Wakatoliki waanza kuona aibu na fedheha, Papa na Vatican wameharibu sana taswira ya ukatoliki

Wakatoliki waanza kuona aibu na fedheha, Papa na Vatican wameharibu sana taswira ya ukatoliki

Kukamia watu ambayo hawafanyi dhambi sawa na wewe...Mimi Bora niwe na rafiki shoga ambaye anafanya mambo yake binafsi bila kumuumiza mtu kuliko nimuamini mchungaji ambae ni mwizi, tapeli, fisadi, mzinzi, mbakaji watoto, muongo, mchoyo na msambaza ujinga na propaganda kwa waumini wake...haya mambo yana madhara makubwa kuliko mtu na mpenzi wake kufanyana ila wanajua mnapenda kukamia ujinga so wanapita na huo upepo...
Nimepata jibu nazungumza na nani sasa, Tuishie hapo tajiri.
 
- Nashangaa mpaka sasa mleta mada bado hajajitokeza kutetea huu ujinga alioandika hapa.

Hii tabia ya mleta mada kuleta uzi halafu anakimbia bila kuutetea uzi wake inaonesha vile alivyo na nia ovu, amekuja kupotosha makusudi akijua vizuri anachoandika ni uongo, huu ni upuuzi usiotakiwa kulelewa hapa JF.

Unaandika uongo makusudi halafu unakaa pembeni kutazama, huu ni sawa na uchonganishi usiokuwa na maana, utoto; kama huwezi kuitetea mada yako next time usiandike ujinga wako hapa.

- Hili sio jukwaa la ushabiki na mihemko, ni jukwaa la facts, kama hauna just shut up.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Dini umeletewa ili utawaliwe...we Mungu umemjua wapi wewe...unajua nani kaandika biblia, hayo maandiko unayotetea Leo uliyajua wewe au ndo hao hao walioandika...Leo hii unaijua dini kuliko papa... unajua process ya biblia iliyopita mpaka imekufikia wewe...?
Wewe kama hujui funga shithole lako
 
Ninyi mmehakikishiwa
Kuhakikishiwa nini, sijakuelewa.

Uislam hauna mfumo wa Kikristo, sisi kila mmoja ni mchungaji (khalifa) wa nafsi yake na wa wenzake.

Usifananishe kabisa, Uislam ni mwema sana, sheria zetu zilikamilika miaka 1,400 iliyopita, mpaka leo hakuna anaeweza kubalisha, kuzipunguza wala kuzizidisha.
 
So kugonga kitoto Cha miaka tisa na kukioa kwako freshi tu...?
 
Hawaujadili ila ndio washiriki wakubwa wa ushoga, uliza wajuzi wakujuze
Haiondoi ukweli uislam hauna room ya kujadili ama ukubaliwe au ukataliwe ni NOOOOO. Lakini kwa papa kila siku anajiuma uma kuhusu ushoga
 
Ukatoliki unaenda kufa kifo Cha mende!! Safi sana!!dhambi ya kuwaua mitume wa kristo inawatafuna .haiji Akilini makao makuu ya katoliki kuwa Roma nchi ya kishenzi iliyomuua Petro mtume mkuu wa ukristo
Ulitegemea Petro ataishi milele ama. Vipi kuhusu waliomuua Yesu?
 
Sio siri tena tangu Papa na Vatican kutoa miongozo ya kuukumbatia ushoga, kwa sasa wakatoliki wengi wameanza kupoteza furaha, amani, ujasiri na ufahari wa kujivunia ukatoliki.

Papa na Vatican walianza kutoa kauli tata za kuona ushoga (kubadili jinsia nk) sio dhambi ya kukemewa na kanisa (yaani mashoga wavumiliwe na kutambuliwa kama sehemu ya waumini ndani ya kanisa katoliki), baadaye wakaja kutoa ruhusa mashoga kuwa wadhamini wa sacramenti za kikatoliki (Ubatizo, Komunio, ndoa) na sasa ruhusa kwa mashoga kubarikiwa! Mwelekeo unaotabiriwa kufuata ni kanisa katoliki kuanza kufungisha ndoa za mashoga na hitimisho ni kanisa katoliki kuja kuruhusu kuwa na makasisi mashoga.

