Halafu kumbe wewe jamaa mpira haujui umekarir. Katika mpira Kuna aina mbili za usajili wa wachezaji.
1) usajili wa mchezaji wa kawaida mwenye kipaji au anayejua mpira.
2) usajili wa mchezaji ambaye anavuma yaani mchezaji nyota (aliyepata mafanikio
Kwenye hiyo namba moja ndio pale unapoona mchezaji asiyekuwa na jina akajakuwa nyota na wa kuogopewa. Embu nitajie wachezaji wa Simba walau saba walioifikisha Simba robo fainali CAF mbao walikuwa na mafanikio huko walipotoka kabla ya kuingia Simba.
Kingine ni kwamba kusajili nyota haikufanyi uwe na 100% kuwa unaenda kukipata ulichokitaraji na ndio maana unaona mchezaji ana jina kubwa lakini akienda club nyingine anakuwa garasa tu. Na ndio maana unaambiwa usajili ni kamari, usajili ni bahati nasibu. Tshabala ambaye alidumu Simba miaka tele na kuiwezesha Simba kufika robo fainali alitokea timu ya nchi gani kabla ya kuja Simba?