ni ngumu
JF-Expert Member
- Sep 25, 2016
- 4,292
- 7,197
Sababu iliyopelekea jamaa kuokoka siyo hizo deal kuwa ngumu,bali kuna sababu nyingine kabisa ni kama tu alipita bara barani akaona pastor anahubiri akakaa ile sehemu kama dakika tano hivi akajikuta ghafla anatubishwa bila hata yeye kuelewa ilikuwaje.
Ila ninachokuambia ni kwamba yule jamaa ilifika mda wakakutana hadi wazungu kutoka ujerumani ambao huwa wanazitafta hizo mali zilizoachwa na mababu zao (maana ramani waliziacha kwa vizazi vyao), yule jamaa amekuja hadi dar (maana ni wa shinyanga) wale wazungu wakamlipia kila kitu hotelini na wakampa hela ya kula million kadhaa then wakamuuliza ni hatua gani wamefikia kipindi wanachimba, jamaaa akawaeleza kila kitu wale wazungu wakamuuliza imekuwaje mfikia hiyo hatua mbona mbali sana bila kutoa kafara, ndiyo wale wazungu wakaanza kumwambia basi nyie mtakuwa na Jini mjerumani, badae mbele sasa ndo amekuja kumtaja kama John ambae alikuwa mjerumani. Sasa ni kwamba kilichokuja kutokea jamaa ndo hivo from no where akaokoka na kabla hajamaliza game na wale wazungu wajerumani na ndo walikuwa wanamsubiei awapeleke hilo eneo ili wakauage umaskini.
NB: kipindi ameitwa dar hotelini na wale wazungu wajerumani anasema pia walikutana na wafanya biashara wakubwa tu hapa tanzania ambao kwa mujibu wake anasema kwenye top ten ya matajiri bongo hawakosekani ila akasema hatowataja majina kwa sababu za kiusalama na akasema hao matajiri wametajirikia mishe hizo hizo za kuchimbua mali za wajeruman then ndo wakaenda kuwekeza kwenye makampuni mengine huko, hiyo stori iko you tube na imetoka tu hivi karbuni kwenye channel inaitwa SYLLUS TV na iko vipande vipande part 1-10
Waitafute hii hapa