Wakati Watanzania wakibishana juu ya Bandari ya Bagamoyo, Kenya wafungua Bandari ya Lamu

Wakati Watanzania wakibishana juu ya Bandari ya Bagamoyo, Kenya wafungua Bandari ya Lamu

Hiyo tu ya Dar inatusumbua ooh mtandao uko chini, ooh nini sijui.
Hatutaki mzigo mwingine wa bandari uliotaka kumnufaisha bwana yulee.
mbona uchumi ulikuwa unakwenda kasi bila hii Bagamoyo yenu.
Hata hivyo haipo kwenye ilani ya CCM.
 
Hiyo ya bagamoyo ina mizengwe mingi kwa mujibu wa JPM inabidi tuwekwe sawa tusije kuuziwa mbuzi kwa mlio.

Afadhali hizi alizoacha mkoloni tunazozijua kwa undani.
JPM alikuwa na fiksi na kamba nyingi. Hakuwa mtu wa kuaminika yule.

Mwanzoni aliisifu project ya bagamoyo na akaahidi kuiendeleza, baadae akairuka kimanga
 
Kuna mda Hadi nawazaga nchi hii mapandikizi ya nchi jirani yamejaa sana kuzuia nchi hii isiwe na miradi ya maendeleo mizuri ya kuleta maendeleo ya kweli.
Unaongea kitu usichokijuaaa...kaa kimyaa mtoto mdogo sana wewe...wacha wakubwa tuongee
 
Wakati Watanzania wakiendelea kubishana juu ya Bandari ya Bagamoyo wao wakiita ni Wizi wakati eneo litakalojengwa Bandari ya Bagamoyo ni pori na hata wapewe miaka 1000 hawataweza kuliendesha kwa faida, na wakiwa wanalalamika kila siku kukosa ajira na kutokuwepo na maendeleo ya kweli, Leo hii watu walio serious na maendeleo na uchumi , Kenya wamefungua rasmi Bandari ya Lamu ambayo inasemwa ndo Bandari kubwa zaidi kusini mwa jangwa la sahara.

Leo Rais Kenyatta amezindua Bandari hii inayosemwa itakuwa na Berth 33 huku kati ya hizo Berth 29 zikiwa zinahudumiwa na sekta binafsi.

Kenya anasemwa anaenda kukamata soko lote na uganda, South Sudan na Ethiopia kutokana na kuanza kwa Bandari hii.

Hongereni watanzania Kwa kupenda umasikini, kupenda kwenu umasikini kunaenda kuifanya kenya kukua zaidi kuichumi na kuwapita mbali sana kwa miaka Mingi isiyohesabika ijayo.

View attachment 1793056
Mkuu hivi Lamu iko upande upi wa Kenya? Itatumika kwa mizigo ya Zambia, Malawi, Congo, Rwanda, na Burundi?
 
Hiyo ya bagamoyo ina mizengwe mingi kwa mujibu wa JPM inabidi tuwekwe sawa tusije kuuziwa mbuzi kwa mlio.

Afadhali hizi alizoacha mkoloni tunazozijua kwa undani.
Hebu wawepo wataalam wa kupitia upya mkataba wa huo ujenz then walete conclusion. Hii mamb ya kufuata mawazo ya mtu ambae hayupo duniani na kumuamin ni vzr tuachane nayo.
 
Wakati Watanzania wakiendelea kubishana juu ya Bandari ya Bagamoyo wao wakiita ni Wizi wakati eneo litakalojengwa Bandari ya Bagamoyo ni pori na hata wapewe miaka 1000 hawataweza kuliendesha kwa faida, na wakiwa wanalalamika kila siku kukosa ajira na kutokuwepo na maendeleo ya kweli, Leo hii watu walio serious na maendeleo na uchumi , Kenya wamefungua rasmi Bandari ya Lamu ambayo inasemwa ndo Bandari kubwa zaidi kusini mwa jangwa la sahara.
Hii tu imekuondolea umakini kwenye mada yako.

