Wakandarasi Tunafilisika. Serikali iangalie utaratibu mzuri wa tenda

Chagueni LISSU. Kwa kweli wakandarasi mmechoka kwelkwel. Kandarasi zote zinafanywa na serikali kuu kupitia TBA, NHC ,JKT. Serikali imehodhi uchumi badala ya sekta binafsi. Kipindi hiki sisi makanjanja tunaweza kumuajiri mkandarasi kusimamia ujenzi wa vyoo vyetu huku mbagala
 
Ni upuuzi kumpa kazi mzawa hata Kama Hana uwezo kwa kigezo cha uzawa hizo ni akili za matope. Mbona songoro anafanya vzr na kazi anapewa? Mjitafakari wananchi wako results oriented.

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Tatizo wakipewa kazi wanaboronga wanasingizia uzawa! Tunataka matokeo, unakuta MTU kapewa kazi haiishi au ubora zero!
Acheni uongo serikali yenyewe haipo tayari kushirikiana na wakandarasi hali ni ngumu mno
Kodi na upatikanaji wa kazi ni mizengwe tupu
 
Ina maana makampuni yote Tanzania hayana uwezo?
Mbona wamesajiliwa na wanalipa kodi zote?
Kwa hio mayanga ya mume mwenza wa Pombe Ndio pekee Wana ubora?
Tumechoka kutawaliwa kidikteta na Familia moja
We can't breathe
Heri umesema ukweli
Wakandarasi wazawa wana uwezo wa kufanya kazi tatizo ni mfumo mbovu wa serikali yetu ni kama wanakomoa wakandarasi
 
Baada ya kupitia michango humu JF yako nimegundua Neno pumbavu unalitumia kila nyuzi unayochangia.
Itoshe kusema huna sifa ya kuwepo JF na naamini una msongo wa mawazo unakusumbua. Heshimu michango ya members wenzako, JF siyo mali yako nawaachia Mods wakupe haki yako I'm sorry, an i ignore you right now Mkuu.
 
Kosa la Nyakirang'anyi ni la kwake binafsi na yeye ni mtu wa mfumo serikali inajua ndio maana wamelifumbia macho.
Kwa taarifa ni kuwa kampuni nyingi za kitapeli ni zile zenye ubia na watu waliopo Serikalini
Kampuni zisizo kuwa na uhusika na SERIKALI zinafanya vizuri
 
Acheni uongo serikali yenyewe haipo tayari kushirikiana na wakandarasi hali ni ngumu mno
Kodi na upatikanaji wa kazi ni mizengwe tupu
Kazi zitapatikanaje wakati mzee kaua kabisa private sector?
  1. Aliagiza kwamba taasisi za serikali zisifanyie mikutano kwenye mahoteli, zifanyie kwenye kumbi zao. Sasa alitaka hawa wamiliki wa hoteli wakale wapi wakati wanailipa serikali kodi. Mapato yatatoka wapi? Waajiriwa wa hizi hoteli wakalazimika kupunguza watendakazi wao
  2. Aliondoa pesa za serikali kwenye benki binafsi na kuzipeleka hazina. Hii imeleta mtikisiko mnene kwenye sekta ya fedha. Kumbuka kwamba pesa hizi ndio ,abenki yalikuwa yanakopesha wakandarasi na wananchi wengine
  3. Serikali imepokonya fedha kwa maduka ya kubadilisha fedha, kwa kisingizio kwamba maduka hayo yanatumika kutakatisha fedha chafu. Kwa nini badala ya kuwapora pesa wasingewawekea utaratibu mzuri wa kutoshawishika kutakatisha pesa?
  4. Kazi za unenzi serikalini wanapewa mawakala wa serikali, i.e. TBA, TEMESA nk. Mpaka hapo bado hujaua sekta binafsi tu?
 
Tatizo wakipewa kazi wanaboronga wanasingizia uzawa! Tunataka matokeo, unakuta MTU kapewa kazi haiishi au ubora zero!
Tatizo rushwa kubwa..hata quotations zinapopelekwa zinapigwa panga, afu utarajie ubora mkubwa kweli. Tusiwaonee, tuwasikilize kwanza.
 

