Wakili Ishabakaki: Idris Sultan anahojiwa kwa kuicheka picha ya Rais


Yote uliyoyasema hapa hayana maana kama tu hujaiona picha, in fact alichokifanya Idriss ni kuunganisha picha ya Rais pamoja na video yake akiwa anacheka, niliiona punde tu alipoiweka kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Nakushauri utafute kwanza hiyo video ndipo tuuanze mjadala.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Angeachana na hizo mambo za rais akatengeneza vichekesho vingine,
Africa sio USA muelewe hilo.

Boost your Immune System to fight a Covid-19.
 
Lakini picha inajieleza jamani kama gunia la mkaaa
 
Kumbe kucheka picha ya Rais ni kosa?
 
kwa hiyo Jpm hachekwi [emoji23][emoji23]

Hii nchi kuja kuendelea ni kazi sana kwa mentality hizi [emoji23][emoji23][emoji23][emoji3069]

Mkulima wa mahindi
Tuna taifa lawajinga, waoga na watumwa wa akili halijawahi tokea.
Zikitokea issues kama hizi halafu ukaanza kusoma comments za watu unaweza kulia, kwanini nimezaliwa zama hizi na nchi hii.
Hii ni 2020 akili zetu ni Paleolithic Period
 
Vijana wa sasa hawana staha hawajui miiko na tamaduni zetu zilizotuunganisha kuwa jamii madhubuti.....utandawazi umewalevya kiasi cha kuiga kizuzu tamaduni za nje wakijihisi ndio maendeleo kumbe ni ufala tu.
Kiongozi, wazazi, na watu waliokuzidi makamo wana heshima zao ambazo wanastahili kupewa. Kuwadhihaki tena hadharani ni utovu wa nidhamu na sio kawaida yetu.
 
Seriously! Yaani ni kosa kumcheka Rais? Tena picha ya mtu aliekuja kuwa Rais!!! Seriously?
WAtu naona wana toa mapovu mm nilibyoelewa ninkuwa Unaweza ikawa chochote kwenye hiiDunia. Ilimradi uweke nia na kuofanyia kz na zaidi nilichoona nikuwa mwonekano I wako wa zamani haureflect fauna mahusiano na future yako....Picha za namna ile ziko nyingi sana kila mtu anayo na ukitizama leo lazima ucheKE
 
Na usikute wala Jpm hajui chochote UNAMJUA teacher mpamire wa UGANDA
 
Umaarufu unatofautiana huyo atapata umaarufu kwa wajinga
UNAMJUA teacher mpamire wa UGANDA Na the more unavyomzuia ndani ndo unamzidishia umaarufu We should take it normal
 
Hivi ni mimi tu sijaona hiyo video ya idriss au tuko wengi?

Yani sielewi chochote acha tu nisome comments sina namna.
Ipo clip iddy anacheka mpk chozi Linamtoka
Mpaka anataka kuanguka kwa kucheko
Nahs Hali Ile imeonesha kama Ana mdhiaki rais
Na kwa. Kitendo kile lazima apate dhoruba
Na akitoka sijui kama atarudia

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alafu hajacheka Mara 1 ujue
Matatizo mengine ni ya kujitakia

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kufanya kosa sio kosa, kurudia kosa ndio kosa.

Asiefunzwa na *****, ufunzwa na ulimwengu.

We ushaona wahusika awapendi mzaha wa aina yako kumfanyia raisi, umeponea chupu chupu mara ya kwanza unaenda unarudia tena.

Ata kama ni petty issue kwa mtazamo wa wengi (which is) lakini wenye mamlaka awapendi sasa kwanini urudie. Ni vigumu sana kumhurumia mtu kama huyo.
 
Bado sioni kosa la "kuwekwa rumande bila dhamana" kwenye hali hiyo uliyoielezea hapo; na bado nakushangaa kabisa umepatwa na mkasa gani kuyashangilia haya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…