Uchaguzi 2020 Wakazi wa Dar es Salaam kweli na nyie mtamnyima Magufuli kura?

Ccm wenyewe wanajua kama watu wa dar hawajawahi kuiamini ccm. Ccm dar labda sana sana waibe kura. Dar ccm inachukiwa kwa sababu ya bomoa bomoa, watu kama wa kimara unategemea wawape kura ccm
 
Unafikiri Dar wanaishi mapoyoyo kama wa Kongwa kwa Ndugai?
 
Mwenyezi Mungu ni wa haki hivyo hupendezwa na matendo ya haki.

Udhalimu ni machukizo na huambatana na adhabu na ugumu ktk namna tofauti tofauti!

Tumuogope Mungu sana!
 
Dar Es Salaam tumeokotana sana beach tukiwa maiti kwenye viroba.
Na tumetekwa sana ndani ya nchi yetu huru..?!
Magufuli hafai ni Muuaji mkubwa.
Oktoba 28 kura zote za DSM, ni kwa mbeba maono #NIYEYE
 
Kwa nini mnaziba masikio na kung'ang'ania vitu badala ya watu?

Hivyo vitu vitano ni vichache kulinganisha na walivyofanya wakoloni, mbona waliondolewa?
 
Wanazo sana akii tatizo wanatuona sisi mazwazwa
 
Kama kukosea ku type tu ndio mtu awe ana matatizo makubwa hivyo, basi angalia na wewe hilo neno uliloliandika urge
 
Bora hao kuliko hao wetu wa Ndio mzee Rubber stamps.. Wakiulizwa Umeoga? Ndio. Hujaoga? Ndio. Enzi za kina Mzindakaya ilikuwa komesha huwezi fananisha na hizi punda akina Kibajaji
 
watanzania wote kwa umojawetu hajaalishi upo wapi, hakikisha tarehe ishirini na nane unakataa ccm, hawandio chanzo cha umasikini Tanzania, wameua kilimo cha kahawa huko mbozi, wamua mbaazi, wameua korosho, wameaua mji wa dar, maduka ya kubadilishia fedha za kigeni, sijui vitambulisho ya mjasiriaa mali mabayo habita hata sifa ya kuitwa vitambulisho, mambo mengi maovu yamefanywa dhidi ya watanzania, tukatae kwa kumpigia kura Lissu, twende naye tupate utawala wa sheria wa kusheshimu taasisi zilizowekwa kisheria.
 
Kwa nini mnaziba masikio na kung'ang'ania vitu badala ya watu?

Hivyo vitu vitano ni vichache kulinganisha na walivyofanya wakoloni, mbona waliondolewa?
Mkoloni asingenyanyasa watu Hadi leo tungekuwa nae akituletea maendeleo
 
Ndoto za mchana hizo,alisema atakaebaki dar ni mwanaume matokeo yake kakimbia mwenyewe,dodoma kuna fursa gani Hadi iishinde dar, population ndio uchumi wa jiji lolote.
Dodoma bado Sana kuifikia hata Mwanza au Mbeya tu sembuse dar
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…