Wakili Ishabakaki: Idris Sultan anahojiwa kwa kuicheka picha ya Rais

Wakili Ishabakaki: Idris Sultan anahojiwa kwa kuicheka picha ya Rais

Kosa la huyo dogo Idris ni lipi?

Ku-juxtapose picha inayosadikika kuwa mmoja wa watu wanaoonekana ni Rais Magufuli na clip ya yeye akionekana kucheka?

Na ‘culture’ yetu uliyoitaja ndo ipi? Hiyo ‘culture’ yetu ndo inayokataza watu kucheka? Inakataza watu kuwa na utani?

Bullshit! Dogo hajatenda kosa lolote lile.

Hiyo picha hata mimi imenichekesha. Sema sina tu muda wa hayo ma Twitter na sipo huko kwenye hayo mamitandao mengine.

Zaidi ya ubabe, ujinga, vitisho, na ushamba, Magufuli na dola yake hawana kesi yoyote ile iwezayo simama kwa merits zake dhidi ya huyo dogo. Wanalazimisha mambo tu.

Hiyo picha, kama kweli huyo anayedhaniwa kuwa ndo yeye aliyetokelezea kwenye hiyo suti, basi inachekesha.

Na si lazima iwe inachekesha kwa watu wote. Kama wewe na Magufuli mnaona haichekeshi, sawa.

Hiyo ni haki yenu. Lakini, hiyo haina maana ya kwamba ndo mminye haki za wengine [akiwemo] Idris, kucheka.

Just as you can’t legislate stupidity. The same goes for humor. You can’t legislate it. You also can’t infringe others from enjoying it, either.

Magufuli [and his ilk] are country bumpkins - chambilecho Kiranga
Kosa la dogo ni la kujitambua. Kosa la kuishi maisha ya kizungu wakati yeye ni mtanzania mwenye asili ya kiafrika. Ni kosa la kutojua values zetu kama jamii ya kitanzania ni zipi. Huyu ndiye mwakilishi wa wote ambao wanaweza kutumiwa na maadui wa nchi yetu na akakubali pasipokuelewa madhara yake kwa jamii yetu. Ni kosa la kuwafundisha vijana wote tabia mbaya kwa kadri ya tamaduni zetu za kitanzania zinazotambua kuwa wakubwa hawapashwi kudhihakiwa. Kama watu wenye dhamana katika nchi hii hatuwezi kukubali huu ujinga kwakua una madhara kwa watoto wetu ambao tumewalea kwa misingi ya kitanzania.

Hata kukaa ndani tu inatosha kumfunza. Sheria zenyewe nyingi ziliwekwa na mkoloni then mnajificha nyuma ya kivuli cha sheria...Subiri akimaliza huyu Mh. Naingia mimi mpaka mnyooke kama rula.
 
Laughing as itself, is not a criminal offense....

May be, it becomes an offense with the way or style of laughing....

How a merely citizen like that young man from nowhere stand and laugh an old designed oversized suit of " The his Majesty, Excellence, Most high President John Pombe Magufuli??"

The action of this youngman has totally caused "emotional distress" to the president hence failing to properly perform his day to day duties...!!
Napoona comment zenye akili na busara kama hizi napata nguvu kwamba tunao watu wenye kujitambua katika nchi hii.

Thank you sir for easying my mind and blessing my soul today
 
Na ndo maana wanapoona sasa hakuna Sheria ya kumshitaki nayo wataamua kumfungulia mashitaka ya uhujumu uchumi,na haya ni madhara ya kufukuzana na upepo unapoona haushikiki unaamua kushika kitu chochote na kusema huu ndiyo upepo niliokuwa naufukuza,na hapo utalazimisha watu wote waamini kuwa huo ndiyo upepo.kwa wale ambao hawataamini utawasweka tena ndani kwa sababu mazoea ya kuweka watu ndani kwavile una mamlaka,hujenga Tabia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nani ka kwambia hakuna sheria? Hiyo kwanza ni cyber crime japo mie sheria siyo mtaalamu. Alipata wapi concert ya wenye picha kuitumia kwa jinsi yoyote ile? Was it a public property? Hiyo picha ni mali ya hao watatu licha ya kuwa ina image ya mkuu wa nchi kwa sasa.

