Wakatoliki waanza kuona aibu na fedheha, Papa na Vatican wameharibu sana taswira ya ukatoliki

Mimi ni mkatoliki ninayoijua na kuiamini dini yangu vizuri. Siwezi kuyumbishwa wala kukwazishwa na mtu yeyote hata kama ni pope. Tuko wengi wa aina yangu
Dini umeletewa ili utawaliwe...we Mungu umemjua wapi wewe...unajua nani kaandika biblia, hayo maandiko unayotetea Leo uliyajua wewe au ndo hao hao walioandika...Leo hii unaijua dini kuliko papa... unajua process ya biblia iliyopita mpaka imekufikia wewe...?
 
We unajuaje Sodom na Gomorrah ni actual historical event na sio hekaya za wayahudi?
Mimi siamini kwenye uwepo wa hiyo miji ya Sodoma na Gomora. Najua kwamba Biblia ni fiction stories.

Nawauliza wakatoliki wanao amini maandiko yao ya Biblia na uwepo wa Mungu wao kwamba, Inakuwaje Mungu wao ali angamiza Sodoma na Gomora kwa sababu ya ushoga?

Halafu wao wakatoliki wana wabariki mashoga hao kwa jina la Mungu huyohuyo asiyependa ushoga?

Wao kama wakatoliki hawaoni hii Contradiction?
 
Kaka utapoteza muda na nguvu kwa huyu mpumbavu nahisi hana Watoto wala ndugu kabaki peke yake kwenye familia tree yao
 
Kasome vizuri huo mstari wa Mungu kuangamiza sodoma na gomora uone kama hakuonesha huruma alipoulizwa unataka kuwahukumu wote? katafute uone alijibu nini.
Kama Mungu huyo alionesha huruma kwa watu wa Sodoma na Gomora, Kwa nini ali waangamiza?

Au alionyesha huruma ya kinafiki?

Mwanzoni ulisema Mungu ana vumilia wadhambi, Sasa nakuuliza hivi, 👇

Mungu huyo Alishindwaje kuwavumilia watu wa Sodoma na Gomora?
Tatizo lenu mnakariri maandiko pasipo kuyaelewa, mnakurupuka tu.

Kuamini Mungu ana kisirani kama wanadamu ni ujinga usio na mipaka.
Kama Mungu huyo hana kisirani, Kwa nini mnadai Mungu huyo hapendi dhambi?

Mungu gani ambaye hapendi dhambi ila anapenda wadhambi?

Huyo Mungu ni mnafiki sana na ndumila kuwili.

Atachukiaje dhambi, halafu apende wadhambi?
Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Madhehebu flani wanaoona ukatholiki kama upinga kristu wamepata point 😁😁
Point huwa ipo siku zote hakuna Yesu pale ni biashara za watu na shetani kama mdhamini mkuu.
 
Walianza zamani kunanilii watoto, ilijuwa swala la muda tu. Papa kazingua sana, najua wahafidhina wa kikatoriki wanamlia timing tu kumuondoa.
 
It's not clear kwamba Sodom and Gomorrah wameangamizwa kwa sababu ya ushoga...makosa pale ni mengi mostly ikiwa lack of hospitality kwa wageni na mambo ya rape na Nini..ila ma pastor wa siku hizi wanasema ni ushoga ili kupush agenda zao
 
Imani inajengwa juu ya yesu kristo siyo mtu we mbumbumbi. Papa ni mtu na silazimiki kufata anachosema. Sema hizi dini zenu za mfukoni za akina mwamposa zimewaharibu sana manadhani kwamba dini ni ya mtu ni si ya yesu. Mmefikia hatua hata kumuabudu mtu as if akifa yeye na kanisa linakufa.kama lilivyo kanisa la tb Joshua kwa Sasa halipo
 
Hiyo Imani ni yangu kutokana na mafundisho niliyopata kanisa Katoliki. Sio lazima ninachoamini Mimi na wewe uamini. Wewe amini unachotaka kuamini. Papa kusema wabariki vitu vya mashoga, Mimi kama Mimi sikubaluani nae. Sio lazima nikubaliane na kiongoz wangu kisa tu yeye ni kiongoz. Wewe kama unaona ushoga ni sawa kisa tu haujatajwa kwenye amri za Mungu, sawa endelea kufanya na kuuishi.
 
We na wewe huna point unajua kuandika vitu ambavyo havina mantiki ,ukiyaangalia maswali ambayo umeyaambatanisha kwenye thread Yako ni vitu ambavyo vinapingana

So Kwahiyo unaona sawa kubariki Mali za mashoga ni? Kwenye vitabu vyako ni wapi umeona kumeandikwa na (tukabariki vitu vyao ? Acha kupelekeshwa
 
Kwa hapa Wakatoliki hata wakatae vipi, viongozi wao wa Vatican wamewaangusha sana. Muelekeo wa kanisa uko wazi, kufungisha ndoa za mashoga na kuwa na mapadri mashoga ni ruksaa. Moja ya baraka ni kubariki ndoa zao, tusijidanganye kwa tafsiri nyingi nyingi. Halafu pia hili la kufungusha ndoa haliko mbali, tutaliona tu siku si nyingi.
 
Kanisa linazidi kuimarika zaidi na zaidi. Ni kwambie Sasa kwa tamko lake tu kanisa limeongeza waumini zaidi ya mil 3 duniani kote. Makanisa yenu ndo yanakufa kwa sababu hnaga elimu kabisa. Kila kinachowajia akilini nyie mnanena kwa lugha wakati ni mapepo. Kila siku mwamposa anadai anatoa mapepo lakini hayaishi. Leo ukienda utaambiwa una Pepo na atajifanya kulitoa, kesho ukienda tena anakwambia una Pepo mana yake ulipotoka tu Pepo akakudaka tena. Nilienda siku moja nikajifanya nakunywa pombe kumbe sinywi akanitabilia kwamba usiku nililewa sana kweli si kweli, ilibidi nicheke sana. Makanisa yenu ya kitapeli sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…