Wakati Watanzania wakibishana juu ya Bandari ya Bagamoyo, Kenya wafungua Bandari ya Lamu

Wakati Watanzania wakibishana juu ya Bandari ya Bagamoyo, Kenya wafungua Bandari ya Lamu

Lakn inasemekana bandari ya Bagamoyo isingekuwa na faida kwetu kama tungekubali ijengwe
sasa ndege zinakua na faida alafu bandari haina kiaje? ata akijenga mwekezaj atarecoup pesa yake alafu atuachie bandari sooner or later. sijahesabu ajira na mabiashara tutayofanya
 
Tanganyika tuna bandari kubwa 3,
Dar es Salaam
Tanga na
Mtwara
Zanzibar yet haijawa fully utilized, Mhe. Hussein Mwinyo kaja na plan nzuri sana kujenga bandari mpya ya kisasa.

Dar inapanuliwa kwa sasa, kama Tanga ikipanuliwa kulifikia soko la kaskazini vema hali kadhalika Mtwara nayo ikipanuliwa na kuongezewa ufanisi nayo itafanya makubwa.

Bagamoyo port sioni kama kuna ubaya kujengwa maadam inakuwa sio ya mikataba ya "kimangungo".
Kile alichokifanya China kwa ujenzi wa bandari ya Sri Lanka na kwa jinsi imeshindwa kurejesha fedha kwa wakati na China kuichukua ndio msingi wa Tanzania kupigania fair deal.

Kumbuka mkataba wa awali wa China na Tz kujenga SGR ulikuwa worth USD 7.6 bn

Badae mwendazake akakujua kumbe Turkey anaweza kutoa fair deal kuliko Mchina; akapata deal ya USD 1.2 bn na baadae 1.9bn

Turkey wins bid to finance, build $1.9b second phase of Tanzania railway | The East African

Mchina kutujengea bandari ya Bagamoyo sio lazima awe yeye tu; hii ni biashara kama biashara zingine na sio lazima awe yeye tu.

Kuna jambo zuri mwendazeka katuachia, kushindanisha kupata fair deal. Angalia ujenzi wa JNHP kapewa Misri, SGR Turkey na Portuguese, then Isaka Mwanza ndio Mchina kaja akiwa na adabu kwa kujua sio lazima awe yeye tu.
 
Nani kakwambia al shabab wanasumbua kenya saivi?? Hujui kuwa situation ya alshabab imeshakuwa contained ndani ya Kenya???

Kwa taarifa yako Kenya anatarget kuwa msafirishaji Mkuu kwa mizigo ya Ethiopia, Sudan kusini, uganda na Congo kwa kupitia uganda. Nyie endelezeni tu tantalila na akili zenu za kijamaa na kimasikini izo huku wenzenu wakikamata uchumi wa East and Central Africa
Hata wiki iliyopita Alshabaab walishambulia Kenya Kaskazini kule Mandela kuteketeza basi na kuuwa abiria. Haijawa Contained. Ni ujinga kufikiri eti bandari ya Bagamoyo itasafirisha mizigo ya Ethiopia au Sudani Kusini!
 
Zama zimepita mkuu ni kama alivyoingia akaanza na yake na huyu aliepo achwe aanze yake mazuri ya kuendeleza ataendeleza.
Bandari ya bagamoyo mwaka huu kwenye bajeti haipo na ikitokea pakahitajika kuongezwa bandari nyingine mahali itakapojengwa pataamuliwa huko mbeleni.
 
Where is your smartness! Yaani huoni kenya anavyoweka Bandari zake vizuri huku akiziendesha kupitia sekta binafsi kutakuwa na ufanisi sana kwenye Bandari zake hadi kupelekea Bandari zetu kukimbiwa hivyo kukosa mapato???

Una akili kweli wewe mtu??

Unaongelea Kenya gani?
 
Bandari ya bagamoyo mwaka huu kwenye bajeti haipo na ikitokea pakahitajika kuongezwa bandari nyingine mahali itakapojengwa pataamuliwa huko mbeleni.
Tunawajua mapandiki mnaopigana kujenga propaganda ili Tanzania isipate maendeleo ya kweli. Hamtusumbui
 
Hata wiki iliyopita Alshabaab walishambulia Kenya Kaskazini kule Mandela kuteketeza basi na kuuwa abiria. Haijawa Contained. Ni ujinga kufikiri eti bandari ya Bagamoyo itasafirisha mizigo ya Ethiopia au Sudani Kusini!
Kwa nini ishindikane?
 
Sijaona utawala wenye nia njema na MTU yeyote. Wanasiasa wenyewe wanajua wanakotupeleka. Katiba yetu inamruhuru MTU yeyote kufanya anavyotaka, Liwe baya au jema, na bado utamaduni na mazizngira yetu yanatufanya tushangilie tunayotendewa. Utamaduni wetu unazaa umbumbumbu, tuko chini ya kifungo cha wanasiasa na viongozi wa dini wanafiki waliotanguliza masilahi yao mbele.
Uhai wetu ni kwa neema tu, maana mwanasiasa ndiye Mungu was dunia hii.
 
Wakati Watanzania wakiendelea kubishana juu ya Bandari ya Bagamoyo wao wakiita ni Wizi wakati eneo litakalojengwa Bandari ya Bagamoyo ni pori na hata wapewe miaka 1000 hawataweza kuliendesha kwa faida, na wakiwa wanalalamika kila siku kukosa ajira na kutokuwepo na maendeleo ya kweli, Leo hii watu walio serious na maendeleo na uchumi , Kenya wamefungua rasmi Bandari ya Lamu ambayo inasemwa ndo Bandari kubwa zaidi kusini mwa jangwa la sahara.