Germany kwa sasa hata public photos lazima ziwe signed na wahusika kutumia na lazima kuwa na photo crediting...Yehe hata ku acknowledge photo crediting haipo alafu ameitumia kwa personal gains.

Kama ana ki akili kidogo kimebaki na haiba kwenye nafsi yake aombe radhi na muache nyie wapambe msio na misingi kumpotosha. Mh. Rais ni mtu mwelewe mwenye upendo wa kweli siyo kinafiki, naamini atamsamehe.
 
Nani ka kwamba huo mnaouita utajiri ndiyo maana ya utajiri?

Au hamkusikia WHO ikiwaambia Africa hatujafa kwa hili gonjwa kwakua tuna watu ambao siyo obese...Then obesity ndiyo utajiri?

Poleni sana...Hii ndiyo ile dhana ya kutaka kuona nyumba ya majani na udongo inayoweza ku control temperature kwa whether ya tropics ni ushamba ila ya bati inayoleta baridi usiku na joto kali mchana ndiyo ustaarabu, kisha mwenye ng'ombe 1000 ni masikini lakini mwenye makaratasi yenye picha na tarakimu ndiyo tajiri, what a mind? Hapo nani ana uelewa wa science katika ujenzi na mali kati ya walioweza kuja na materials ya temperature control na wale wanao copy pasipo context?...utumwa usio na jina. Sisi ni masikini kwakua tuna watu wengi kama ninyi mnaopenda vya watu na kusahau kisha kuvidharau vya kwenu vyenye thamani...Mnapenda kutumikia na kuheshimu weupe mkiwadharau wale wote ambao wanajiamini na kuwapenda kweli watu wao.

Unataka kusema kula mboga za kikwetu, matunda yenye vitamins na madini yote na yenye afya ni ushamba na kula GMOs ndiyo maendeleo? Poleni sana...Watu kama ninyi ndiyo mmesababisha dunia kukosa value mpaka mkaamua kuendeleza tabia za aibu za jinsia moja kuoana mkiyaita maendeleo. Mtoto kukosa utii eti ndiyo kujiamini...Ndiyo maana wengi wa ninyi mlitoroka kwenu mkaenda kuishi kitumwa nchi za watu...poleni sana. Ngoja sisi turudishe nidhamu na utu na kuweka maana nyingine ya maendeleo ndiyo ikifikia wakati huo tutaweza kujua tofauti ya maendeleo na kukosa ufahamu kwa jinsi mlivyoleweshwa na mvinyo wa kutukuza weupe.

Unaniwekea maneno mengi sana ambayo hata sijayagusia, mara nyumba za nyasi, mara GMO.

Tubaki kwenye mada ya uhuru wa watu kuchekana, kukosoana.

Usinitoe kwenye reli.

Kwa hiyo unaona Magufuli kutoa kauli za kejeli, dharau za kishenzi na vitisho, ambazo hazikubaliki kwenye ustaarabu wowote, kwamba atawapiga mpaka shangazi za wapinzani wake, mfano mmoja kati ya mingi tu ya kauli mavi za Magufuli ni sawa.

Lakini yeye mtu akimcheka tu kwa kuwa kavaa suti mswelepwete si sawa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo ndo imekuwa MO yao.

Wanakukamata. Wanakusweka ndani. Halafu wanakubambikia mashtaka.

Hicho ndicho wanachoweza. Uhalifu wa kweli [kama wa jaribio la kumuua Tundu Lissu] hawana ubavu, weledi, wala uthubutu wa kuufanyia uchunguzi.

Wanaishia kuhangaika na wachekeshaji wa kwenye mitandao wasio na athari zozote zile kwa yeyote yule.

Sema tu kwa vile sisi jamii yetu haiko litigious. La sivyo, huyo dogo angekuwa na kesi moja nzuri sana!

First of all, hiyo picha inachekesha sana, kwa maoni yangu.

Hivi Magu ni mfupi hivyo kweli? Dude in the photo looks like is about 5’2 - 5’4, at the most.

