Wakati Urusi bado wanahangaika na HIMARS, sasa USA kutuma 'VAMPIRE' Ukraine

Fahamu hili
 
Huelewei unachosema
 
Congress wamempa Biden dola bilioni 40 za kuanzia atumuie kwa ajili ya Ukraine, bajeti ya mwaka ya ulinzi tu ya US ni dola bilioni 750.
Vita vya Iraq US ilikuwa inatumia dola milion 300 kwa siku kwa miaka 20.
Hawafilisiki leo wala kesho hao.
Sio kwa Urusi! Hapo Marekani atatoa mikopo mingi kwa Ukraine ila akija kushtuka Ukraine yenyewe haitokuwepo tena.
Yani kwa kifupi Marekani atakula hasara kubwa itakayopelekea anguko lake
 
Mfano wa hao watu wanaoitwa "finance capital" ni kina nani?
Wataje watatu tu.
 
Kumbe Hypersonic na thermobaric bombs ni silaha za vita vya pili vya dunia![emoji1787]

Kitu Mrusi hajatumia Ukraine ni mabomu ya nyuklia tu wewe kilaza.
 
Bullshit na mawazo ya kijima ya kumhesimu mkubwa tu.

Mbona Finland imepeleka maombi ya kujiunga na NATO na huyo mkubwa hajamvamia mpaka sasa hivi?
Wewe ni team America. Tutaishia tu kubishana na kamwe hatutaelewana.
 
Uongo mtupu,

1.Zelenskyy haiwezi kuiingiza Ukraine NATO, Bunge la Ukraine ndilo lenye mamlaka hayo.

2.Ukraine pia haiwezi kuingia tu NATO bila nchi wanachama wote wa NATO kuridhia kupitia mabunge ya nchi zao.

3.Mbona Finland imepeleka maombi ya kujiunga NATO na mchakato wa kuifanya mwanachama umeanza ila Putin hajaivamia mpaka sasa??
 
... uko tayari ku-surrender uhuru wa familia yako simply jirani yako hataki ufanye kitu fulani chenye manufaa kwa family yako?
Kwani kungetokea nini iwapo hiyo Ukraine ingebakia kuwa neutral State kama alivyotaka Urusi?

Na hasa umichukulia uhasama wa muda mrefu uliopo kati ya Urusi na Marekani, na baadhi ya nchi za Ulaya Magharibi! Na hasa Uingereza?
 


Well said binafsi nawashangaa JF Members wanao support Ma-Gringo hawa wauuaji, wakatiri, wafitini,roho za kutu walio kubuhu kwenye vices zote ovu hapa Duniani!!

Wao ndio walio changia sana kwenye vita hii inayo endelea nchini Ukraine walimvimbisha kichwa Zelensky ili apuuzie makubaliano ya Minsk vile vile NATO specifically USA ikapuuzia/dharau concerns za Urusi kuhusu kuwakikishiwa usalama wa Taifa lake baada ya kuona NATO alliance inajisogeza sogeza na kuizingira mipaka yote ya Urusi, kufanya mazoezi mara kadhaa kwa mwaka wakiwa mipakani mwa Urusi kwa lengo la kujaribu kuwa tisha tisha Warusi, yaani ujeuri wa Merikani unaifanya kusahau kwamba Urusi ni a thermonuclear Super Power yenye uwezo mkubwa wa kuifuta kwenye uso wa Dunia Taifa lote la Merikani in no time - Urusi iliwaonya Wamerikani kidiplomasia mara nyingi tu lakini Merikani ikampuuzia tu kutokana na ujeuri na dharau za kitoto,walifikiri Urusi haiwezi kufanya lolote kukomesha ujinga/uchokozi wao, Wamerikani walivyo watu wa ajabu Urusi ikipeleka silaha kwenye mipaka ya Mexico na Merikani, Cuba,Venezuela, Nicaragua na Canada na kuanzisha mazoezi ya kijeshi ikishirikiana na mataifa tajwa hapo juu, nawa hakikisheni siku hiyo Merikani itaitisha kikao cha dhalula cha Umoja wa mataifa kuishutumu Urusi kwa hatarisha amani Duninani lakini wao kuwafanyia ujinga kama huo huo Warusi wao wanaona hilo balabala.

