Wakati gani mtu anapaswa kuwa na mshauri binafsi wa fedha?

Wakati gani mtu anapaswa kuwa na mshauri binafsi wa fedha?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Wataalam wa aina hiyo wanapatikana Tanzania? Nafahamu kuwa Tanzania kuna watu waliosomea masuala ya FINANCIAL PLANNING, lakini sikumbuki kama nimeshawasikia Watanzania wakishuhudia jinsi ushauri wai ulivyowawezesha kufikia malengo yao ya kifedha!

Lakini kupitia baadhi ya vitabu nilivyovisoma, watunzi wamesisitiza umuhimu wa kuwa na financial planner wako binafsi, tena wa kulipwa.

Napenda kufahamu:
1. Ni kweli hao wataalam wana msaada kwa wateja wao?

2. Kuna Watanzania waliowahi kusaidiwa na ushauri wao?

3. Wakati gani unapaswa kuwa na mtaalam wako binafsi wa kifedha? Ukiwa na hali ngumu ya kifedha? Ukiwa tajiri? Ukiwa unataka kufanya biashara?

4. Ni sahihi kwa mtu ambaye si "tajiri" kuwa na "financial planner" wake binafsi?
 
Muhimu sana kuwa na Mentor mkuu!!, Kila hatua ya maisha hata kipindi unaanza biashara ndogo.

Mentor anakusukuma kufanya kilasiku hata pale unapokua hujisikii, anakupa moyo wa kutake Highrisks ambazo ndizo huleta matunda.
 
Nafikiri MENTOR na FINANCIAL PLANNER/FINANCIAL ADVISOR ni watu wawili tofauti.
 
Kitaalamu wanasema ukiona unaazima kitu zaidi ya mara 2 ndani ya muda mfupi, unapaswa kununua kitu hicho. Mfano pasi ya nguo n.k. Tukija kiuchumi ,Ukiona malengo yako ni makubwa na ujuzi huna eneo husika, ajiri kwa muda mtaalam wa eneo hilo ,hapo tunaita KUKUA
 
🙏🙏🙏
 
Tumia financial consultants ,inamlipa pale unapohitaji msaada tu,kuwa na elimu kunapunguza gharama,na huitaji kuwa na elimu kubwa Kuna vyuo vinatoa kozi fupi ktk mambo ya msingi tu na unaweza soma online.
🙏🙏🙏🙏

Labda mkuu unaweza kupendekeza aina ya kozi fupi kwa mtu asiye na background ya taaluma ya fedha? Inachukua muda gani? Wapi?(hata kama ni nje ya nchi)
 
Muhimu sana kuwa na Mentor mkuu!!, Kila hatua ya maisha hata kipindi unaanza biashara ndogo.

Mentor anakusukuma kufanya kilasiku hata pale unapokua hujisikii, anakupa moyo wa kutake Highrisks ambazo ndizo huleta matunda.
Nina kitu nataka kufanya sijui pakuanzia msaada wenu
 
Hela yangu niitafute kwa jasho na damu halafu aje mtu tu anishauri namna ya kuifanyia? Ukiona umefikia hatua hiyo hata hujuyi pesa yako uifanyie nini si bora uache mara moja kutafuta zingine!
Mkuu, mbona ndivyo wafanyavyo "wakubwa " huko duniani? Wanafanya hivyo ili waendelee kupata hela nyingi zaidi kwa kutumia "mawazo" ya wengine badala ya damu na jasho lao pekee!

Wazo moja sahihi linaweza kubadilisha hali yako ya kifedha "milele"
 
Kitaalamu wanasema ukiona unaazima kitu zaidi ya mara 2 ndani ya muda mfupi, unapaswa kununua kitu hicho. Mfano pasi ya nguo n.k. Tukija kiuchumi ,Ukiona malengo yako ni makubwa na ujuzi huna eneo husika, ajiri kwa muda mtaalam wa eneo hilo ,hapo tunaita KUKUA
mtalaam wale wanaoazima zaidi ya mara mbili huoni kwamba wanabana bajeti?
 
Pale utakapo kuwa na uwezo wa kupata fedha nyingi.mfano bilioni Moja na kuendelea
Kuna kitabu kimoja nilikisoma, mwandishi anashauri watu wenye madeni wawatafute washauribwao binafsi wa kifedha, tena wa kuwalipa, ili wawe wanawasaidia kupangilia fedha zao. Unafikiri wazo kama hilo ni "applicable" huku kwetu? Kwamba financial advisors/planners wanaweza kukusaidia (kwa ushauri wao wa kitaalam) kutoka kwenye hali duni ya kifedha? Nilitamani pia nijue kama kuna Mtanzania wa kipato cha kawaida alishawahi kuwatumia hao wataalam na matokeo yakawaje!
 
Mkuu, mbona ndivyo wafanyavyo "wakubwa " huko duniani? Wanafanya hivyo ili waendelee kupata hela nyingi zaidi kwa kutumia "mawazo" ya wengine badala ya damu na jasho lao pekee!

Wazo moja sahihi linaweza kubadilisha hali yako ya kifedha "milele"
Sawa mkuu mimi huko siwezi fika.
 
Back
Top Bottom