Standing there with his oversized suit...looking too cool [emoji41] for school and shit[emoji3]. That picture is funny as hell.

What’s more offensive, though, is the arrest of the young man and what is alleged to have done.

I don’t think the photo was doctored in any way. He simply just laughed.

Laughing is offensive now? Where they do that at?

Serikali ya Magufuli imekuwa ni serikali ya vitisho kwa watu. Magufuli anatania mpaka wake za watu. Leo yeye can’t take a joke?

Ila, pengine mambo kama haya ndo yanaweza kutufanya tusonge mbele kwenye mambo ya freedom of speech.

Angalia hata Marekani kwa mfano...makundi ya hip-hop kama 2 Live Crew na N.W.A. yalipata misukosuko mingi sana kwenye miaka ya 80 hadi ya 90 dhidi ya maneno yaliyokuwa kwenye nyimbo zao.

2 Live Crew moja ya kesi zake ilifika mpaka US Court of Appeals, 11th Circuit. Hadi kwenye US Supreme Court, kesi ilifika na Uncle Luke na wenzake wakashinda....mambo ya free speech hayo.

Leo hii 2 Live Crew na N.W.A. ni moja pioneers wa hip hop wanaoheshimika.

Magufuli is not a god. He is not above criticism nor below praise. He can be lampooned and caricatured.

His deification should stop.
Magufuli alimbaashia Mama Salma Kikwete live kwenye hotuba.

Halafu huyu ndiye mtu hata kumcheka tu iwe nongwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo unaona Magufuli kutoa kauli za kejeli, dharau za kishenzi na vitisho, ambazo hazikubaliki kwenye ustaarabu wowote, kwamba atawapiga mpaka shangazi za wapinzani wake, mfano mmoja kati ya mingi tu ya kauli mavi za Magufuli ni sawa.

Lakini yeye mtu akimcheka tu si sawa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kiranga heshima yako...I think unajua neno "context" ambayo hainaga 1+1=2.

Hata kama yeye angekuwa kakosea haina maana mwingine afanye yale yale, for two wrongs never make a right. Na kama kweli anakosea kuna jinsi ya kumwajibisha yeye kama politician kuna Sanduku la kura, akiwajibishwa huko tutajua kweli hatukupenda hiyo context yake kama mwanasiasa ila akipata kura za kishindo ndiyo ujue tulikubali na yenyewe ni regulatory mechanism kwa mtu wa calibre yake. Madogo kama hawa wana madhara sana kwa vijana wetu, njia pekee ni hizi za kuwafinya kidogo ili wengine wao wajue hii siyo sawa.
 
Kiranga heshima yako...I think unajua neno "context" ambayo hainaga 1+1=2.

Hata kama yeye angekuwa kakosea haina maana mwingine afanye yale yale, for two wrongs never make a right. Na kama kweli anakosea kuna jinsi ya kumwajibisha yeye kama politician kuna Sanduku la kura, akiwajibishwa huko tutajua kweli hatukupenda hiyo context yake kama mwanasiasa ila akipata kura za kishindo ndiyo ujue tulikubali na yenyewe ni regulatory mechanism kwa mtu wa calibre yake. Madogo kama hawa wana madhara sana kwa vijana wetu, njia pekee ni hizi za kuwafinya kidogo ili wengine wao wajue hii siyo sawa.
Heshima ni kujiheshimu.

Hutakiwi kufanya mambo ya aibu halafu bado utake heshima.

Whats good for the goose is good for gander.

Hizi sheria za kuwakinga viongozi, lese majeste, ni medieval.

Kiongozi anatakiwa awe na protection ndogo zaidi ya kisheria kwenye kukejeliwa kuliko raia wa kawaida.

Yani inatakiwa iwe kuna adhabu kubwa sana kwa Magufuli kutishia kupiga shangazi za wapinzani wake, kuliko adhabu ya Idris kumcheka Magufuli.

Kwa sababu Idris ni comedian tu, hana dhamana ya kuchaguliwa na watu. Magufuli anatakiwa kujiheshimu zaidi kwa sababu kachaguliwa na watu.

