Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

Pole sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesoma uzi huu kwa kweli watu wamepitia msoto Ila maisha safari wengi washatoboa wachache wapo kwenye situation.
Mine is a little different
Mara tu baada ya kumaliza elimu yangu ya chuo haukupita mwezi nikapata kazi kwene international NGO mshahara ulikua unatosha na safari kibao.
Nilifanya kwa muda wa miaka 9.baada ya hapo kazi ikakata nyumba ipo kwa linta.kiinua mgongo nilichopata Kama milioni 4 kutoka kazini nikaezeka upande.ujenzi ulinila sana hela sikua na ramani yoyote nyumba niliyokua nakaa Kodi imeisha.nikahamia kwangu.
Nilitamani kila kazi kuanzia kuuza nyanya hadi maandazi nilishawahi fanya kazi nalipwa 90 kwa mwezi niliona muujiza
Fikiria kutoka mshahara wa milioni 2.8 mpaka elfu tisini na nikashukuru jinsi msoto ulivonikamata
Japo Bado nasota Ila angalau nilipata kazi za hapa na pale za mwezi mwezi Ila nimejifunza kwamba.
Kujijenga ni muhimu hata kama una ndugu wanakuzunguka

Nikikumbuka kipato changu chote miaka 9 nimeishia kuwasomesha wadogo zangu ambao kwa Sasa wananidharau inanouma
 
Sorry lakink kwani ulijua kazi ni ya milele au kuacha ilikuwa ni ghaflaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mngepanga siku nyingine mvunje kiuno hata Mwarabu mmoja


Sent using Jamii Forums mobile app

Kiukweli tulipanga kisasi cha mda mrefu kama tungefanya mda ule tungekuwa jela sasa hivi, ila hakikufanikiwa maana boss nilirudi full time school afu nikaja home dar kwa mshua baada ya hilo balaa, nilikuwa nna mabalaa sana moshi mtukutu kweli kweli
 
Daah mkuu ulijitoa haswaa!!
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimerudia kusoma ×5

YAANI UMESEMA

Mshahara 2.8M
Umefanya miaka 9

Mshahara 2.8M
Umefanya miaka 9

Mshahara 2.8M
Umefanya miaka 9

Then umeachishwa kazi huna kitu.

Hivi ni sijaelewa au sijasoma vizuri.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Samahan sana wadau nimechelewa kuchangia huu mjadala heavy asikwambie mtu maisha kuna kipindi yanakaza kiasi mtu unanyongorota kabisa km sio kupinda kuna kkipindi nilipewa tender ya kulinda shule aisee ile kaz km huna chale itakoma yaan kuna kipindi usingiz unakuchukua unasikia km kuna mtu anakutikisa uamke unaamka huonk mtu mara unasikia nje kuna mtu anakuita unachungulia dirishan huoni mtu kuna siku nilizabwa vibao na mtu nisiyemuona toka siku nikaacha
 
Ungeendeleza Ile ari yako ya 'sitaki shida mm' yngeshatoka huko serikalini. Nimecheka sana kwenye unywaji na uvutaji, na bado hukutetereka masomoni!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msoto nimeuanza kitambo sana wakuu mpaka sasa napambana na bado sijaiona nuru.
1999-Kisanga kilianzia hapa.
Huu mwaka mambo yalizidi kuwa magumu sana kwa upande wa bi.mkubwa(mama),kipindi hicho nakaa na bi.mkubwa tu tumepanga nyumba ya bibi fulani ni mchawi balaa,yani full mauza uza hiyo nyumba.
Mambo yakazidi kuwa magumu balaa,bi.mkubwa akaona eeh hii ngoma ngumu,acha anipeleke kwa baba yangu (hapo tangu nazaliwa 199* sijawahi kumuona huyo wa kuitwa baba). Hata bi.mkubwa kuna muda alikua ananifanyia vitu hadi najiuliza huyu ni mama angu mzazi kweli?. Anyways tuyaache hayo..
Nakumbuka nilisafirishwa kutoka Bukoba-Rwamishenye mpaka Dodoma kama bahasha inavyoagizwa katika bus. Na kipindi hicho usafiri mkubwa ilikua ni meli mpaka Mwanza then train(gogo) mpaka Dodoma,to be the honest kipindi hicho nilikua na miaka 5.