Unaongelea serikali au private sector? Hizo call centres za india ni za Her royal majesty government? Mimi nimesema tender za kujenga barabara na infrastructure na miradi ya government ulaya hutoona wanawapa wachina bali wanawapa wazungu tu. TATA kununua range rover si aliingia kichwa kichwa, private dealing ni maamuzi ya wafanyabiashara wenyewe siyo government hata wewe ukiweza kanunue hata ManU. Ila kwenye government tender wapo na uzalendo siyo kama sisi mabarabara na matenda yoote ya government wanapewa wachina, wadosi na warabu alafu wazawa wanapigwa chini alafu jitu likisimama jukwaani “uzareendo”.
 
Wengine wamefilisika kwa serikali hii kushindwa kuwalipa madai yao kwa muda mrefu
 
Kuna utaratibu wa kutoa tenda na utaratibu huo haujabadilishwa wakati Magufuli amechukua madaraka. Mleta uzi pengine sio Mtanzania atajuaje ya Tanzania? Wivu tu unawauma Tanzania inapaa katika nyanja zote.
Unapaa wewe pamoja na mayanga construction
Sisi mbona hatuoni zabuni zikitangazwa?
Inamaana mayanga inashinda kila zabuni kwa vigezo gani
 
Hawana sababu hizo kwani kampuni zao za wazawa can deliver the same quality, hao wachina wenyewe ujuzi wanajifunza huko.

Lakini kama kampuni inakuja na tender nzuri serikali yao aiwezi kataa 5G ilikuwa ajenge mchina, kuna kiwanda cha umeme kitakachotumia nuclear tender kapewa mchina na atakiendesha for 15 years kabla ya kuwakabidhi serikali and those are sensitive National security investment huko kwao but value for money remains a priority.
 
Mkuu construction industry iko hoi. Si jambo la kisiasa japo approach yake yaweza kuwa ni ya kisiasa. Kuna possibility kubwa kuwa JPM alipoingia madarakani hakukuwa na fedha za kutosha kujenga miundimbinu mingi kwa muda mfupi hivyo akaamua atumie approach ya kutumia taasisi za serikali na majeshi pamoja na force account. Matokeo yake pesa inazunguka ndani ya serikali yenyewe.

Project zinazofanywa na makampuni ya nje kama China mengi ni ya Serikali ya uchina hivyo hata kama serikali haina pesa ya kutosha kulipa kwa wakati bado makampuni hayo yatasaidiwa pesa na serikali yao kutekeleza miradi ya inchini mwetu na pesa italipwa na interest kutokana na delayed payment.

Performance ya kampuni nyingi za kizawa inategemea na cash flow ya mradi husika. Kama nilivyoeleza hapo juu projects nyingi za serikali zinaanza bila kuwa na pesa ya kutosha ama miss allocation ya fund hivyo most ya makandarasi wanaingiza pesa zao kwenye projects na kujikuta hawalipwi kwa wakati hivyo inawalazimu kuomba mikopo yenye riba kubwa bank ili ku-fund project ya serikali na hatimae mzigo wa riba unakuwa mkubwa hivyo kuwa fanya wakandarasi wa under perform. Serikali inatakiwa ilipe riba kwa delayed payment ila huwa hailipi.

Tafiti mbalimbali zinaoyesha kuwa sector ya ujenzi uchangia 75% ya uchumi wa inchi ivyo ikiyumba effect yake inakuwa kubwa sana.
Washauri wa ujenzi nao wanalia ivyo ivyo wengi wamefunga Ofc.

Natumaini this time serikali itakuja na approach nzuri zaidi ya kufufua tena hii sector
 
Unapaa wewe pamoja na mayanga construction
Sisi mbona hatuoni zabuni zikitangazwa?
Inamaana mayanga inashinda kila zabuni kwa vigezo gani
Mbona hako ni kakampuni kadogo tu huoni wanaojenga bwawa la umeme au SGR wacheni wivu wa kike.
 
Mkuu kwenye projects kubwa uwa kuna siasa zake. Uwezi kuta kampuni ya China kwenye mradi wa European Union ama kampuni ya kizungu kwenye Chinese funded projects.
 
Ndugu kumbuka kuna mdudu anaitwa FORCE ACCOUNT.

Huyu mdudu anacho fanya ni miradi kusimamiwa na eng wa halmashauri, akisaidiana na fundi mchundo mmoja kusimamia vibarua.

Hii maana yake nini, prpffesional engineers wengi kazi zao zimechukuliwa na fundi mchundo.

Vituo vya afya karibia vyote vimejengwa lwa force account.. fundi mchundo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…