Pre GE2025 Wajumbe Mkutano Mkuu CCM wapitisha Rais Samia, Dkt. Mwinyi kugombea Urais 2025
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kwani kulikuwa na shida gani kama wangerihusu wanachama wengine kuchukua fomu na kuomba kuteuliwa?..... Si ndiyo demokarsia yenyewe?
 
Kumbe Samia mwenyekiti wangu, bonge la mjanja; kamteua Wasira kutoka Kanda ya ziwa kwenye wapiga kura wengi,kamteua yule mbunge wa viti maalumu mkoa wa Mwanza,
huku akijifanya hamfahamu hata jina, ili asome azimio la kumteua agombee urais.Azimio hilo lilitakiwa kusomwa na Katibu Mkuu wa CCM ambaye ndiye mwenyekiti wa sekretariati iliyoandaa azimio hilo.
Halafu mkutano ukaiagiza Halmashauri kuu kuwasilisha jina moja kwa mkutano Mkuu ambao tayari umewateua tayari.Duniani maajabu jamani.
Samia kawapiga bonge la surprise.
Lakini Mimi toka jana nilikuwa nashangaa kicheko cha Mangula kuelekea kwa Kinana.Hakikuwa kicheko cha kawaida.
Good Governance and Checks and Balances was purely contravened and impaired!!😭
 
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa amewasilisha hoja kwa mkutano mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa Mwenyeiti wa chama hicho, Rais Samia Suluhu Hassan awe mgombea urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Pia, Kimbisa amesema Makamu Mwenyekiti Zanzibar wa CCM, Dk Hussein Mwinyi awe mgombea urais wa Zanzibar.

Baada ya kutoa hoja hiyo leo Jumapili, Januari 19, 2025 katika kikao hicho kinachoongozwa na Rais Samia, wajumbe wote wa mkutano huo wakasimama kushangilia na kuunga mkono hoja hiyo.

Hoja kama hiyo imetolewa wakati wajumbe wa mkutano huo wakichangia taarifa za utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/25 kwa upande wa Zanzibar na Tanzania Bara.

Hoja za wachangiaji wote zinaeleza kuwa ni kutokana na ubora na ufanisi wa utekelezaji wa ilani wakisema hakuna mbadala wa wawili hao kuwania Urais.

Kikwete Azungumza na Wajumbe Kuhusu Rais Samia Kugombea Urais 2025

"Azimio liwe Rais Samia amechaguliwa kuwa mgombea Rais wa CCM 2025"

Rais mstaafu na Mwenyekiti mstaafu wa CCM, Jakaya Kikwete, alilazimika kutoa busara zake baada ya wajumbe wa mkutano mkuu maalum wa CCM kutaka kuanzisha mjadala kuhusu wagombea wa urais katika Uchaguzi Mkuu ujao kupitia chama hicho.

Katika kikao hicho, ilikubalika kuwa Rais Samia Suluhu Hassan atakuwa mgombea urais wa CCM kwa uchaguzi wa 2025, huku Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, pia akijitokeza kama mgombea mwenye nguvu.



Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemteua rasmi Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wa urais kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Uamuzi huu wa kihistoria unaonyesha imani kubwa na matumaini makubwa ambayo CCM inayo kwa uongozi thabiti na wa kimkakati wa Rais Samia, pamoja na dhamira yake isiyotetereka ya kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025.

Katika kipindi chake cha uongozi, Tanzania imeshuhudia mafanikio makubwa katika ukuaji wa uchumi, ujenzi wa miundombinu, maboresho ya huduma za afya, na kukuza demokrasia kupitia falsafa yake ya "4Rs. Akiwa Rais wa kwanza mwanamke katika historia ya Tanzania, Rais Samia si tu kwamba amevunja vikwazo vya kijinsia, bali pia ameweka viwango vipya vya uongozi shirikishi na wa maono.
View attachment 3206297
Kwa sasa CHADEMA inamuhitaji sana LISSU kuliko MBOWE a.k.a Museveni
 
Mama alishamaliza kusukuma kete zake mapema sana. Watu wamekuja kushtuka ameingi King. Anastahili kwani kama ni maendeleo, yanaonekana kwa macho na wote tunayaishi
 
IMG_20250120_005036.jpg
IMG_20250120_005011.jpg
IMG_20250120_004947.jpg


Imekuwa ni siku ya furaha tele kwa wanachama wa chama cha CCM leo baada ya rais kutangazwa upya mgombea wa CCM 2025.

Wajumbe hawa wote majimbo yako huru naona ubunge unanukia 2025.

Mbunge mtarajiwa kinje na mbunge mtarajiwa faraja.
 
Jpm alituonyesha jinsi katiba yetu ilivyo mbovu...akaondolewa tukaendelea kuikumbatia wapinzani wakalia lisu akasema...Sasa hivi CCM wanalia...hakuna anayeweza kumtoa Samia madarakani labda mwenye mamlaka ya roho yake...
 
Back
Top Bottom