Vita ya Ukraine ndio Merikani imeona imepata golden opportunity ya kutekeleza njama/malengo yake ya miaka mingi dhidi ya Urusi kwa kulitumia taifa kubwa kieneo Barani Ulaya lenye wanajeshi wengi pamoja na silaha nyingi ndio maana Amerika imeshupalia Taifa la Ukraine lipigane a proxy war kwa niaba ya Merikani walishirikiana na wamiliki wa viwanda vinavyo unda silaha(MIC) - wamiliki wa viwanda hivyo huko Merikani ni kama Serikali ndani ya Serikali hao ndio wanamwendesha puta Biden afanye wapendalo si wao wala Biden wenye uchungu wa kweli kuhusu Ukraine na raia wake, wanacho fanya ni maigizo tu akili zao zote zipo kwenye uuzaji wa silaha kwa wingi na kutaka kusambaratisha taifa la Urusi wako, overly obsessed na Urusi, lakini wanagwaya kupigana na Warusi moja kwa moja ndio maana wanawatumia watu/mataifa mengine kabisa kutekeleza malengo yao ya siri.

Watu wangapi wanajua kwamba mwanae Biden alikuwa mshauri mkubwa wa Serikali ya Ukraine wakati baba yake akiwa makamu wa Rais Obama, akamilikishwa kampuni ya Ukraine inayo deal na biashara ya mafuta na gesi - huu ni ushahidi tosha wa kudhilisha kwamba familia ya Biden wana vast vested interest kwenye taifa la Ukraine - hivyo Rais Biden atalazimika kufanya lolote ili kuhalikisha maslahi ya familia nchini Ukraine yanalindwa these are some of reasons why Biden ana chuki binafsi kwa Putin,swali ni: wangapi wanajua ukweli huo.
 
Kwani kungetokea nini iwapo hiyo Ukraine ingebakia kuwa neutral State kama alivyotaka Urusi?

Na hasa umichukulia uhasama wa muda mrefu uliopo kati ya Urusi na Marekani, na baadhi ya nchi za Ulaya Magharibi! Na hasa Uingereza?
... "kama alivyotaka Urusi"! Kama thinking zenyewe ndio hizo ni hatari sana! Kuna mktaba wowote baina ya Ukraine na Urusi ambao Ukraine ameuvunja? Au ni kwa kuwa Putin hataki tu? In short, Russia hana justification yoyote ya kuivamia Ukraine.
 
... "kama alivyotaka Urusi"! Kama thinking zenyewe ndio hizo ni hatari sana! Kuna mktaba wowote baina ya Ukraine na Urusi ambao Ukraine ameuvunja? Au ni kwa kuwa Putin hataki tu? In short, Russia hana justification yoyote ya kuivamia Ukraine.
Justification zipo kiusalama zaidi kilaza huwezi elewa. Ni sawa tu na ndugu yako akitaka kukuingiza matatizoni ukaamua kumchukulia hatua wengi watakuona huna maana ila kumbe unalinda usalama wako.
 

Hata Putin naye anatumika pasipo yeye kujua, waukraine na warusi wanakufa kwa faida ya Marekani.
 
Justification zipo kiusalama zaidi kilaza huwezi elewa. Ni sawa tu na ndugu yako akitaka kukuingiza matatizoni ukaamua kumchukulia hatua wengi watakuona huna maana ila kumbe unalinda usalama wako.
... nakuheshimu sana humu jamvini bro; tumia lugha ya staha. Kwa hiyo tangu Russia kuivamia na kuimiliki Crimea back 2014 ilikuwa ni kulinda usalama wake (Russia) au alikuwa na mengine?
 
Ukraine haijwahi kuacha kuwa neutral state.

Kwa nini Putin anataka Ukraine tu ndio iwe neutral state ila sio nyingine kama Finland, Estonia, Latvia au Japan anazopakana nazo?
Kwani kungetokea nini iwapo hiyo Ukraine ingebakia kuwa neutral State kama alivyotaka Urusi?

Na hasa umichukulia uhasama wa muda mrefu uliopo kati ya Urusi na Marekani, na baadhi ya nchi za Ulaya Magharibi! Na hasa Uingereza?
 
Wazungu nao wameonesha utahiira wao kwenye hili. Wameshindea kuwa na misimamo yao binafsi. Hawana tofauti na huku Africa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…