Nilipofika Dom..
Kufika Dodoma nikakutana na mother wa kambo jau sanaaa,hapo ndio nikaanza kunyimwa msosi live huku nauona huu hapo,mixer vile visa vyote vya step mother nishapitia.
Njaa ilipozidi nikawa napita mitaani katika zile nyuma wanauza maandazi nje either ni barazani au pembezoni,nikawa naiba sana yale maandazi ya watu.
Ule mchezo ukaninogea,nikinyimwa msosi mi kwenda kufunua vindoo ya kachori na maandazi ya watu. Basi kuna siku nikanyimwa msosi tena na yule mother wa kambo nikapita katika machimbo yote ya maandazi na kachori nikakosa,nikarudi zangu home kinyonge sana, ni mida ya kama saa 1 kasoro night hiyo.
Kufika home nikakuta kuna mia mbili zile za noti( wahenga tunaenda sawa hapa) nikatembea na ile pesa wakuu,nikazama shop nikanunua zangu mazaga nikala.
Niliporudi home kilipigo nilichokutana nacho ni cha jibwa koko mpaka nikazima,yule mother akadhani kaua basi akataka aue soo kwa kunitupa katika kisima. Daah wakuu! hii dunia kuna watu wana roho mbaya kinomaaa,yani bila msaada wa majirani waliosikia kile kilio wakati napigwa bila shaka nisingekua naandika comment hii leo. (Nitakuja siku moja na thread kuelezea juu ya kunusurika kwangu kutupwa kisimani).
Kwa wakazi wa Dodoma waliokuepo kipindi kile bila shaka huu ukatili nilifanyiwa wa kutaka kutupwa kisimani ni lazma mliusikia,kwasababu iligeuka ni habari ya mji.

Baada ya lile tukio kuna ndugu alinichuka nikaishi nae,huku msoto ndipo ulikolea. Mwanzo mambo yalikua poa,ila baadae mkewe akaanza kunifanyia vimbwenga,mumewe akiwa kazini msosi sipewi,na mwanae anakula nikimtizama,na hakuna kushitaki kwa mumewe,thubutuuuuu.
Nikaona isiwe kesi,nikaanza kuokota vyuma,uza sana screpa,nikipata pesa nanunua juice ya unga ile(tulikua unaiita juice kola) nakoroga na mandazi nakula weee! Kitumbo ndiii!!

Kufikia darasa la saba nikawa nina energy ya kwa kias fulani,basi nikitoka shule nachukua mkweche wangu (baiskeli zile mnaziita Anita,ila inakua haina kiti cha nyuma wala zile gards za matope,haina vipra vya kukanyaga,ina misongo tu) au waweza kuuita "mfupa".
Basi bwana,huu mfupa nikawa naenda nao kubeba miwa huko bush,naifunga katika mwamba then narudi town kuiuza. Kuna kipindi nikawa mtoro sana shule,saa 4 tu sipo, niko road na mfupa wangu kuelekea kwa mzee Mtivike kulangua miwa.

2008
Hapa nilianza form one,kule kwa ndugu yangu wakawa kama wamenitelekeza hivi,yani niwe muwazi tu ambacho nilikuwa napata pale ilibaki kuwa ni mahala pa kulala tu pamoja na umri wangu mdogo.
Bahati mbaya katika kupangiwa shule nilipangiwa shule ya kata iliyo nje kiasi na mji,ilikua mpya hii.

Time ya kureport imefika mi niko niko tu mtaani kama chokoraa, nikijicheki sina pa kuanzia daah wakuu!! I remember nilizaka dox magari mabovu,watu wa Iringa wanapajua hapa nikadaka shati langu la langi nyeupe iliyokataa (dona), nikalifua fresh kesho nikatinga school na chini nina suruali ya home, tena kwa kuchelewa.
Nilifika pake kila teacher ana nishangaa tu kwasababu nilikua niko niko tu. Confidence ndio kitu nimejaaliwa,directly nikatamka kuwa nataka kuonana na mkuu wa shule, staff nzima wakaangua vicheko! Ila baadae nikaelekezwa ni wapi niende.
Nilipofika nikamdanganya kuwa mimi yatima na uongo mwingine mwingi tu mixer na ukweli kiasi ndani yake.
Kwa jinsi nilivyokua najieleza alitokea kunionea huruma sana,kwa kufupisha ni kwamba huyu mzee baadae alikua kama mfadhili wangu wa kimasomo.

