Wakati Tanzania ipo busy na masuala ya Simba na Yanga, Wakenya wanazidi kutupiga gap. Ujerumani imekubali kuwapokea Wakenya 250,000

Wakati Tanzania ipo busy na masuala ya Simba na Yanga, Wakenya wanazidi kutupiga gap. Ujerumani imekubali kuwapokea Wakenya 250,000

Natumaini mu wazima humu, ni siku nyingine tukiwa bado tunasubiri muafaka wa mchezaji Kagoma kama atabaki Simba au atarudi Yanga, Mzee wetu magoma na yeye ni mpaka kieleweke !!,

Anyway tukirudi kwenye kichwa cha habari, Ujerumani imekubali kuwapokea Wakenya 250,000 na kuwapa nafasi za kufanya kazi nchini humo.

Makubaliano hayo yamefikiwa kati ya Rais William Ruto na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz.

Tayari madereva Watano toka Kenya wamefika kwenye mji wa Flensburg Ujerumani kupitia mpango huu. (Maderva hulipwa wastani wa euro 14 / shilingi elf 42 kwa saa)

Lugha kuu ujerumani ni kijerumani lakini asilimia 56 ya watu Ujerumani wanaweza kuongea kiingereza, ni sawa na kwenda Uganda unaweza usijue lugha yao ya kiganda lakini ukijua kiingereza inasaidia, inakuwa rahisi zaidi kujifunza kijerumani taratibu unapojua kiingereza.

Faida..
  • Fursa za kujiongeza kielimu na kupata kazi zenye mishahara ya kizungu (Mwalimu analipwa milioni 8 kwa mwezi)
  • Kupunguza tatizo la wahitimu wengi wasio na ajira Kenya, hata kwenye ajira za kiswahili mfano walimu wa kiswahili na watangazaji wa vituo vya Idhaa za Kiswahili kama BBC na DW, wakenya ni wengi na wanaenda kujazana zaidi.
  • Kupata connections za biashara za kimataifa, Mfano kununua maparachichi Tanzania kwa mia mbili, kuyauza ujerumani kwa elf 5.
  • Diaspora inazidi kupanuka, baadhi ya sehemu kunakuwa na vijiji / mitaa iliyojaa wakenya
  • Inakuwa rahisi kwa wakenya kuingia ujerumani wakiwa na ndugu, marafiki na jamaa waliojaa nchini humo.
  • Wakenya kupata fursa za kutumia vipaji kupata pesa zaidi, Kuna vijana wadogo ujerumani wanacheza mpira wanakunja milioni 200 kila wiki.
  • n.k.
Ni vile naheshimu sheria za JF nineanza na maneno yasiyofaa kwa serikali ya Tanzania.

Hii serikali yetu inastahiki kulaaniwa na kila mpenda maendeleo.

Nchi imejaa viongozi wabinafsi, wakatili na wasio na utu kuanzia juu hadi chini
 
moja kati ya vitu vizuri alivyofanya Kikwete ni kurudisha waTanzania waliopo nje na kuwapa nafasi za ndani kuendeleza nchi, ni ujinga, narudia tena ni ujinga kujisifia kutoa workforce ya Nchi kupeleka Nchi nyengine, just imagine mtoto kasoma msingi bure, sekondari bure, Chuo na Heslb zote hizo ni kodi za wananchi halafu akaifaidishe ujerumani wakati nchi hapa hata wataalamu hatuna?
 
mtoto wa mkulima anamaliza chuo una ajira ya kumpa ? una mtaji wa kumpa ?

Viongozi wananunua vx za milioni 300 kwa kodi zetu finyu, miradi ya ajira na pesa za kuwapa mitaji rafiki wahitimu inatoka wapi kwamfano ?
 
mtoto wa mkulima analiza chuo una ajira ya kumpa ? una mtaji wa kumpa ?
it doesnt matter kapata ajira ndani ama hajapata ila kutoa resource za nchi nje ni ujinga, na usifikiri Ujerumani wana Target mtoto wa mkulima, wakitaka daktari wanachukua yule bingwa mwenye uzoefu, wakitaka injinia hawachukui mwenye gentleman ambaye anahangaika na bahasha, wanataka first class mwenye uzoefu. kesho na keshokutwa mgonjwa wa mguu akifanyiwa operation ya kichwa mtalalamika hali ya kuwa top cream za nchi mnazigawa.

watu ni resource kama madini na bandari, kama unaamini madini yanaibiwa na ni sawa kutoa watu 250K uwapeleke nchi nyengine basi tuna safari ndefu sana.
 
ndio hivyo mkuu, kuna wasomi kibao wapo mitaani Kenya wenye gpa za maana, hakuna ajira wala mitaji, wanaenda kupunguza makali Ujerumani, wakenya 250,000 si haba, ni wengi wanaenda kupata nafuu ya maisha Ujerumani
 
ndio hivyo mkuu, kuna wasomi kibao wapo mitaani Kenya wenye gpa za maana, hakuna ajira wala mitaji, wanaenda kupunguza makali Ujerumani
Again Soma comment yangu vizuri, they won't take those jobless, watachukua top cream za Nchi, sio mara Ya kwanza na wala haitakua mara ya mwisho.
 
