Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

Mimi siji kusahau hii
kuna jamaa yangu tulikutana mtaa akanipa dili la kuchimba mashimo ya nguzo za Tanesco; kila shimo moja futi sita sh elfu 10.nikimchek jamaa alienipa dili ni mchovu tu,nikamuuliza yeye anachimba mangapi kwa siku? akasema mpaka 4

Bana tukaenda asubuhi full kugombeana sululu na ma makoreo mimi nikafanikiwa kupata spade tukapanda gari..kumbe tunaenda mlima kawetele kama ushawahi fika mbeya unaujua.

Kwanza kufika tu juu ya mlimani nimeshachoka balaa tukapewa eneo la kuchimba bahati mbaya duu unapiga sululu mia unachota spade mbili yaani mwambaa...... nimechoka kuandika ngoja nipige kamtungi kwanza!!
 
Huyo alikuwa anataka kukuuza kwa maharamia

sent from toyota Allex
 
Ebana ee mwaka 2016 ulinikuta nipo vibaya sio kitoto , niliomba kazi ya kibarua kwenye ujenzi wa ghorofa moja lipo katikati ya jiji moja , kulikuwa na kazi ya kuchimba mashimo ya nguzo za ghorofa urefu, upana na kimo vyote viwe 240cm shimo moja sh 40,000 , tulichimba asee asikwambie mtu , kuna layer kama nne wakati mnachimba mara mkute walimwaga kokoto , ardhi ngumu sio kitoto mwanzoni nilijua kazi ingeisha kwa siku mbili lakini tulijikuta wiki moja inakata tupo hapo hapo maana tulikuwa wawili jamaa siku ya tatu akakimbia show, Sasa ubaya ni kwamba msimamizi analipa hela mwisho wa kazi, sitasahau hasara niliyoipata maana hela iliisha kwa mama ntilie na nauli ya kurudi geto
 
Da hiyo inaitwa ajali kazini

sent from toyota Allex
 
Mkuu ulikosea ungetafuta mabintibwa kukusaidia wanalipwa kwa siku 1500 ....ulibaki kidogo ungetoboa

sent from toyota Allex
 
Dah hatari we jamaa umenchekesha balaa ko vp jamaa yako alikua karani kweli au

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka 2010 baada ya kumaliza f6, niko kitaa sina moja wala2, naona gazeti la udaku, nafasi za kazi mshahara mnono, kesho yake naenda kwny intaviu, nashangaa kupewa chupa za chai na mabeseni, tukaenda tegeta huko, unamsaundisha mtu eti themos inaweza kuchemsha maharage halafu hanunui. Aisee we acha tu, hata chakula hakuna, tulishindia mihogo. Kwakweli kesho yake sikurudi tena, kwani miguu ilikuwa haifai kwa maumivu. Maisha haya...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…