Wakati Watanzania wakibishana juu ya Bandari ya Bagamoyo, Kenya wafungua Bandari ya Lamu

Wakati Watanzania wakibishana juu ya Bandari ya Bagamoyo, Kenya wafungua Bandari ya Lamu

Mada ina lengo la kuwapa uoga watanzania.

Upanuzi wa bandari zote tulizonazo na uendelee kama kawaida.

Pwani yetu ni kubwa kuliko ya jirani zetu wa kaskazini hivyo hatuhitaji kujiona tumechelewa, hizo fursa zipo tu.
Endeleeni kujisifu kwa sifa za kijinga, sijui tuna PWANI kubwa wakati wenzenu wanatumia kidogo walichonacho kwa akili inayowapa faida maradufu
 
Unapinga ndege,
Unapinga sgr
Unapinga bwawa la nyerere
Unapinga bara bara za juu ubungo na tazara

Ila unasifia na kupigania bandari ya bagamoyo.

Huu upumbavu mwingine ni wa kujitakia tu
Nani alipinga na alipingaje?
 
Sgr ikikamilika bandari yetu ya dar itakuwa na uwezo wa kuilisha mzigo wa kutosha??
SGR inayokwenda wapi??? Burundi na Rwanda???

Nyie mna akili kweli?? Badala ya kujenga SGR TAZARA inapokwenda mizigo mingi kwenye nchi tano zenye biashara za uhakika nyie mnajenga SGR kwenda Rwanda na Burundi!

Izo ni akili Au matope???
 
Kwa akili zako hizi lazima utajisifu sana kuwa wewe ni mnyonge
Tanzania tayari tuna bandari sijui mapepe ya bandari nyingine ni ya nini wakati mizigo inatosha pale Dar pakipanuliwa vizuri. Lakini ni ujinga kujenga bandari nyingine kwa mikopo na kuwapa wageni waendeshe kwa faida zao. China anafikiria kufanya sehemu ile iwe kambi ya jeshi na dampo la vitu vya China. Yaani sisi tutoe miaka 100 na mizigo yote ihamie bagamoyo ina maana tutakuwa tumeuwa bandari ya Dar!. Hiyo bandari ikijengwa haitakuwa yetu kwa mikataba ya sasa itakuwa balozi ya china pale hata bendera itakuwa ya china. Je Kenya wametoa kwa miaka 100! ni ujinga mtupu
 
Mombasa imechukuliwaje na wachina??? Wewe unaangalia idadi ya Bandari tulizonazo au ufanisi wa hizo Bandari???

kuna ufanisi gani kwenye hizo Bandari in terms of kuhudumia mteja compared na Bandari moja tu ya Mombasa???
Wenzenu wanaipa kipaumbele kikubwa sekta binafsi ili kuleta ufanisi nyie kila siku kuita sekta binafsi wezi sasa mtawazidi wapi??? Wenzenu kila siku wanakaribisha uwekezaji nyie kila siku kuu Ponda uwekezaji eti wanapewa miaka mingi wakati hata akili na uwezo wa kifedha wa kufanya uwekezaji wa namna iyo hamna!

k
Unataka wasifungue nyingine wakati Mombasa imechukuliwa na wachina?
Kwa hiyo na sisi tufungue nyingine? Pwani yetu ina bandari ngapi na Kenya inazo ngapi? Lengo ni kufungua tu, bila sababu? Foolish creature!
 
Tatizo hujaelewa! Kenya target yake ni kufanya Ethiopia na South Sudan watumie Bandari yake hata kama wana options za kutumia Bandari zingine.

Na kwa kusisitiza ilo Ndo mana kwenye Bandari ya Lamu ameweka Berth 29 ziendeshwe na sekta binafsi! Hujaona logic ya kenya hapo we chato gang???

Basi Ngoja nikusaidie, sababu ya kuweka berth 29 kuendeshwa na sekta binafsi ni kuwa kutakuwa na ufanisi mkubwa sana kwenye operations hivyo mteja lazima atafuata huduma bora, na Kama mteja siku zote anafuata huduma Bora basi ataenda kenya badala ya Eritrea, Djibouti na huko Sudan
 
Hii tu imekuondolea umakini kwenye mada yako.

Unazuzuka na nini hasa!

Hiyo bandari ya Lamu itakataza Bagamoyo tusijenge?

Hiyo hapo unayoishangilia ni "white elephant", in the true name of that phrase.

Lamu inakunyima nini wewe kama ni mtu wa Bagamoyo (mTanzania)?

Wao wanalenga Ethiopia, ambayo tayari inatumia bandari mbili, Eritrea na Djibouti, tena zenye mafanikio makubwa Sudan Kusini wanatumia bandari za Sudan!