Unazuzuka na nini hasa!

Hiyo bandari ya Lamu itakataza Bagamoyo tusijenge?

Hiyo hapo unayoishangilia ni "white elephant", in the true name of that phrase.

Lamu inakunyima nini wewe kama ni mtu wa Bagamoyo (mTanzania)?

Wao wanalenga Ethiopia, ambayo tayari inatumia bandari mbili, Eritrea na Djibouti, tena zenye mafanikio makubwa Sudan Kusini wanatumia bandari za Sudan!

Wewe ukisikia kelele nyingi akili inakuruka na kuanza kulialia kwa jambo lisilokuwa na athari yoyote kwa Bagamoyo?

Haya, una hisa huko, au wewe ni wakala wa walanguzi wanaotaka utuhimize tufanye mambo kwa papara kwa hasara ya nchi?

Bagamoyo itajengwa kwa utashi wetu, na sio kwa mihemuko ya watu kama wewe. Unakuja hapa kusema hatuwezi kujenga hata katika miaka 1000, wewe ni nani? Bure kabisa.
 
Unapinga ndege,
Unapinga sgr
Unapinga bwawa la nyerere
Unapinga bara bara za juu ubungo na tazara

Ila unasifia na kupigania bandari ya bagamoyo.

Huu upumbavu mwingine ni wa kujitakia tu
Halaf hii kitu naitafuta sana mkuu, unaweza weka evidence ya hao jaman walivyokua wanapinga hayo uliyo mention? Ili angalau nione hoja yao ilikua ni nn.
 
uzur wa bandari ya bagamoyo itakua na faida zaidi kwa kua kutajengwa na industrial pack kuliko bidha zitoke china sitakua zinategenezwa hp nakusafirishwa nchi zingine za africa
tatizo kubwa ni hizo terms na condition za wachina wamejipendelea wao kama watapunguza mashart bora tujenge nchi itapata export kubwa na kuongeza GDP
 
Wallah tutajutia sana ujinga wa kupingapinga tu. Jamaa alitudanganya watu wakaingia kingi. Ukweli inakuja ngoja yatasemwa zaidi kwenye magazeti rasmi ili tuondokane na ujinga uliowekwa hapa miaka ya karibuni.

Berth 33 sio mchezo tena za kisasa sio hizi tunahangaika nazo sijui berth 10 Ila mpaka leo hatuna Cha maana na hazijaisha.

Deal done we are out of the league.
Hakuna lolote hapo, usipandishe mori bila sababu.

Huo mradi wa Lamu umekosa wawekezaji miaka na miaka, kwa kujua hauna manufaa yoyote, leo hii mtu anakuja hapa kulialia kwa kusikia makelele tu?

Kwani kuna ushahidi gani kwamba Bagamoyo haitajengwa?

Watu wanajiuza na kupiga makelele kupotezea wengine malengo, halafu tunaletewa hapa kelele hizo tuamini kwamba tumepigwa bao?

Bagamoyo itajengwa, na wala haiwezi kushindana na Lamu kwa njia yoyote ile!
 
pia huko lamu kupata wateja itakuwa ngumu kutpkana na tishio la magaidi Alshabab ndio maana hakutokea mwekezaji na mradi umejengwa karibia miaka kumi
 
Haha Nachocheka Watanzania wanasifu Kenya kwa bandari ila wakenya wanalia kwa utapeli wa hiyo bandari. Same na sgr lao la moshi na Vumbi.

Kinachekesha wakenya wanapongeza sgrya Tanzania nk

Wanadamu atupendi kujivunia vyetu ila vya jirani sasa😀

Zaman Hata flyover au interchange watanzania walikua wanananga watu ni aibu nchi haina hata daraja moja zaidi ya la manzese😀 Ila now walaa hawana time na fly over zinazolekea kuwa 10 Hapa Dar
 
Acha kujichoresha kuwa huna exposure! Hizo Bandari za Mtwara, Tanga na Dar zinaleta nini?? Zimeleta ufanisi na competition gani???

