Wakati Watanzania wakibishana juu ya Bandari ya Bagamoyo, Kenya wafungua Bandari ya Lamu

Wallah tutajutia sana ujinga wa kupingapinga tu. Jamaa alitudanganya watu wakaingia kingi. Ukweli inakuja ngoja yatasemwa zaidi kwenye magazeti rasmi ili tuondokane na ujinga uliowekwa hapa miaka ya karibuni.

Berth 33 sio mchezo tena za kisasa sio hizi tunahangaika nazo sijui berth 10 Ila mpaka leo hatuna Cha maana na hazijaisha.

Deal done we are out of the league.
Tanzania tumejaa masihara sana mdau berth 12 ni upuuzi mtupu kwa dunia ya leo tena ukizingatia tunahudumia nchi nyingi za pembeni yetu.....
 
Wakati Watanzania wakiendelea kubishana juu ya Bandari ya Bagamoyo wao wakiita ni Wizi wakati eneo litakalojengwa Bandari ya Bagamoyo ni pori na hata wapewe miaka 1000 hawataweza kuliendesha kwa faida, na wakiwa wanalalamika kila siku kukosa ajira na kutokuwepo na maendeleo ya kweli, Leo hii watu walio serious na maendeleo na uchumi , Kenya wamefungua rasmi Bandari ya Lamu ambayo inasemwa ndo Bandari kubwa zaidi kusini mwa jangwa la sahara.

Leo Rais Kenyatta amezindua Bandari hii inayosemwa itakuwa na Berth 33 huku kati ya hizo Berth 29 zikiwa zinahudumiwa na sekta binafsi.

Kenya anasemwa anaenda kukamata soko lote na uganda, South Sudan na Ethiopia kutokana na kuanza kwa Bandari hii.

Hongereni watanzania Kwa kupenda umasikini, kupenda kwenu umasikini kunaenda kuifanya kenya kukua zaidi kuichumi na kuwapita mbali sana kwa miaka Mingi isiyohesabika ijayo.

View attachment 1793056

Tanzania tayari tuna bandari sijui mapepe ya bandari nyingine ni ya nini wakati mizigo inatosha pale Dar pakipanuliwa vizuri. Lakini ni ujinga kujenga bandari nyingine kwa mikopo na kuwapa wageni waendeshe kwa faida zao. China anafikiria kufanya sehemu ile iwe kambi ya jeshi na dampo la vitu vya China. Yaani sisi tutoe miaka 100 na mizigo yote ihamie bagamoyo ina maana tutakuwa tumeuwa bandari ya Dar!. Hiyo bandari ikijengwa haitakuwa yetu kwa mikataba ya sasa itakuwa balozi ya china pale hata bendera itakuwa ya china. Je Kenya wametoa kwa miaka 100! ni ujinga mtupu
 
Acha kujichoresha kuwa huna exposure! Hizo Bandari za Mtwara, Tanga na Dar zinaleta nini?? Zimeleta ufanisi na competition gani???

Hivi Unajua berth katika Bandari zote za Tanga, Dar na Mtwara hazijazizidi kwa idadi berth za Bandari moja tu ya Mombasa ambao wana berth zaidi ya 18???

Sasa kenya kaongeza Bandari nyingine yenye berth 33 na hapo berth 29 amezipa sekta binafsi ili kuweka ufanisi. Sasa utamzidi nini kenya zaidi ya yeye kuzidi kukupiga gap???
Haujamuelewa.... Tufundishe ni namna gani iyo bandari italeta faida wakati kuna bandari kibao na hatujawah kuona zikileta faida....

Then kwa nini ijengwe ingine kuliko kutanuliwa zilizopo?

Then kuna sababu hipi kuwa ni bagamoyo tu.... Kitaalamu au kibiashara??

Wajinga tupo weengi ukitaka tukueleww ni lazima kutuelekeza na sio kutulaumu tukipinga.

Berth ni kizungu tu kisikuchanganye..... Parking lot tu
 
Wakati Watanzania wakiendelea kubishana juu ya Bandari ya Bagamoyo wao wakiita ni Wizi wakati eneo litakalojengwa Bandari ya Bagamoyo ni pori na hata wapewe miaka 1000 hawataweza kuliendesha kwa faida, na wakiwa wanalalamika kila siku kukosa ajira na kutokuwepo na maendeleo ya kweli, Leo hii watu walio serious na maendeleo na uchumi , Kenya wamefungua rasmi Bandari ya Lamu ambayo inasemwa ndo Bandari kubwa zaidi kusini mwa jangwa la sahara.

Leo Rais Kenyatta amezindua Bandari hii inayosemwa itakuwa na Berth 33 huku kati ya hizo Berth 29 zikiwa zinahudumiwa na sekta binafsi.

Kenya anasemwa anaenda kukamata soko lote na uganda, South Sudan na Ethiopia kutokana na kuanza kwa Bandari hii.

Hongereni watanzania Kwa kupenda umasikini, kupenda kwenu umasikini kunaenda kuifanya kenya kukua zaidi kuichumi na kuwapita mbali sana kwa miaka Mingi isiyohesabika ijayo.

View attachment 1793056
Halafu kuna wajinga wanamuita Mbeba maono?? Kama Mwendazake alijuwa mbeba maono bassi alibeba maono ya vipofu. Na vipofu wenyewe Ni sisi Watanzania Milioni 60.