Wewe ukisikia kelele nyingi akili inakuruka na kuanza kulialia kwa jambo lisilokuwa na athari yoyote kwa Bagamoyo?

Haya, una hisa huko, au wewe ni wakala wa walanguzi wanaotaka utuhimize tufanye mambo kwa papara kwa hasara ya nchi?

Bagamoyo itajengwa kwa utashi wetu, na sio kwa mihemuko ya watu kama wewe. Unakuja hapa kusema hatuwezi kujenga hata katika miaka 1000, wewe ni nani? Bure kabisa.
Tatizo hujaelewa! Kenya target yake ni kufanya Ethiopia na South Sudan watumie Bandari yake hata kama wana options za kutumia Bandari zingine.

Na kwa kusisitiza ilo Ndo mana kwenye Bandari ya Lamu ameweka Berth 29 ziendeshwe na sekta binafsi! Hujaona logic ya kenya hapo we chato gang???

Basi Ngoja nikusaidie, sababu ya kuweka berth 29 kuendeshwa na sekta binafsi ni kuwa kutakuwa na ufanisi mkubwa sana kwenye operations hivyo mteja lazima atafuata huduma bora, na Kama mteja siku zote anafuata huduma Bora basi ataenda kenya badala ya Eritrea, Djibouti na huko Sudan
 
Nchi yetu haingozwi na Kenya, kwamba Kenya akijamba na sisi tujambe, Kenya akianza uwizi na sisi tuibe.
 
..mimi nilidhani reli itatukomboa.

..lakini nimeanza kuwa na wasiwasi kandarasi wa kituruki.

..pia nimechanganyikiwa na kipande cha Dodoma-Tabora kilivyoachwa na badala yake wanajenga Mwanza to Isaka.
Unajenga SGR kuelekea vinchi Rwanda na Burundi alafu unaacha kuboresha TAZARA inayoenda kwenye nchi za uhakika kama Congo, Zambia, Malawi, Zimbabwe na sasa mpaka Botswana, sasa wewe una akili Au matope kichwani?
 
Nchi yetu haingozwi na Kenya, kwamba Kenya akijamba na sisi tujambe, Kenya akianza uwizi na sisi tuibe.
Hatuongozwi na Kenya Ila kwenye dunia hii ya ushindani ili kuwa na maendeleo ya kweli kwa watu wako ni lazima ujitahidi kuwa mbele ya mwenzako hasa kifikra na kimipango ili kukamata vizuri fursa za maendeleo. Na kwenye hili Kenya ametuzidi kwa kuendekeza kwetu wapuuzi ndo waamue mipango yetu ya kimaendeleo
 
F**my mleta hoja umefika hapo Lamu ukajiridhisha na ulichoandika au ndio MSOGA Work.

Hivi mnatuona watanzania woote ni wapumbavu kama nyinyi mnaowazia matumbo yenu na watoto wenu all time!

Ndio maana hamtaki kustaafu, mama bungeni, mtoto bungeni na Baba kashikilia Remote!
Tunawavutia subira......
FB_IMG_1621656049774.jpg
 
Tujihadhari na China. China ya sasa sio ile ya wakina Mao -Tse - Tung na Choenlai. Hawa sasa ni mabepari wanaotaka kufanya Afrika koloni lao kwa mikopo ya miradi isiyolipa huku dhamana ikiwa kubwa sana. Djibouti na Zambia ni mifano ya nchi ambazo zimelizwa na hao Wachina. Kuwakataa Wachina ilikuwa ni kuona mbali! Hatukatai bandari bali tunakataa masharti ya mkataba!
issue sio mikopo. issur inaongelewa hapa nn faida ya bandari ys bagamoyo? kwann ijengwe?
 
Hebu wawepo wataalam wa kupitia upya mkataba wa huo ujenz then walete conclusion. Hii mamb ya kufuata mawazo ya mtu ambae hayupo duniani na kumuamin ni vzr tuachane nayo.
Huyo mtu alikuwa Rais wetu hakuwa muuza samaki pale feri.

Alikuwa na washauri wa kila aina. Tuwe waangalifu wasije kuumia watanzania wa miaka 30 ijayo halafu sisi wa leo tukalaaniwa kama babu zetu kwa kukubali kuuza watumwa kwa malipo ya shanga.
 
Endeleeni kujisifu kwa sifa za kijinga, sijui tuna PWANI kubwa wakati wenzenu wanatumia kidogo walichonacho kwa akili inayowapa faida maradufu
Tunapozipanua bandari lengo ni kupata mzigo mkubwa. Acheni mawazo ya kitumwa.