Again Soma comment yangu vizuri, they won't take those jobless, watachukua top cream za Nchi, sio mara Ya kwanza na wala haitakua mara ya mwisho.
kuna wakenya wengi hawana ajira rasmi na wana gpa kubwa wapo mitaani, cv tayari zinaonyesha wameshajitolea taasisi kadhaa, experience ipo ya kutosha tu !!

vigezo vikuu vitakuwa elimu na uzoefu, watu wapo mitaani ila cv zimesimama
 
Tayari madereva Watano toka Kenya wamefika kwenye mji wa Flensburg Ujerumani kupitia mpango huu. (Maderva hulipwa wastani wa euro 14 / shilingi elf 42 kwa saa)
Una hakika na hiyo pesa wanauolipwa mzee Mimi nichukue uraia wa Kenya saa hii
 
moja kati ya vitu vizuri alivyofanya Kikwete ni kurudisha waTanzania waliopo nje na kuwapa nafasi za ndani kuendeleza nchi, ni ujinga, narudia tena ni ujinga kujisifia kutoa workforce ya Nchi kupeleka Nchi nyengine, just imagine mtoto kasoma msingi bure, sekondari bure, Chuo na Heslb zote hizo ni kodi za wananchi halafu akaifaidishe ujerumani wakati nchi hapa hata wataalamu hatuna?
Kwa hiyo nchi hii wataalamu wote wana ajira?
 
Una hakika na hiyo pesa wanauolipwa mzee Mimi nichukue uraia wa Kenya saa hii
kima cha chini kabisa cha kazi yoyote ujerumani ni euro 12.4 (elf 37) kwa saa), maisha yapo juu sana lakini ukitunza pesa unaweza kupata pesa nyingi kwa maisha yetu ya Afrika
 
Hii deal ilisainiwa zamani sana.
Berlin has agreed to allow skilled and semi-skilled Kenyan workers into Germany in a controlled and targeted labour migration deal. Kenya is struggling with increasing difficulties in providing work and sufficient income for its young professionals, while Germany is facing a shortage of skilled labour.11 hours ago umeona jana tu. Sio yasiku nyingi
 
Wao wachache hivyo sisi tushauzwa wote hata wewe mtoa mada huko saudi arabia na mkataba ushasainiwa
 
Kasome huu uzi afu angalia ni wa lini niliweka link inayohusu hii habari comment #13. Hii agreement ilikua tayari toka mwanzo wa mwaka ilikua bado kusign tu ambako ndo kumefanyika Leo.

Nchi zenye watu walioelimika, skills na wanaojua lugha wanaingia mikataba ya hivi toka miaka ya zamani sana ndo maana unaona wakenya, Nigerians wapo nje kibao. Nchi zao zinafanya jitihada za makusudi kabisa to export skilled labors to curb the unemployment crisis. In return hao watu wanatuma remittances inayochangia pato la taifa kuliko wizara zenu zote combined.

Deal inakuwa "deal" wakati sahii zikiwekwa!
 
Achana na takwimu zako kutoka unknown sources na wikipedia,
Uliza walio na Experience ya kuishi Ujerumani watakwambia jinsi ilivyongumu kama huwezi kuongea kijerumani. Sipingi uwepo wa wazungumzaji wa kiingereza Ujerumani hata hapa Tz wapo pia shida ni nyinyi kulazimisha watu waongee English kama lugha ya Kwanza mkihisi ndo inafanya watu wapate fursa. Huo ni upuuzi
Kama ni "upuuzi" basi waJerumani na waKenya ni wapuuzi kwa kukubaliana upuuzi huo!
 
kuna wakenya wengi hawana ajira rasmi na wana gpa kubwa wapo mitaani, cv tayari zinaonyesha wameshajitolea taasisi kadhaa, experience ipo ya kutosha tu !!

vigezo vikuu vitakuwa elimu na uzoefu, watu wapo mitaani ila cv zimesimama
Seems like Comprehension sio strong suit yako. Usijali endelea kudanganya wenzio.
 
Tanzania ni pazuri kuishi, kuna amani na utulivu. Kenya nchi yao siyo nzuri kama Tanzania ndiyo maana wanakubali kuomdoka nchini mwao.
Tanzania hata wazungu wanalilia waende wakaishi
Amani kwenye njaa?bongo kuna ukimya wa kulazimishwa? Siku moja amka asubuh uende hospital ya ocean load, au, muhimbili kule dar, au, General Hospital Dodoma, uone u maskini wa wa Tanzania,
Wabongo tunabanwa tusiondoke nchini,kupata passport ni shida, unajua, balaa la ukosefu wa ajira,? Elimu yetu duni, bongo hapa hapa viwanda na ma kampuni yanaona wasomi we tu ni vilaza, hawaajiriki, sasa, wataondokaje waende nje? Kama hauajiriki bongo, utaajirika vipi ulaya na America? Acha uzwazwa!
Kenya wanaenda nje, maaana, elimu wanayo, na, wanakubalika Sana kwa, uchapa kazi wao, nimefanya kazi, na wa Kenya hapa bongo tangu miaka ya 2000,kijana mwenye diploma kutoka Kenya, ana ujasili na anajiamini kuliko kijana mwenye masters wa bongo,
Nilijifunza vingi Sana kutoka kwao, Mkenya yeye anajiona ni grobal citizen, popote kambi, haoni hatari kuhamia kama mafinga, au, masasi,anaoa au kuolewa, anaomba uraia maisha ya naenda, wakati wabongo, anaona Bora ajibane Dar, ili mradi weekend aende club,
 
Back
Top Bottom