Wengine walijaribu kutetea Kanisa Katoliki kwa kusema Papa na Vatican wamenukuliwa vibaya, lakini kadri muda ulivyokwenda hali imezidi kuwa wazi na mbaya kiasi cha watetezi wa Katoliki kuanza kusalimu amri.

Kwa sasa ukatoliki umewekwa kapu moja na harakati za kuukuza na kuulinda ushoga duniani.

Mwaka huu huenda ndio mwaka mbaya zaidi kwa waumini wa kikatoliki katika kujivunia imani yao. Upepo bado unavuma, mawimbi bado yanaibuka na chombo kimeanza kuyumba huku safari ikiwa imeshika kasi.
Maadui wa ukatoliki yakiwemo makanisa ya mfukoni na ile dini ya shetani yamepata hoja ya kushambulia wakatoliki.
Kwanza kanisa hadi sasa halijaruhusu ndoa za mashoga. Ni kweli kuwa papa amepotoka kwa kuruhusu kundi moja la watenda dhambi kupewa recognition, lakini kwa mfumo wa ukatoliki nguvu iko kwa maaskofu wa majimbo na hata pale vatican papa hana mamlaka ya kidikteta ya kuimpose hoja yake katika dunia ya wakatoliki. Kwa wale mapadre ambao ni watenda dhambi katika baadhi ya nchi hasa za ulaya kama maaskofu wao wanaowasimamia nao ni watenda dhambi ndio watakaobariki mashoga kwani watakuwa hawana kikwazo, lakini huku africa na sehemu nyingi zaidi hizo baraka hazitatolewa.

Natumaini Papa wa sasa atatoka soon na papa mpya atafuta hayo maelekezo.

Kanisa katoliki halijaacha wala halitaacha misingi yake na Yesu hawezi kuruhusu lipotee kwani ndio kanisa lake pekee alilolisimika na alitoa uhakikisho kuwa milango ya kuzimu haitalishinda.

Endeleeni kufurahi enyi maadui wa Kanisa Katoliki lakini ndoto zenu hazitatimia kamwe.
 
Umepotosha kwa kiasi kikubwa, unaonekana hujasoma hata ule waraka wa Vatican, ulichofanya ni kuokoteza maneno kwa wengine na kuja kuanzisha huu uzi wako hapa, hujafanya uchunguzi wowote, sasa hiyo aibu aione nani?

- Kama hutaki mashoga wavumiliwe na kutambuliwa ndani ya Kanisa Katoliki, unataka wezi, waongo kama wewe, na wazinzi, wao pekee ndio waendelee kuvumiliwa? Kanisa Katoliki haliishi kwenye misingi ya kinafiki.

- Kwanini hutaki mashoga wapewe sakramenti kama waumini wengine? au wale wanaopewa ni watakatifu? hayupo yeyote miongoni mwao mwenye dhambi? Hapa unaonesha ulivyojaa ubinafsi, Papa yuko above your thinking capacity.

- Wapi umeona kwenye ule waraka wa Vatican pameandikwa Kanisa Katoliki litabariki mashoga? tuwekee hapa tupaone, kisha nami nitakuwekea pale palipoandikwa Kanisa Katoliki litabariki mali za mashoga, sio mashoga kama ulivyopotosha hapa.

Hii ni sawa na kubariki mali za wengine wasiojulikana tabia na matendo yao, hakuna yeyote anayejulikana kama ni mzinzi sababu hufanyia sirini, mwizi hufanyia sirini, kujaribu kuwatenga mashoga kama vile wao pekee ndio wenye dhambi ni unafiki na ubinafsi, Papa hataki huu unafiki.

Papa anajua miongoni mwetu hayupo aliyekamilika, Kanisa Katoliki pia linajua hivyo, tukianza kutazamana usoni na kutengana mwisho wa siku huko kanisani atabaki nani? injili atahubiriwa nani? hujui hata Yesu Kristu alikuja duniani ili kuwahubiria wenye dhambi wapate kuokoka?

Mna upeo mdogo sana kifikra, na thinking yenu ni ya kijima sana wakati Kanisa Katoliki lilishatoka huko.
Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
denoo JG
Naona unanilaumu bure, nadhani kwa kuwa umepanic.
Umesoma mada yangu na kuelewa?