Wakuu ng'ombe wa masikini hazai,akizaa anazaa dume tena asie zaa pia.
Basi bwana,yule mzee (headmaster) ambae alianza kunisaidia hakuchukua muda mrefu sana akafariki,ingawa hata kiafya hakua imara sana ila nilihisi ni pigo kwangu.
Kufikia form two hali ya kimaishanikaona inazid kuwa mbaya kwangu,na kipindi hicho nilikua nishaondoka pale home nikawa naishi ghetto na brother anafanya kazi ya kupakia mchanga,mawe,kokoto na tofali katika maroli (huyu brother nilikutana nae kipindi nauza miwa,nae alikua anauza miwa kama mimi kwa kipindi hicho).
Mimi wakati huo niko bize nauza pipi na bubble gum (tulikua tunaziita big jii/bablishi) kuanzia mtaani mpaka darasani.
Getto tulikua tunalipa 3000,ni chumba cha giza,hakuna maji wala choo,chini vumbi ila kitanda kilikuepo japo kidogo dogo. Kwa kifupi ilikua ni nyumba ambayo haijakamilika ujenzi, mitaa ya Kihodombi kanisani kwa chini katika yale maporomoko.

Baadae nikaamua na mimi kujiungana yule brother katika shughuli za kupakia mchanga,kokoto,tofali na mawe. Kituo chetu cha kazi ilikua ni hapo samora njia ya veta yalipokua yanapark maroli. Kijana mdogo nikapakia sana jiwe,pakia sana mchanga,kokoto na tofali...baadae nikawa mtoro shule,naenda mara mbili tu per week nabaki kitaa nikipiga hard works.
Nishachimba sana mchanga na kuchimba mawe huko Isakalilo,mapogoro mpaja kitasengwa(watu wa Iringa nadhani mnayajua haya maeneo).
Nishanusurika vifo na ulemavu mara kibao katika ajari za haya maroli , kuna muda mko mlimani huko porini roli lina kutana na kigongo cha maana then lina kua kama limezima ghafla! Kifuatacho hapo ni kuanza kuporomoka kinyume nyume! Hapo kila mtu anafanya jitihada za kuruka ili kuokoa maisha yake.
Mfano ni ajari fulani ilitutokea wakati tunapanda mlima wa kutokea chini huko wanapaita Zizi la Ng'ombe,dereva gari likamshinda katika corner akaingia bondeni gari miguu juu tukafunikwa humo,THANKS GOD nilitoka salama ingawa nilishudia kifo cha jamaa wa mkaa nae alipewa kama lift tu.

Mpaka namaliza kidato cha nne ni mambo mengi sana nilikua nishayafanya,ila siwezi kuyaweka hapa ili kufupisha story.

Nitaendelea...




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilihitimu kidato cha nne japo kwa tabu sanaaa! Yani kwa mbinde kweli kweli!!
Wakati nasubiri matokeo...
Nikaendelea na mishe zangu ngumu,kwa wakati huu niliamua kufyatua tofari za udongo,nikatengeneza tanuru nikalichoma ingawa upatikanaji wa kuni za kuchomea tanuru ulikua ni unjanja ujanja tu.

Msimu wa mvua nikaanza mishe za kusajili line jama wakala wa tigo (Freelancer),nikasajili sana wakuu,sisi tulikua tunaita kupiga connections. Ni kile kipindi kuna ile promo ya joti(toa buku urudishiwe buku). Nikamaliza karibu kusini yote nikiwa nasajili tu,nilipiga hela sana kipindi hiki ukizingatia kusini Tigo ndio walikua kama wanaanza kubamba. Confidence nilikua nayo,then sikuwa naona aibu kwa mtu yeyote yule, na sijawahi kuona aibu likija suala la kazi,hata iweje hiyo kazi huwa sioni aibu, jambo la msingi kazi iwe legalized.
Kipindi hiki hela nilizikamata wakuu, mpaka nikaanza kuwekeza katika ventures ndogo ndogo,mfano saloon,goal la chips,mitumba,n.k.

Kuna kipindi nikawa nakula tender za kubandika mabango town,yani unazunguka mji mzima kama mwehu huku ukibandika mabango. Kuna time wewe uko bize unabandika huko nyuma kuna binadamu vichwa maji wanayachana.

