Wakili Ishabakaki: Idris Sultan anahojiwa kwa kuicheka picha ya Rais

Kosa la dogo ni la kujitambua. Kosa la kuishi maisha ya kizungu wakati yeye ni mtanzania mwenye asili ya kiafrika. Ni kosa la kutojua values zetu kama jamii ya kitanzania ni zipi. Huyu ndiye mwakilishi wa wote ambao wanaweza kutumiwa na maadui wa nchi yetu na akakubali pasipokuelewa madhara yake kwa jamii yetu. Ni kosa la kuwafundisha vijana wote tabia mbaya kwa kadri ya tamaduni zetu za kitanzania zinazotambua kuwa wakubwa hawapashwi kudhihakiwa. Kama watu wenye dhamana katika nchi hii hatuwezi kukubali huu ujinga kwakua una madhara kwa watoto wetu ambao tumewalea kwa misingi ya kitanzania.

Hata kukaa ndani tu inatosha kumfunza. Sheria zenyewe nyingi ziliwekwa na mkoloni then mnajificha nyuma ya kivuli cha sheria...Subiri akimaliza huyu Mh. Naingia mimi mpaka mnyooke kama rula.
 
Napoona comment zenye akili na busara kama hizi napata nguvu kwamba tunao watu wenye kujitambua katika nchi hii.

Thank you sir for easying my mind and blessing my soul today
 
Nani ka kwambia hakuna sheria? Hiyo kwanza ni cyber crime japo mie sheria siyo mtaalamu. Alipata wapi concert ya wenye picha kuitumia kwa jinsi yoyote ile? Was it a public property? Hiyo picha ni mali ya hao watatu licha ya kuwa ina image ya mkuu wa nchi kwa sasa.

Germany kwa sasa hata public photos lazima ziwe signed na wahusika kutumia na lazima kuwa na photo crediting...Yehe hata ku acknowledge photo crediting haipo alafu ameitumia kwa personal gains.

Kama ana ki akili kidogo kimebaki na haiba kwenye nafsi yake aombe radhi na muache nyie wapambe msio na misingi kumpotosha. Mh. Rais ni mtu mwelewe mwenye upendo wa kweli siyo kinafiki, naamini atamsamehe.
 

Unaniwekea maneno mengi sana ambayo hata sijayagusia, mara nyumba za nyasi, mara GMO.

Tubaki kwenye mada ya uhuru wa watu kuchekana, kukosoana.

Usinitoe kwenye reli.

Kwa hiyo unaona Magufuli kutoa kauli za kejeli, dharau za kishenzi na vitisho, ambazo hazikubaliki kwenye ustaarabu wowote, kwamba atawapiga mpaka shangazi za wapinzani wake, mfano mmoja kati ya mingi tu ya kauli mavi za Magufuli ni sawa.

Lakini yeye mtu akimcheka tu kwa kuwa kavaa suti mswelepwete si sawa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magufuli alimbaashia Mama Salma Kikwete live kwenye hotuba.

Halafu huyu ndiye mtu hata kumcheka tu iwe nongwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiranga heshima yako...I think unajua neno "context" ambayo hainaga 1+1=2.

Hata kama yeye angekuwa kakosea haina maana mwingine afanye yale yale, for two wrongs never make a right. Na kama kweli anakosea kuna jinsi ya kumwajibisha yeye kama politician kuna Sanduku la kura, akiwajibishwa huko tutajua kweli hatukupenda hiyo context yake kama mwanasiasa ila akipata kura za kishindo ndiyo ujue tulikubali na yenyewe ni regulatory mechanism kwa mtu wa calibre yake. Madogo kama hawa wana madhara sana kwa vijana wetu, njia pekee ni hizi za kuwafinya kidogo ili wengine wao wajue hii siyo sawa.
 
Heshima ni kujiheshimu.

Hutakiwi kufanya mambo ya aibu halafu bado utake heshima.

Whats good for the goose is good for gander.

Hizi sheria za kuwakinga viongozi, lese majeste, ni medieval.

Kiongozi anatakiwa awe na protection ndogo zaidi ya kisheria kwenye kukejeliwa kuliko raia wa kawaida.

Yani inatakiwa iwe kuna adhabu kubwa sana kwa Magufuli kutishia kupiga shangazi za wapinzani wake, kuliko adhabu ya Idris kumcheka Magufuli.

Kwa sababu Idris ni comedian tu, hana dhamana ya kuchaguliwa na watu. Magufuli anatakiwa kujiheshimu zaidi kwa sababu kachaguliwa na watu.

Katika nchi nyingi sana kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya nchi kukosa uhuru wa watu kujieleza na watu kuwa na uwezo mdogo wa kiuchumi.

Sasa hivi tunaambiwa kwamba serikali ilificha mikopo mingi sana ya ajabu, hata haikutajwa katika bajeti.

Sasa wananchi wanaotishwa kwa kucheka suti ya rais tu, wataweza kuhoji matumizi ya mabilioni ya fedha aliyofanya huyu Mungumtu wa kujitakia wenyewe?




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na yule aliyetoa formula ya dawa tiba Ya corona ya pilipili kichaa na upupu ati akakamatwa lkn nimesikia ktk moja ya mchanganyiko wa majani ya tiba kwa maradhi hayo ni pilipili kichaa kwamba inaaminika kusaidia sana, sasa kijana yule atafutiwa yale mashtaka au la?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wanashindwa kuelewa,hajakamatwa sababu ya kumcheka,mbona hata wewe ukiamua unacheka Ile picha kwa Nini usikamatwe?
Hoja ni kwamba kwa Nini ucheke halafu utupie kwenye social media huku ukiicheka?
Kama angecheka weeeee kwenye social media bila ya picha Nani angehangaika nae?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kucheka ni jinai?
 
Rais ni mtu tu.

Anachekwa, majumbani, kwenye social media.

Serikali ikitaka kufunga watu kwa hili, itachekesha zaidi.

Utasikia dunia nzima watatangaza kwenye habari, serikali ya Magufuli inafunga watu wanaomcheka Magufuli.

Atakuwa kichekesho zaidi.

Atachekesha zaidi ya hiyo suti mswelepwete.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa ukiamua kung'ang'ania maneno yako tutafanyaje...Itabidi tu tukuache kama ulivyo. Vinginevyo hakuta kuwa na tofauti.

We uchukue picha ya mtu ambaye hajakupa concert uanze kuifanyia your project kwa faida binafsi kisha inaacha tungo tata kwa jamii uachwe!

Kwamba! Hii ni Tanzania ina value zake
 
Value gani na ziliwekwa na nani na kwa nini kila mtu azifuate?

Kipanya na cartoonists wengine wanamchora rais kwa caricature karibu kila wiki.

Na wao mtawafunga kwa sababu wanamdhalilisha rais?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulimbukeni wa mitandao ya kijamii ili kupata likes na views ndio kinapelekea watu ku-share kila kitu.

Inatosha ukicheka na kufurahi binafsi, alichofanya Idris asingeweza fanya kwa baba yake au ndugu.

HOPE>fear
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…