Miaka yore tangu uhuru hatukuona huo umuhimu wa kuwa na bandari zenye kupokea mzigo mwingi ndio leo tumekuja kuufahamu!!??.

Muwe waangalifu msije kuwa mnafanya udalali utakaokuja kuwaumiza watanzania wa miaka mingi ijayo.
 
Kama mnataka kuendesha Bandari wenyewe Kwa nini msifeli?? Wenzenu wanaendesha kwa kushirikiana na sekta binafsi ndo mana zina ufanisi. Nyie endeleeni kunywa kahawa na kupiga kelele tunaibiwa
Hata hiyo kushirikiana na sector binafsi ilishindikana, kumbuka Karamagi
 
Hatuongozwi na Kenya Ila kwenye dunia hii ya ushindani ili kuwa na maendeleo ya kweli kwa watu wako ni lazima ujitahidi kuwa mbele ya mwenzako hasa kifikra na kimipango ili kukamata vizuri fursa za maendeleo. Na kwenye hili Kenya ametuzidi kwa kuendekeza kwetu wapuuzi ndo waamue mipango yetu ya kimaendeleo
Hamia Kenya
 
Wakati Watanzania wakiendelea kubishana juu ya Bandari ya Bagamoyo wao wakiita ni Wizi wakati eneo litakalojengwa Bandari ya Bagamoyo ni pori na hata wapewe miaka 1000 hawataweza kuliendesha kwa faida, na wakiwa wanalalamika kila siku kukosa ajira na kutokuwepo na maendeleo ya kweli, Leo hii watu walio serious na maendeleo na uchumi , Kenya wamefungua rasmi Bandari ya Lamu ambayo inasemwa ndo Bandari kubwa zaidi kusini mwa jangwa la sahara.

Leo Rais Kenyatta amezindua Bandari hii inayosemwa itakuwa na Berth 33 huku kati ya hizo Berth 29 zikiwa zinahudumiwa na sekta binafsi.

Kenya anasemwa anaenda kukamata soko lote na uganda, South Sudan na Ethiopia kutokana na kuanza kwa Bandari hii.

Hongereni watanzania Kwa kupenda umasikini, kupenda kwenu umasikini kunaenda kuifanya kenya kukua zaidi kuichumi na kuwapita mbali sana kwa miaka Mingi isiyohesabika ijayo.

View attachment 1793056
Sisi tunazo za Mtwara , Tanga na bado ya Lindi kufunguliwa
 
Kuna mda Hadi nawazaga nchi hii mapandikizi ya nchi jirani yamejaa sana kuzuia nchi hii isiwe na miradi ya maendeleo mizuri ya kuleta maendeleo ya kweli.

Yaani unaamini uamuzi wa kukataa bandari ya Bagamoyo ulizuiliwa na huyu unayemuita pandikizi!! Sio JPM tena???

Kweli akili ya baadhi yetu ni ya kula, kulala na kuvaa tu!! Ndio ninyi mnaambiwa tuna maadui na kuamini na msihoji ni wapi hao!!!
 
Wakati Watanzania wakiendelea kubishana juu ya Bandari ya Bagamoyo wao wakiita ni Wizi wakati eneo litakalojengwa Bandari ya Bagamoyo ni pori na hata wapewe miaka 1000 hawataweza kuliendesha kwa faida, na wakiwa wanalalamika kila siku kukosa ajira na kutokuwepo na maendeleo ya kweli, Leo hii watu walio serious na maendeleo na uchumi , Kenya wamefungua rasmi Bandari ya Lamu ambayo inasemwa ndo Bandari kubwa zaidi kusini mwa jangwa la sahara.

Leo Rais Kenyatta amezindua Bandari hii inayosemwa itakuwa na Berth 33 huku kati ya hizo Berth 29 zikiwa zinahudumiwa na sekta binafsi.

Kenya anasemwa anaenda kukamata soko lote na uganda, South Sudan na Ethiopia kutokana na kuanza kwa Bandari hii.

Hongereni watanzania Kwa kupenda umasikini, kupenda kwenu umasikini kunaenda kuifanya kenya kukua zaidi kuichumi na kuwapita mbali sana kwa miaka Mingi isiyohesabika ijayo.

View attachment 1793056
Mkataba wa ujenzi wa hiyo Bandari ya lamu upoje kama wa Bagamoyo au ? Na je upanuzi wa Bandari ya Tanga na Mtwara hautaongeza uwezo wa Bandari zetu??? Na malango ya Bandari ya dam nasikia yanataka kuongezwa na hizo ghati sasa hivi zinaongezwa kina toka 9 m hadi 15m je hizi juhudi bado zitatuweka pabaya vs port za majirani zetu.
 
Back
Top Bottom