Leo Rais Kenyatta amezindua Bandari hii inayosemwa itakuwa na Berth 33 huku kati ya hizo Berth 29 zikiwa zinahudumiwa na sekta binafsi.

Kenya anasemwa anaenda kukamata soko lote na uganda, South Sudan na Ethiopia kutokana na kuanza kwa Bandari hii.

Hongereni watanzania Kwa kupenda umasikini, kupenda kwenu umasikini kunaenda kuifanya kenya kukua zaidi kuichumi na kuwapita mbali sana kwa miaka Mingi isiyohesabika ijayo.

Watz wamebaki wakiwa baada ya kifo cha magufuly. Lais magufuly aliwatetea san watz kwenye mambo kama haya yenye tija kwa taigha
 
Tuna bandari ya Tanga, Mtwara, Dar....wewe ulitakaje?
Labda dar huko kwingine hamna kitu labda kulipia mishahara tu, bandari ya bagamoyo ingejengwa hata wafanyabiashara wanaohangaika kwenye mitandao na kutapeliwa hela wangekuwa wanapata mizigo yao hapa hapa na hata mashine za kisasa kubwa tunazoshindwa kununua kwa kuogopa gharama za usafiri na njia za kusafirisha tungepata hapa hapa na mambo mengine mazuri.
 
Mibandari tunayo mingi,kama tulizo nazo zinatushinda,,unataka tujenge nyingine si litakua gofu?
Hizo zingine kuzifanya za kisasa ni ngumu maana gharama ni kubwa hivyo mpaka zije zilete faida na miundo mbinu ya kale haiwezekani.
 
Kwanza unaijua kenya ipi?

Shida yetu mitandaoni tunajua sana. Uzuri akili za kuambiwa lazima uchanganye na za kwako.
Endelea kuiogopa bandari ya Lamu ili Bandari ya Bagamoyo ijengwe....😂😂😂😂😂
Wana nzengo wanazoom tu
 
Acha kujichoresha kuwa huna exposure! Hizo Bandari za Mtwara, Tanga na Dar zinaleta nini?? Zimeleta ufanisi na competition gani???

Hivi Unajua berth katika Bandari zote za Tanga, Dar na Mtwara hazijazizidi kwa idadi berth za Bandari moja tu ya Mombasa ambao wana berth zaidi ya 18???

Sasa kenya kaongeza Bandari nyingine yenye berth 33 na hapo berth 29 amezipa sekta binafsi ili kuweka ufanisi. Sasa utamzidi nini kenya zaidi ya yeye kuzidi kukupiga gap???
Na kama ameweka sekita binafsi yeye anachukua kodi, na bado sekita binafsi zinajua kutafuta masoko na kusimamia wafanyakazi ambacho serikali haiwezi, sisi itabidi tuendelee kwenda kununua kwao hata cherehani za kushona maana tutapata huko kwa urahisi.
 
Chadema ndege walipinga, reli walipinga, bwawa la nyerere walipinga, lakini kutwa macho kodo kusifia maendeleo ya Kenya
Chadema haileti mkate kwenye familia zetu ila kazi zetu Kama hao chadema wanapinga Kama njia ya ajira kupeleka chakula kwenye familia zao hapo unayehangaika na hao chadema ndo utakuwa unajitafutia pressure kikubwa ni wewe kutambua lililojema kwa nchi yako na jinsi ya kustawisha familia yako Kama hao wanasiasa wanavyotumia muda kupinga Ili wastawishe familia zao.
 
Tumpongeze mwendazake kwa kusitisha mradi wa bandari ya Bagamoyo , kisa wivu ,roho mbaya , uncouth , unskilled , bipolar disorder unategemea nini?
 
Tunawajua mapandiki mnaopigana kujenga propaganda ili Tanzania isipate maendeleo ya kweli. Hamtusumbui
Hizo bandari zilizopo zinaendelea kupanuliwa na zote hazitakosa mizigo.

Hiyo ya bagamoyo kama umuhimu utatokea huko mbeleni itajengwa lakini ni kwa terms and conditions ambazo hazitatuumiza.
 
Wakati Watanzania wakiendelea kubishana juu ya Bandari ya Bagamoyo wao wakiita ni Wizi wakati eneo litakalojengwa Bandari ya Bagamoyo ni pori na hata wapewe miaka 1000 hawataweza kuliendesha kwa faida, na wakiwa wanalalamika kila siku kukosa ajira na kutokuwepo na maendeleo ya kweli, Leo hii watu walio serious na maendeleo na uchumi , Kenya wamefungua rasmi Bandari ya Lamu ambayo inasemwa ndo Bandari kubwa zaidi kusini mwa jangwa la sahara.

Leo Rais Kenyatta amezindua Bandari hii inayosemwa itakuwa na Berth 33 huku kati ya hizo Berth 29 zikiwa zinahudumiwa na sekta binafsi.

Kenya anasemwa anaenda kukamata soko lote na uganda, South Sudan na Ethiopia kutokana na kuanza kwa Bandari hii.

Hongereni watanzania Kwa kupenda umasikini, kupenda kwenu umasikini kunaenda kuifanya kenya kukua zaidi kuichumi na kuwapita mbali sana kwa miaka Mingi isiyohesabika ijayo.

Ugaidi umeisha Lamu? Tanzania tuna fursa nzuri ya kukamata soko lakini ndiyo hivyo tena. Hiyo bandari ya Bagamoyo ingejengwa Uganda ingehamia kwetu, maana tuna reli na meli pale Mwanza hivyo mizigo ingepita kirahisi sana!
 
Back
Top Bottom