya Hindi alikoingilia kuja Afrika ya Mashariki bali hata bara.''

Inachekesha kuwa Speke abebwe na wananchi wampeleke kwenda kulivumbua ziwa Victoria kama Wakikuyu walivyowapeleka Krapf na Rebmann kwenda kuuvumbua Mlima Kilimanjaro.

Sasa mbona kwenye kava...Umemchora mtu aliyevaa kama wakoloni wa kiarabu na kuna majina ya kiarabu na sio kibantu.
Au ndio mzee wangu unawapromoti wakoloni wa kiarabu na mazalia yao ya wafuasi wao wa kibantu...na sio wabantu.
Kitabu chako bila hata kukisoma.....kinaonekana kunawapromoti wakoloni wa kiarabu na dini yao...!!
 
Waafrika tunakosea sana kujaribu kuruka hatua za maendeleo ya jamii yetu bila hata kujiaandaa, hii picha iwe ni kweli au si kweli Ila inatokana na matukio ya kweli.

Hapo ni Miaka ya 1800s wazungu walikuwa tayari wana miundombinu yote, barabara, reli, hospital, shule, vyuo Vikuu, wameshaanza kuandika faida na hasara za Upebari na Ujamaa, ni Miaka 100 tangu Industrial Revolution ianze.

Sisi waafrika Miaka hiyo hata viatu hatuna, shule za umma hatuna, hatujui uchumi wa soko yaani yuko nyuma Miaka 800 na zaidi, mwaka 2024 Tanzania ndio nchi yenye SGR ndefu Africa nzima na haijaisha, umeme wa mgao,

Alafu kuna waafrika wanataka nchi iwe ya kipebari, sijui soko huria tubinasishe kila kitu, wakati ilatakiwa tuwekeze kuwasomesha watoto wetu watoe ujinga kwanza
 
Ndugu zangu,
Nina kitabu nimeandika miaka miwili iliyopita.

Baada ya kusoma hii post ya Speke nimeona niweke kipande kifupi katika yale ambayo nami yamenifikirisha na nikayaandika katika kitabu cha maisha ya Rajabu Ibrahim Kirama:

''Msimamo wa Bruno Gutmann wa kuwaheshimu Wachagga katika maandiko yake akiwaonesha kama watu waliostaarabika ulimletea upinzani mkubwa kwao Ujerumani na katika duru ya wasomi wa enzi zile.

Haikuyumkinika kwao kuwa lile bara ambalo wao waliliita, “Dark Continent”, yaani “Bara la Kiza”, liwe na watu waliostaarabika.

Inasikitisha sana kuwa hawa Wamishionari hawakueleza uhusiano wao na wale Waafrika ambao wao waliwategemea kwa mengi katika safari zao. Hii ndiyo hali iliyopo katika historia nzima ya Wachagga.

Ingekuwa kama si kwa Susi na Chuma kubeba mwili wa David Livingstone kuufikisha Bagamoyo huenda watu hawa ambao walikuwa karibu sana na Livingstone wasingefahamika.

Chuma anafahamika kwa jina moja tu lakini kwa bahati nzuri mwenzake kabahatika kujulikana kwa majina yake mawili - Abdallah Susi.

Inafahamika kuwa Johannes Rebmann alifikishwa kuuona Mlima Kilimanjaro kwa msaada wa Wakikuyu lakini katika historia hii hakuna hata jina moja la Mkikuyu waliyoongozana nae katika safari hiyo limetajwa.

Baada ya hawa Wamishionari kufika Uchagga wakaiandika historia ya Wachagga historia hii ambayo haikuwa imeandikwa popote.

Historia yote, Wazungu waliipokea kutoka katika kumbukumbu ambazo zilikuwa zimehifadhiwa katika vichwa vya watu.

Iwe iwavyo Johann Krapf alipofika Usambaa mwaka wa 1848, nchi ambayo haikuwa mbali na Uchaggani kwa Chifu Kimweri, alimkuta Kimweri katika mahakama yake Vuga.

Alikuwa akihukumu mashauri ya raia zake huku akisoma na kuandika kwa herufi za Kiarabu na amevaa kanzu, juba na amepiga kilemba kama kile wanachofunga Waarabu wa Omani.

Watoto wake pia walikuwa wanajua kusoma na kuandika.

Na bila shaka raia zake pia walikuwa wanajua kusoma na kuandika.

Chifu Kimweri alikuwa na uhusiano mzuri na sultani wa Zanzibar.

Krapf akiwa mmishionari aliyekuja kueneza Injili bila shaka hasad iliingia katika nafsi yake kwa kushuhudia, kwa macho yake, kuwa kama ni suala la kumjua Mungu, Mwenyezi Mungu alikuwa anafahamika na kuabudiwa si pwani ya Bahari ya Hindi alikoingilia kuja Afrika ya Mashariki bali hata bara.''

Inachekesha kuwa Speke abebwe na wananchi wampeleke kwenda kulivumbua ziwa Victoria kama Wakikuyu walivyowapeleka Krapf na Rebmann kwenda kuuvumbua Mlima Kilimanjaro.

Vipi kuhusu babu yake na tip tip kudai kua ndie aliyevumbua mji wa ujiji???
Hiyo haichekeshi????
Au washirazi kudai kua walivikuta visiwa vya unguja na pemba vitupu????
Hiyo haichekeshi???
 
Back
Top Bottom