Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

Hongera jamaa...keep hiyo discipline na hard working utafika mbali sana
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati nimemaliza chuo sina ramani nikakutana na mwana kitaa,tukapanga dili ya kununua kuku vijijini na kuuza mjini' tukasema tufanye simple research kabla ya kuingia vijiji vya ndanindani kwahiyo tukaona tutembelee vijiji vya karibu' tukajikoki asubuh moja hivi na baiskeli zetu za kukodi huku tumefunga matenga yetu nyuma ya baiskeli mpaka vijijini huku tunapita nyumba kwa nyumba kuulizia kuku, hapo tupo na bajeti kama ya 120' tukanza kununua kwa buku 7 Mpaka 8 kwa matembe na majogoo kwa buku 12 tulizunguka kuanzia alfajir mpaka usiku tukapata kuku kama 12 hivi'.Kwa bei amboyo tulikua nayo kichwani ni kwamba wale kuku wa buku 7 na 8 tunauza kwa buku 11 mbaka 12 na majogoo kuanzia 16 mpaka 18, dadeki ikafika asubuh hao na matenga yetu tunapita chocho kitaa wasituone si unajua noma wasomi tena na tenga la kuku inakua jau' ile tunatua tu sokoni kuku wa kutoka vijiji kama wote wametua sokoni' kumbe wanunuzi huwa hawanunui kuku mmoja mmoja walioko kwenye matenga ' huwa wanawahesabu then wanakulipa kwa ujumla wao , daa nakumbuka walikuja wateja kama watano hivi wote wanaishia bei ya elfu 80 kudadeki , kwahiyo tukawa tunaishia kuangaliana tu na mwana na kuwasepesha, kumbe time inazidi kwenda ikafika kama saa tatu asubh hivi tukaanza kujiona kama tupo sisi tu na kuku zetu, hapo mzee baba tumetoil kinoma tukipiga hesabu baiskeli tumekodi buku jero kutwa afu zipo mbili, msosi, Muda, bei ya kuku ,full kuchoka lakini kwakua ilikua ni kama sehemu ya kujifunza tukapiga moyo konde..huku na huku akatokea mwana mmoja ndio akatugea maufundi na lecture lakutosha kuhusu hiyo biashara' akatuambia tuzunguke kwenye baa na mama ntilie tutapiga pesa maana huwa wananunia kwa jumla' basi tukajikoki tukaanza kuzungusha mzigo' daa dakika kama 20 tukamaliza kuuza tukapata kama 140k hivi ila kimsingi ilikua hasara' tukarudi kwa jamaa akazidi kutupa maufundi namna ile biashara ilivyo nae kumbe ndio ulikua mchongo wake kutoa kuku vijijini kuleta town ' tukaona mambo si ndio hayo bhana full kumwamini jamaa tukaungana naye " tukatupia mtaji wetu kama 800k hivi hao vijiji vya mbali na wilayani tukakusanya wakutosha kuleta town, huku mchakato wote akiwa anausimamia yeye, tukagonga faida kimtindo tukafanya kama miezi 3 hivi jamaa akalala mbele kusikojulikana na mpunga wote mshenzi yule, na hapo ndio ikawa mwisho wa biashara

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Igoma pamoja sana mkuu, anga hizi.
 
Baada ya kumaliza chuo niliyofautiana na mzee. Nikasepa zangu na kuanzisha biashara ya juisi k.koo.

Niliuza juisi kwa mkokoteni. Yani natengeneza kwenye ndoo alafu napaki sehemu nauza. Nilikuwa nanunua bites kwa jamaa mmoja hivyo nauza na juisi. Faida haikuwa kubwa sana lkn changamoto zikawa nyingi sana.

Kuna siku niligonga garibya jamaa mmoja na mkokoteni wangu maglasi yote chini paaaaa. Kama unavyojua wamachinga wa k.koo kila mtu kelele wengine wakishangilia.

Kijana nimejawa hofu na woga, jamaa mwenye gari alinizingua sana ukicheki Gari nimepasua taa ya nyuma na bampa.

Watu waliniombea pale lkn wapi. Akanisachi na kuchukua pesa zote na mkokoteni akabeba.

Mambo ya biashara yakafia pale. Nikarudi zangu gheto na kuwaza nianze fanya nini. Baada ya wiki ya msoto ndipo nikafanya maamuzi ya kwenda kuomba kazi kwa mjomba wangu ambae anamiliki maukumbi makubwa ya harusi.

Sikutegemea kama angenipokea vizuri vile, palepale nikapelekwa kwenye moja ya ukumbi wake na kutangazwa meneja.

Nyota ndio ilianza kung'aa kuanzia hapo. Mambo si mabaya sasa, watu waliokuwa wananijua nauza juisi walikuwa hawajui kama nimesoma. Leo wakinikuta wananiambia nilikuwa USALAMAA wala sio muuza juisi [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Watu tumesota sana, ndio maana sipendi kuishi maisha ya kishenzi, kula sana bata.
Maamaaeee!!
 
Dah pole sana bwana mze, usiwaze utatoboa tena..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aiseeeeeee....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kwanini usimtafute Ontario akupe mbili tatu za kutoboa...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ngoja Siku mjomba akukatae..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
👊👊👊
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…