Hii ni mbinu sahihi kabisa na imefanywa makusudi kwa sababu hizi;
1. Urio ndio alikuwa mtoa habari mkuu wa kesi nzima.
2. Mkaguzi Swila ndiye aliyekuwa mpelelezi wa kesi hii. Yeye ndio aliyefungua kesi, kupewa maelekezo na Kinga, kuomba vyombo vya uchunguzi kufanya kazi zake na hata kumhoji mtoa taarifa na hata kuandika maelezo ya Kingai.
Baada ya watu hawa, kesi itakwenda haraka sana ili utetezi nao ulete mashahidi wao. Ninahofia kuwa kutakuwa na mashahidi wa utetezi wengi waliohusishwa na Kaaya, Urio na kesi ya ugaidi kuliko Mbowe. Nina dhana kuwa uchunguzi dhidi ya makomandoo inatokana na zile mambo za Kibiti - Mbowe aliingizwa tu baada ya kuona amewasiliana na Urio ambaye alikuwa na kazi ya kuchoma makomandoo wote wasio kazini!!