Kanisa linazidi kuimarika zaidi na zaidi. Ni kwambie Sasa kwa tamko lake tu kanisa limeongeza waumini zaidi ya mil 3 duniani kote. Makanisa yenu ndo yanakufa kwa sababu hnaga elimu kabisa. Kila kinachowajia akilini nyie mnanena kwa lugha wakati ni mapepo. Kila siku mwamposa anadai anatoa mapepo lakini hayaishi. Leo ukienda utaambiwa una Pepo na atajifanya kulitoa, kesho ukienda tena anakwambia una Pepo mana yake ulipotoka tu Pepo akakudaka tena. Nilienda siku moja nikajifanya nakunywa pombe kumbe sinywi akanitabilia kwamba usiku nililewa sana kweli si kweli, ilibidi nicheke sana. Makanisa yenu ya kitapeli sana
Mi ni mkatoliki pure, na najivunia ukatoliki wangu ,maana ndio umenipa confidence ya kumkili Yesu kristo siyo kwa habari zake tu Toka kwa bible Bali hata kwa miujiza, lakini suala hili la ushoga na msimamo wa kanisa ,hasa Hilo tamko la juzi na Jana Kuna kitu hakipo sawa,na nahisi ni kazi ya Mungu kutuonyesha ni kiasi Gani kanisa limeharibika, Sasa ni wajibu wangu Mimi na wewe kufunga na kuomba kwa ajili ya kanisa ,siyo kutetea tu ili lionekane vyema machini pa watu japo linapotezwa, let's be positive, kama unalipenda kanisa hili kwa thamani lilizokupa utaomba tuu, na ifahamike tu kanisa Bora ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu, mdudu kaingia , Mungu anamtoa kwa kufanya hata yaliyo sirini tuyajue
Kulianza na kashifa ya mapadre kushiriki ushoga pale Roma, ikaja kashifa ya kulawiti watoto, imekuja baraka za jinsia Moja, imefuata na hili la kutenganisha asili na ukisasa , kwamba kung'ang'ana na asili ni jambo linalozuia mabadiliko ndani ya kanisa,. ,,,,,Bado tu hujamruhusu roho MTAKATIFU kuzungumza na wewe?!!!tuombee kanisa, kubadili dini ni udhaifu mkubwa zaidi,. Yanayotokea ni sababu ya vita ya asili kati ya Mwili (wenye uhaeibifu wa kiulimwengu dhidi ya roho) na inavoonekana roho zetu na hata za viongozi wetu zimekuwa dhaifu kwa mwili, maamuzi mengi yamebezi katika kuuridhisha mwili, (ubinaadamu)
Unaongelea waumini million 3!???uko serious kweli!?tunataka watu au tunataka roho zilizoongoka!?kama ni case ya waumini mbona tunaweza pata zaidi ya hao tukisema tugawe K-vant na kupiga sebene church!?
Ninaomba kwa ajili ya kanisa langu katoliki,najua Nini kinaenda kutokea, siyo kwa ajili ya kanisa ila kwa ajili ya ukristo halisi, ikumbukwe hili ndio kanisa mama la ukristo, ila limekuwa chini ya mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke kwa zaidi ya miaka 2000, limeanguka, likachechemea ,likasimama, Tena likaanguka na kusimama Tena, am sure hata hapa litapita ,hata kama ni kwa kuanguka na kusimama Tena , na linaposimama husimama na watu haswaa , this time I ll be among them
Kaa nasi tuitetee imani dhidi ya wavamizi wa kiroho kupitia viongozi tuliowaamini,kubadili dini ni udhaifu mkubwa wa kiimani, maana Kila mtu ana wajibu dhidi ya mwenzake,na siyo kwa ajili yake peke yake, kama bwana wetu Yesu kristo kwa ajili ya ulimwengu hata akayapoteza maisha yake, nasi hivohivo,
Tumsifu Yesu kristo ,
Kristo............