Wakatoliki, imekuaje kipindi cha Kwaresma mmefungisha ndoa ya Mrema?

Wakatoliki, imekuaje kipindi cha Kwaresma mmefungisha ndoa ya Mrema?

Chukwu emeka

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2018
Posts
24,314
Reaction score
38,919
Habari wana Jukwaa,

Niende moja Kwa moja kwenye hoja, imekuaje sheria ya Kanisa imekiukwa Kwa kufunga ndoa wakati wa mfungo wa Kwaresma? Kwa kipindi hiki huwa hakuna harusi au sherehe yoyote Makanisani ikiwemo ndoa.

Imekuwa ni jambo la kawaida kwa nchi yetu, watu maarufu kupewa kipaumbele hata kama nikwakuvunja sheria zilizopo, yaani mtu akiwa na vijisenti au kiongozi mkubwa serikalini ni mara chache sana sheria kufuatwa.

Wakatoliki nisaidieni kunipa mwongozo hili la Mrema limekaaje?

Kila la heri mzee Mrema katika maisha yako ya ndoa takatifu.

FB_IMG_1648191730031.jpg
 
... ,imekuaje sheria ya Kanisa imekiukwa Kwa kufunga ndoa wakati wa mfungo wa Kwaresma? Kwa kipindi hiki huwa hakuna harusi au sherehe yoyote Makanisani ikiwemo ndoa.
Sio sheria, ni utaratibu ambao nao huwa haupo juu ya jambo la kiroho, ikiwa na maana kwamba utaratibu unaweza ukawekwa pembeni kwa jambo mahususi, na kinaweza kikatolewa kibali na Paroko au Askofu kulingana na mamlaka ya jambo husika. Kwa hiyo ndoa inaweza ikafungwa kutokana na sababu walizozieleza wahusika na jinsi lilivyopokelewa na kutafsiriwa na mamlaka.

Mfano mwingine ni kufunga ndoa au kufanya misa ya mazishi siku ya Jumapili, huwa hairuhusiwi kiutaratibu kwa baadhi ya majimbo, lakini kwa sababu maalum inaweza kuruhusiwa. Kwa hiyo just take it easy, kwa vyovyote vile watakuwa waliomba wakakubaliwa
 
Sio sheria, ni utaratibu ambao nao huwa haupo juu ya jambo la kiroho, ikiwa na maana kwamba utaratibu unaweza ukawekwa pembeni kwa jambo mahususi, na kinaweza kikatolewa kibali na Paroko au Askofu kulingana na mamlaka ya jambo husika. Kwa hiyo ndoa inaweza ikafungwa kutokana na sababu walizozieleza wahusika na jinsi lilivyopokelewa na kutafsiriwa na mamlaka. Mfano mwingine ni kufunga ndoa au kufanya misa ya mazishi siku ya Jumapili, huwa hairuhusiwi kiutaratibu kwa baadhi ya majimbo, lakini kwa sababu maalum inaweza kuruhusiwa. Kwa hiyo just take it easy, kwa vyovyote vile watakuwa waliomba wakakubaliwa
Kama ni utaratibu uwe Kwa wote siyo Kwa watu wa tabaka fulani
 
Nasoma comments.

Sikuwahi ona huu utaratibu kwakweli
 
Nasoma comments..
Sikuwahi ona huu utaratibu kwakweli
sikuhiz muda unavosonga hiz sheria zinaanza kujiumbua moja baada ya nyingine.

means zimepitwa na wakati na ziliwekwa kugandamiza akili ya mweusi.
 
Kama ni utaratibu uwe Kwa wote siyo Kwa watu wa tabaka fulani
Una inferiority complex. Kama hujafunga ndoa na unaona ni vyema ukafunga wakati huu wa Kwaresma, peleka hoja zako kwa Paroko wako, kuna mambo huwa wanayazingatia. Ikionekana sababu za msingi zipo, basi utafunga ndoa yako. Usitangulize kuweka kwamba upo tabaka la chini wakati hata haujaomba, au pengine hata mchumba haujapata. Kama una nia kweli nenda tu. Sisi hapa juzi juzi tumeomba ibada ya wafu siku ya Jumapili kwa hoja kwamba tunasafirisha umbali mrefu, na tukapewa tu ibada, wala hakuna mmoja wetu aliyepo kwenye hilo unaloita tabaka la juu
 
Hapo hujadili hoja ila unaleta personal attack........jadili hoja mkuu na Kwa taarifa yako mm siyo mkatoriki ila nimeishi kwenye ukatoriki Kwa miaka kama 6 hivi...... kwahiyo usilete ujuaji sana mkuu
 
Ndoa siyo sherehe mkuu?
mi niliona picha za GIGY MONEY akiwa ndan ya tinted na macho matatu pembeni mzee wa tLp

hata hawakukaa pozi la kikanisani

utazani wasanii PAPA YA MOBIMBA.

Sizani km ilikuwa ni ndoa ile.

kilaini alifafanue hili
 
Ndoa ni sakramenti inayotolewa kanisani, sherehe ni nje ya utaratibu wa ndoa, ndio maana inafanyika nyumbani au ukumbini
Unadhani kwanini utaratibu umewekwa kipindi hiki zisifungwe?
 
Back
Top Bottom