Wakala wa Mzize: Yanga wameamua kufanya kazi unprofessionally

Wakala wa Mzize: Yanga wameamua kufanya kazi unprofessionally

Mchezaji kaamua kubaki Yanga, na Yanga wanamhitaji. Wakala hana choice zaidi ya kuafiki na kukubali.

Sasa akili za kuambiwa achanganye na zake, asije saini mkataba halafu msimu ujao akaja na drama mpya za Yanga hawataki kuniuza.

Unaombwa ubaki katika mazingira ambayo timu za nje zinakuhitaji, huu si wakati wa kujifanya unaipenda Club na kushusha tu wino, ni wakati wa win-win.

KILA LA HERI MZIZE.
 
Login • Instagram
"Mzize ameniambia kuwa wamemuomba abaki sababu wanamuhitaji Msimu Ujao wanashiriki ligi ya mabingwa, nikamwambia kwahiyo imekuwaje akaniambia wamesema watamboreshea maslai watampa mkataba, So hapa nilipo nasubiri mkataba wa Mzize wakishampa ananipatia tunarekebisha Baadhi ya vipengele tunaurudisha"

"Sina mahusiano nao mazuri, lakini ni vile tu wameamua kufanya Kazi unprofessionally , mi sihitaji tuwe marafiki, Wala sihitaji tuwe tunaongea Unaweza Ukatuma E-mail tukakujibu na tukaendelea na mambo mengine akini kwakuwa wameamua kufanya Kazi Unprofessionally na huwezi kuwabadilsha"

-Msimamizi wa Clement Mzize Jasmine Razack

My Take
Ndugu Polepole kuna wahuni wengine huku tunaomba uwachambue
Ngasa part two
 
Watu wa mikia buana,mnajifanya mnamachungu ya Mzize kwenda nje, wakati nyiee mnamrudisha Mwalimu toka wydad kurudi Tz,kama mnajifanya mnapemda Maendeleo mngemuacha wydad ila mmerudisha kipaji Bongo tena
 
Watu wa mikia buana,mnajifanya mnamachungu ya Mzize kwenda nje, wakati nyiee mnamrudisha Mwalimu toka wydad kurudi Tz,kama mnajifanya mnapemda Maendeleo mngemuacha wydad ila mmerudisha kipaji Bongo tena
Mikia hawajielewi
 
Ndio yaleyale yaliyomkuta Jerry Tegete na Mrisho Ngassa
Umjumlishe pia na Selemani Mwalimu aliyesajiliwa simba kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea Wydad Casablanca. Siyo kila siku tunatumia tu mifano ya zamani, na wakati kuna mifano mingine imeongezeka.

Furaha yenu ni kumuona dogo anaenda nje halafu akishindwa kufikia malengo na kurejea nchini, mpate tena cha kusema! Kama ameboreshewa maslahi yake, mtaka nini kingine?

Mbona Fei Toto mnayemsifia kila siku humu jukwaani, haendi kucheza soka nje! Na badala yake ameendelea kubakia kucheza Azam?

Kwenye timu ya simba hakuna wachezaji wazawa wenye sifa ya kucheza nje? Mbona hatuwaoni wakienda?
 
Kuna sehemu nimesema kuwa kuna kibaya?
Nimenukuu kauli ya huyo Jasmine akiongea alichoambiwa na Mzize. Kwa kauli hiyo ni wazi Mzize kaamua kubakia Yanga baada ya kuafikiana kuhusu maslahi binafsi. Sasa mtu anasema Yanga wanafanya kazi unprofessional kisa tu Mzize hajauzwa. Wewe inakuingia akilini?
Sasa aliposema Yanga hawafanyi kazi unprofessional alimaanisha hajauzwa?
Nikupe mfano mmoja timu kuvunja mkataba wa mchezaji halafu usimlipe aende kukushitaki Fifa unafungiwa kwa mda mpk ulipe that professional..?..inshort mgogoro wake na Yanga ni kusema kwa nini Yanga hawajibu ofa za Mzize wanazoletewa,walichokifanya Yanga waliweka price tag ya Mzize $1 million ambayo esperance walifika sasa hapo unprofessional ni nani?..na bado wakagoma kujibu wala kusikiliza ofa lkn kumbe wazi alikua hauzwi na laiti Yanga wangekurupuka mapema kusema hauzwi ingeleta picha mbaya ndo mana'ke wamempa ofa ambayo dogo Mzize kaikubali kwa afya ya soka lake kwnd esperance sababu ya pesa tu isingekua bora kwake kulikoni kupata uhakika wa kucheza...
Cha msingi na muhimu awe na afya njema mbeleni majeruhi yakimuweka mbali mwakani Yanga hawatambakiza sababu atabakiza mwaka mmoja
Lkn huyo mama yupo sahihi kabisaa kwa kazi yake kama wakala alicholalamikia ni kwa nini ofa za Mzize hazisikilizwi na hazijibiwi hapo weeh utahisi vipi?Si unabaniwa?Sio eti kwa nini hauzwi si kweli....ukweli umegeuzwa kuwa uadui...hapo Yanga huyo dada ana wachezaji karibia 5 ambao ana wasimamia huu mgogoro ni mwepesi sana kuulewa kama usipoutazama kwa jicho la kishabiki
 
Huyo Mzize kichwa kama sanduku la kubebea chatu, sijawahi kumtarajia awe na akili timamu. Na kwa hili kathibitisha mtazamo wangu juu yake.
Injinia wa mchongo nae anahusika kwa 100%
Amemlaghai na kumrubuni kijana wa watu...roho mbaya sana yule mbwa ...wasomali Wana roho za paka...
 
Back
Top Bottom