Kwa kufupisha story ni kuwa,nilifaulu japo kwa tabu sanaaaa! Yani chupu chupu nifeli,ila sikwenda kusoma kwa wakati huo nikawa bize na utafutaji wa pesa. Ila baadae niliendelea na shule (advanced level) nayo nilisoma kwa shida kiasi japo si sana kwasababu nilikua na vijipesa vya madafu.

Nitakuja kumalizizia msoto mkali niliokutana nao na ninaozidi kukumbana nao baada ya kuhitimu chuo.

Itaendelea...



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Basi wakuu,nilipoenda chuo nikaendeleza harakati zangu,nilikua nauza nguo,kofia,sabuni hasa hasa manjano akina dada wanazipenda sana hizi,liwa,n.k. Nikawa dalali wa simu na assets mbalimbali. Yani nilikua bize haswaa muda wote kichwa yangu inawaza pesa tu,japo mkopo sikukosa japo kwa asilimia kadhaa,hapo mixer niliambatanisha vyeti vya vifo vya kutosha,yani full viambata.
First year mapema semester ya pili nikajichanga vijisent vyangu vya mtaa na nyingine nyingine nikachukua boxer mpyaaaa!!! then nikamuachia mwanangu Yuzzo kitaa apigie kazi.
Mikosi ikaanza upyaa...
Third year final semester nikaibiwa hiyo pikipiki,wahuni walikata rock wakatembea nayo,(kilikua ni kitendo cha kuingia ndani na kuchukua koti,kutoka nje wameacha alama tu za matairi chini. Daah niliumia sana but nikapiga moyo konde. Hapo katikati sijasimulia jinsi miradi ya saloon,chips na mitumba ilivyokufa kisa wana,sitaki story iwe ndefu.

Msoto mkali baada ya Chuo.
Basi wakuu,nikamaliza chuo then nikarud kitaa kupambana,hapo sina A wala B,kila kitu kimepukutika,nina akiba tu kiasi. Nikajaribu kucheki upepo street nikaona pagumu, nikapata wazo la kwenda kuuza moja kati kiwanja changu nje kidogo ya mji(hivi nilinunua bei ya mbuzi kipindi cha ufreelancer wangu,sehemu fulani panaitwa Kitasengwa).
Sikua na namna nikauza then nikamchek mwanangu fulan yuko Mbeya tukazama bush kwako kuchek mali nije nayo town (kosa kubwa kutokusoma alama za nyakati) daah mvua ikaharibu kila kituuu!! Tukakwama bush kama week mbili nikajikuta nazidi kuishiwa tu na hakuna tumaini la kuokoa mzigo.
Niko bush nahangaika napata taarifa huku getto wameiba kila kitu!
Daah wakuu! Nilitamani hata nitoweke tu duniani,nikajiona si kitu mbele ya uso wa dunia! Nikawaza mengi sana! Why Mungu ananiacha nitaabike hivi?
Nilidhoofu sanaaa,sikua hata na hamu ya kutafuta pesa tena! Nikajiona ni mtu nisiepiga hatua katika maisha. Yani bush nmekula loss na huku town wameniliza kila kitu daah wakuu!!

Kwa kifupi nilichoka nikachakaa,hali ikazidi kuwa mbaya nikaona bora nirudi kwa jamaa wa TIGO,jamaa wakanipa mashine zile za kusajilia line kwa alama za vidole "FAMOCO" kidume nikaingia kitaa daah!
Nikaona hapa hakuna namna wacha nipige kazi,issue nzuri ni kuwa mtu akiniona alikua anadhani either nimetoka makao makuu au niko kitengo tofauti na kile cha kusajili,hapa nazungumzia usmart,convincing,e.t.c. So nilipiga noti kwa kiasi fulani mpaka December 31 nilikua nishapata kianzio nikaachana na ile kazi, ijapokuwa kwasasa bado sijakaa sawa kabisa ila angalau ninacho kianzio.

Hayo ni baadhi tu ya niliyopitia wakuu,jambo la msingi katika maisha ni kutokukata tamaa,haijalishi ni magumu kiasi gani unapitia. Ukianguka usilale hapo hapo,inuka songa mbele kwa umakini zaidi.
Maisha ni kama mshale,ili uende mbali zaidi ni lazima uvutwe sana nyuma,so GOD PULLS US BACK TO SHOOT US FORWARD.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…