Kweli mtu aliyenakili (Plagiarist) andiko la PhD la mwenzie anaweza akawa na maono?

Magufuli alikuwa na akili za wastani tu, yaani karai au Grade "C", lakini alitaka tumtambue kama intellectual visionary leader.

No way, alikuwa ni BIG FAILURE
 
Lakn inasemekana bandari ya Bagamoyo isingekuwa na faida kwetu kama tungekubali ijengwe
Tujihadhari na China. China ya sasa sio ile ya wakina Mao -Tse - Tung na Choenlai. Hawa sasa ni mabepari wanaotaka kufanya Afrika koloni lao kwa mikopo ya miradi isiyolipa huku dhamana ikiwa kubwa sana. Djibouti na Zambia ni mifano ya nchi ambazo zimelizwa na hao Wachina. Kuwakataa Wachina ilikuwa ni kuona mbali! Hatukatai bandari bali tunakataa masharti ya mkataba!
 
Wakati Watanzania wakiendelea kubishana juu ya Bandari ya Bagamoyo wao wakiita ni Wizi wakati eneo litakalojengwa Bandari ya Bagamoyo ni pori na hata wapewe miaka 1000 hawataweza kuliendesha kwa faida, na wakiwa wanalalamika kila siku kukosa ajira na kutokuwepo na maendeleo ya kweli, Leo hii watu walio serious na maendeleo na uchumi , Kenya wamefungua rasmi Bandari ya Lamu ambayo inasemwa ndo Bandari kubwa zaidi kusini mwa jangwa la sahara.

Leo Rais Kenyatta amezindua Bandari hii inayosemwa itakuwa na Berth 33 huku kati ya hizo Berth 29 zikiwa zinahudumiwa na sekta binafsi.

Kenya anasemwa anaenda kukamata soko lote na uganda, South Sudan na Ethiopia kutokana na kuanza kwa Bandari hii.

Hongereni watanzania Kwa kupenda umasikini, kupenda kwenu umasikini kunaenda kuifanya kenya kukua zaidi kuichumi na kuwapita mbali sana kwa miaka Mingi isiyohesabika ijayo.

View attachment 1793056
Unataka wasifungue nyingine wakati Mombasa imechukuliwa na wachina?
Kwa hiyo na sisi tufungue nyingine? Pwani yetu ina bandari ngapi na Kenya inazo ngapi? Lengo ni kufungua tu, bila sababu? Foolish creature!
 
Acha kujichoresha kuwa huna exposure! Hizo Bandari za Mtwara, Tanga na Dar zinaleta nini?? Zimeleta ufanisi na competition gani???

Hivi Unajua berth katika Bandari zote za Tanga, Dar na Mtwara hazijazizidi kwa idadi berth za Bandari moja tu ya Mombasa ambao wana berth zaidi ya 18???

Sasa kenya kaongeza Bandari nyingine yenye berth 33 na hapo berth 29 amezipa sekta binafsi ili kuweka ufanisi. Sasa utamzidi nini kenya zaidi ya yeye kuzidi kukupiga gap???
Foolish! Unadhani ukiongeza ndo unapata ufanisi? Mizigo inatengenezwa na berth? Mtu nguchiro?
 
Kwa hiyo kwa sababu Kenya wamezindua bandari mpya basi ni kigezo cha sisi kujenga bandari ya Bagamoyo? Je bandari za Dar es salaam, Tanga na Mtwara tumeziwezeshaje ili ziweze kutoa huduma nzuri na kubeba mizigo mingi?
 
Chadema ndege walipinga, reli walipinga, bwawa la nyerere walipinga, lakini kutwa macho kodo kusifia maendeleo ya Kenya
Hapo kuna mengi Boss! Wanasifia Kenya ili kuonesha hasira yao tu ya kikabila. Ukiwauliza malengo ya Bandari ya Lamu ni yapi, wao wanahesabu mizigo utadhani kuna meli zinasubilia bandari mpya. Ukiwauliza kama wana mizigo imekosa bandari, watasema iko mingi tu!
 
Kwa hiyo kwa sababu Kenya wamezindua bandari mpya basi ni kigezo cha sisi kujenga bandari ya Bagamoyo? Je bandari za Dar es salaam, Tanga na Mtwara tumeziwezeshaje ili ziweze kutoa huduma nzuri na kubeba mizigo mingi?
Sgr ikikamilika bandari yetu ya dar itakuwa na uwezo wa kuilisha mzigo wa kutosha??
 
Mkataba kwanza ukajadiliwe bungeni na akina Msukuma.
Halafu wataalam watuambie wananchi.
 
Mada ina lengo la kuwapa uoga watanzania.

Upanuzi wa bandari zote tulizonazo na uendelee kama kawaida.

Pwani yetu ni kubwa kuliko ya jirani zetu wa kaskazini hivyo hatuhitaji kujiona tumechelewa, hizo fursa zipo tu.
 
Unazungumzia vibandari hivi mbuzi vilivyoachwa na mkoloni?

Hivi vibandari haviwezeshi mimeli mikubwa kutia nanga, ni vidogo sana na hiyo ya Dar kina chake ni kidogo sana kuwezesha mimeli hiyo kutia nanga
 
Hiyo ya bagamoyo ina mizengwe mingi kwa mujibu wa JPM inabidi tuwekwe sawa tusije kuuziwa mbuzi kwa mlio.

Afadhali hizi alizoacha mkoloni tunazozijua kwa undani.
 
Back
Top Bottom