Wakenya wanajua kuitumia ardhi kwa manufaa zaidi kuwazidi Watanzania?

Tatizo siyo ukubwa wa ardhi, tatizo ni ubora wa AKILI walizonazo hao watu wenye ardhi. Akili yako ikiwa mbovu, hata uwe na ardhi au rasilimali zingine nyingi au kubwa kiasi gani, bado ardhi au rasilimali hizo hazitakusaidia wala hazitakunufaisha.
 
Mpaka sasa bado sijajua sababu ya Serikali kuingilia soko la kahae na korosho. Kwa nini mkulima asiruhusiwe kuuza mazao yake kwa bei na mahali atakayopenda, hata kama ni Ulaya?
 
Wao wanawezaje kuipeleka huko kwao kutokea Tanzania lakini Watanzania wanashindwa kuwapelekea wao huko kwao Kenya au kupeleka kwa wateja "wengine" huko dunianai?
 
muda ukiwa sawa hakuna shaka niko dar nimekuja kufanya operation ya cataracs CCBRT jicho linasumbua, ila uwe a shmba, nakaa shamba huko huko
Pole sana mkuu. Ugua pole.

Mimi nayamudu mazingira yote:

1. Kukaa kwenye hoteli ya nyota tano

2. Kulala shambani kwenye banda la majani ambalo mlango wako ni kipande cha gunia

3. Kutumia usafiri wa ndege

4. Kutembea kwa miguu kwa masaa mengi bila kupumzika, hata zaidi ya masaa kumi, ikibidi.

5. Kuvaa kinadhifu

6. Kuvaa ",kishamba", ikibidi, na kutembea peku

7. Kulima muda mrefu kwa jembe la mkono, muhimu tu nisiwe na njaa. Naweza nikakaa shambani Asubuhi hadi Usiku

Kwa kifupi, ninayaweza mambo yote...
 
Mpaka sasa bado sijajua sababu ya Serikali kuingilia soko la kahae na korosho. Kwa nini mkulima asiruhusiwe kuuza mazao yake kwa bei na mahali atakayopenda, hata kama ni Ulaya?
Na ni cash crops zote .
Imagine bei ya kahawa hapo Uganda ni mara mbili ya bei ya Tanzania ,ila mkulima akivuna hawezi ruhusiwa kupakia kwenye fuso aende Kampala kuuza kahawa yake aliyovuna , ni mwiko .
Unakuta wakulima wamedumaa na mfumo wa kipumbavu wa ushirika ambao kwanza malipo ni madogo mno yasiyo endana na hali halisi na yanachelewa sana .
Huwezi kutoboa kwa mwendo huu
 
Wao wanawezaje kuipeleka huko kwao kutokea Tanzania lakini Watanzania wanashindwa kuwapelekea wao huko kwao Kenya au kupeleka kwa wateja "wengine" huko dunianai?
Wakenya wanalangua matunda na mbogamboga wanapeleka kwao kufanya package na kuuza nje ,mkuu kuuza mboga na matunda nje ya nchi sio kwamba unaamka tu na unajiamlia kuna utaratibu maalumu na makubaliano ambayo serikali ya nchi husika lazima ifanye na nchi unayoenda kuuza hizo bidhaa .
Sisi balozi zetu zimelala hazifungui masoko na kuingia mikataba ya kibiashara ya kumnufaisha mkulima directly ,sasa hilo ni tatizo .
Huwezi leo hii ukasema umelima zako Matango ,tikiti , spinach organic fresh kwenye greenhouses zako halafu unataka ukayauze UK bila pre agreement na vibali maalumu , haipo hiyo .Bidhaa yako yenye package na mambo ya Tanzania toka Tanzania haiwezi ingia UK bila makubaliano ya Tanzania na UK na vibali maalumu vya ukaguzi kuhusiana na hiyo bidhaa unayopelekea .
Hii haifanywi na raia ,ni kazi ya serikali kufungua hizi fursa
 
Sidhani kama ni lazima uamini
Ila Mimi nimeamini mkuu! Angalia
1. Ana wafanyakazi anaowalipa kila mwezi. Na hao wafanyakazi wanakula na kunywa kwa gharama za bustani. Kuna wanaoingja Asubuhi na kutoka Jioni na kuna wanaolala shambani kwenye nyumba zilizopo shambani.

2. Huwalipa wataalam kila anapiwaita kwa jambo fulani la kikazi.

3. Kaweka miundombinu ya uhakika.

4. Kuna gari la "maana" mahsusi kwa shughuli za shambani

5. N.k.
 

Kabisa mkuu,jamaa wameamka na wanachangamkia fursa
 
Ok! Ok! Nashukuru mkuu!!!

Naona kama wazo linanijia la kwenda kufungua biashara Kenya! Nitaona!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…