Hivi Unajua berth katika Bandari zote za Tanga, Dar na Mtwara hazijazizidi kwa idadi berth za Bandari moja tu ya Mombasa ambao wana berth zaidi ya 18???

Sasa kenya kaongeza Bandari nyingine yenye berth 33 na hapo berth 29 amezipa sekta binafsi ili kuweka ufanisi. Sasa utamzidi nini kenya zaidi ya yeye kuzidi kukupiga gap???

..mimi nilidhani reli itatukomboa.

..lakini nimeanza kuwa na wasiwasi kandarasi wa kituruki.

..pia nimechanganyikiwa na kipande cha Dodoma-Tabora kilivyoachwa na badala yake wanajenga Mwanza to Isaka.
 
Wallah tutajutia sana ujinga wa kupingapinga tu. Jamaa alitudanganya watu wakaingia kingi. Ukweli inakuja ngoja yatasemwa zaidi kwenye magazeti rasmi ili tuondokane na ujinga uliowekwa hapa miaka ya karibuni.

Berth 33 sio mchezo tena za kisasa sio hizi tunahangaika nazo sijui berth 10 Ila mpaka leo hatuna Cha maana na hazijaisha.

Deal done we are out of the league.

Sasa Kama mwendazake aliongoza nchi kwa mawazo ya watu miserable Kama akina Kinuju Kijogoodi jingalao et al unategemea nini?
 
Nani kakwambia al shabab wanasumbua kenya saivi?? Hujui kuwa situation ya alshabab imeshakuwa contained ndani ya Kenya???

Kwa taarifa yako Kenya anatarget kuwa msafirishaji Mkuu kwa mizigo ya Ethiopia, Sudan kusini, uganda na Congo kwa kupitia uganda. Nyie endelezeni tu tantalila na akili zenu za kijamaa na kimasikini izo huku wenzenu wakikamata uchumi wa East and Central Africa
pia huko lamu kupata wateja itakuwa ngumu kutpkana na tishio la magaidi Alshabab ndio maana hakutokea mwekezaji na mradi umejengwa karibia miaka kumi
 
Sasa Kama mwendazake aliongoza nchi kwa mawazo ya watu miserable Kama akina Kinuju Kijogoodi jingalao et al unategemea nini?
pia huko lamu kupata wateja itakuwa ngumu kutpkana na tishio la magaidi Alshabab ndio maana hakutokea mwekezaji na mradi umejengwa karibia miaka kumi
Mradi wa bandari ya Lamu feasibility study yake ilitegemea sana bomba la gesi kutoka Hoima, wakalikosa. Makamanda wnasema tumelala eti Kenya wanazindia bandari, kasahau Mu7 yuko mjini. Unatumpanishaje na bandari ya kwenda Ethiopia? Peoplezzzz wako tayari kula wembe kuisifu Kinya.
 
Kwa akili yao we biashara kubwa ya Bandari ni kusafirisha mafuta? Bandari za China ziko juu Kwa kusafirisha mafuta??? Embu acheni kupotosha Kwa kutokujua kwenu
Mradi wa bandari ya Lamu feasibility study yake ilitegemea sana bomba la gesi kutoka Hoima, wakalikosa. Makamanda wnasema tumelala eti Kenya wanazindia bandari, kasahau Mu7 yuko mjini. Unatumpanishaje na bandari ya kwenda Ethiopia? Peoplezzzz wako tayari kula wembe kuisifu Kinya.
 
Hizo tu tumeshindwa kuziendesha bado tunalilia mpya
Kama mnataka kuendesha Bandari wenyewe Kwa nini msifeli?? Wenzenu wanaendesha kwa kushirikiana na sekta binafsi ndo mana zina ufanisi. Nyie endeleeni kunywa kahawa na kupiga kelele tunaibiwa
 
Back
Top Bottom