Katika nchi nyingi sana kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya nchi kukosa uhuru wa watu kujieleza na watu kuwa na uwezo mdogo wa kiuchumi.

Sasa hivi tunaambiwa kwamba serikali ilificha mikopo mingi sana ya ajabu, hata haikutajwa katika bajeti.

Sasa wananchi wanaotishwa kwa kucheka suti ya rais tu, wataweza kuhoji matumizi ya mabilioni ya fedha aliyofanya huyu Mungumtu wa kujitakia wenyewe?




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na yule aliyetoa formula ya dawa tiba Ya corona ya pilipili kichaa na upupu ati akakamatwa lkn nimesikia ktk moja ya mchanganyiko wa majani ya tiba kwa maradhi hayo ni pilipili kichaa kwamba inaaminika kusaidia sana, sasa kijana yule atafutiwa yale mashtaka au la?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wanashindwa kuelewa,hajakamatwa sababu ya kumcheka,mbona hata wewe ukiamua unacheka Ile picha kwa Nini usikamatwe?
Hoja ni kwamba kwa Nini ucheke halafu utupie kwenye social media huku ukiicheka?
Kama angecheka weeeee kwenye social media bila ya picha Nani angehangaika nae?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wanashindwa kuelewa,hajakamatwa sababu ya kumcheka,mbona hata wewe ukiamua unacheka Ile picha kwa Nini usikamatwe?
Hoja ni kwamba kwa Nini ucheke halafu utupie kwenye social media huku ukiicheka?
Kama angecheka weeeee kwenye social media bila ya picha Nani angehangaika nae?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kucheka ni jinai?
 
Watu wanashindwa kuelewa,hajakamatwa sababu ya kumcheka,mbona hata wewe ukiamua unacheka Ile picha kwa Nini usikamatwe?
Hoja ni kwamba kwa Nini ucheke halafu utupie kwenye social media huku ukiicheka?
Kama angecheka weeeee kwenye social media bila ya picha Nani angehangaika nae?

Sent using Jamii Forums mobile app
Rais ni mtu tu.

Anachekwa, majumbani, kwenye social media.

Serikali ikitaka kufunga watu kwa hili, itachekesha zaidi.

Utasikia dunia nzima watatangaza kwenye habari, serikali ya Magufuli inafunga watu wanaomcheka Magufuli.

Atakuwa kichekesho zaidi.

Atachekesha zaidi ya hiyo suti mswelepwete.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais ni mtu tu.

Anachekwa, majumbani, kwenye social media.

Serikali ikitaka kufunga watu kwa hili, itachekesha zaidi.

Utasikia dunia nzima watatangaza kwenye habari, serikali ya Magufuli inafunga watu wanaomcheka Magufuli.

Atakuwa kichekesho zaidi.

Atachekesha zaidi ya hiyo suti mswelepwete.


Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa ukiamua kung'ang'ania maneno yako tutafanyaje...Itabidi tu tukuache kama ulivyo. Vinginevyo hakuta kuwa na tofauti.

We uchukue picha ya mtu ambaye hajakupa concert uanze kuifanyia your project kwa faida binafsi kisha inaacha tungo tata kwa jamii uachwe!

Kwamba! Hii ni Tanzania ina value zake
 
Sasa ukiamua kung'ang'ania maneno yako tutafanyaje...Itabidi tu tukuache kama ulivyo. Vinginevyo hakuta kuwa na tofauti.

We uchukue picha ya mtu ambaye hajakupa concert uanze kuifanyia your project kwa faida binafsi kisha inaacha tungo tata kwa jamii uachwe!

Kwamba! Hii ni Tanzania ina value zake
Value gani na ziliwekwa na nani na kwa nini kila mtu azifuate?

Kipanya na cartoonists wengine wanamchora rais kwa caricature karibu kila wiki.

Na wao mtawafunga kwa sababu wanamdhalilisha rais?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulimbukeni wa mitandao ya kijamii ili kupata likes na views ndio kinapelekea watu ku-share kila kitu.

Inatosha ukicheka na kufurahi binafsi, alichofanya Idris asingeweza fanya kwa baba yake au ndugu.

HOPE>fear
 
Back
Top Bottom