Embu sema ni upi uongo nimeandika?
Hivi unadhani wakatoliki wana furaha na haya mambo ya Papa kuwakumbatia mashoga kwa mwamvuli wa kanisa katoliki?
 
Maadui wa ukatoliki yakiwemo makanisa ya mfukoni na ile dini ya shetani yamepata hoja ya kushambulia wakatoliki.
Kwanza kanisa hadi sasa halijaruhusu ndoa za mashoga. Ni kweli kuwa papa amepotoka kwa kuruhusu kundi moja la watenda dhambi kupewa recognition, lakini kwa mfumo wa ukatoliki nguvu iko kwa maaskofu wa majimbo na hata pale vatican papa hana mamlaka ya kidikteta ya kuimpose hoja yake katika dunia ya wakatoliki. Kwa wale mapadre ambao ni watenda dhambi katika baadhi ya nchi hasa za ulaya kama maaskofu wao wanaowasimamia nao ni watenda dhambi ndio watakaobariki mashoga kwani watakuwa hawana kikwazo, lakini huku africa na sehemu nyingi zaidi hizo baraka hazitatolewa.

Natumaini Papa wa sasa atatoka soon na papa mpya atafuta hayo maelekezo.

Kanisa katoliki halijaacha wala halitaacha misingi yake na Yesu hawezi kuruhusu lipotee kwani ndio kanisa lake pekee alilolisimika na alitoa uhakikisho kuwa milango ya kuzimu haitalishinda.

Endeleeni kufurahi enyi maadui wa Kanisa Katoliki lakini ndoto zenu hazitatimia kamwe.
Umeandika vitu vya kufirika na kujifariji zaidi kuliko uhalisia.

Tangu lini wakatoliki wameanza kufundishwa kumpuuzia Papa?

Kila mkatoliki ameaminishwa kuwa Papa ndio sauti ya mungu hapa dunia, akisema mungu amesema!

Hivi wewe hujui kuwa ukatoliki umedumu kwa enzi nyingi kwa sababu ya kuuheshimu na kuutii upapa na kauli za Vatican?

Hivi wewe hujui Papa na Vatican wanaweza kumvua uaskofu askofu yoyote wa kikatoliki popote, tena wakati wowote wakitaka?

Nini kitatokea kwenye ukatolìki ikiwa kila jimbo litakuja na msimamo wake tofauti na msimamo rasmi wa Vatican au msimamo wa Papa?
 
Yote yaliyo gizani yatafichuliwa

Ni wakati wa watakatifu wa Mungu kujidhihili ndani ya kanisa Catholic

Huu ni wakati wa muhimu sana katika kanisa kuliko wakati wote ndani ya kanisa

Nyakati kama hizi zimetoa watakatifu wengi sana ndani ya hili kanisa langu,

Kanisa letu ni kama ziwa hupokea uchafu uliojificha kama usafi,Kisha baadae hutapika nje taka zote, Sasa kanisa linatapika , wanaooona kwa macho ya kibinadamu wanafurahii
Kanisa Katoliki linatapika nini wakati limeshameza ushoga na sasa linaimba, kucheza na kupumua ushoga mtupu?

Kuna mtakatifu kuliko Papa ndani ya kanisa Katoliki?
Kama Papa kasema mabwabwa ni sehemu ya kanisa katoliki na wathaminiwe, wewe mkatoliki wa huko mbagala charambe uliyejipaka paka ukatoliki wa kuunga unga unawezaje kupinga?
 
Ukatoliki unaenda kufa kifo Cha mende!! Safi sana!!dhambi ya kuwaua mitume wa kristo inawatafuna .haiji Akilini makao makuu ya katoliki kuwa Roma nchi ya kishenzi iliyomuua Petro mtume mkuu wa ukristo
Mkuu ukatoliki hauendi kufa Bali ndio unaenda kupata nguvu zaidi Ili kuuua uKristo...
 
nasikia anataka kubadili gia angani, kuwa et alinukuliwa vibaya, si unajua alijiweka kimbelefront ndo papa akaja na kauli waache ushamba.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Ruwaich aache ushambaaaa.
 
Back
Top Bottom