Wakili Mwabukusi na Mdude Nyagali kushtakiwa kwa makosa ya UHAINI

Wakili Mwabukusi na Mdude Nyagali kushtakiwa kwa makosa ya UHAINI

Tuweni wakweli na msema kweli ni kipenzi cha Mungu.
Unaposema utaiangusha serikali ya Tanzania chini ya mwevuli wa CCM ikiongozwa na Mh.Samia Suluhu au kusema Utaishinda serikali ya Tanzania chini ya mwevuli wa CCM ikiongozwa na Mh Samia Suluhu.

Sasa waliosema tuseme wakubali tu kuwa wameteleza sio lengo lao ili yaishe.
" Kusema utaitisha maandamano ya nchi nzima yasio na ukomo tena mtahakikisha mpaka serikali ya Tanzania chini ya Mheshimiwa Samia suluhu mnaiondosha madarakani kabla ya muda wake"
Ingependeza kusema mpaka inajiuzulu na sio kusema mnaiondoa madarakani.

Kuondoa madarakani inaweza kuwa kwa hayo maandamano yatakayokuwa hayana mwisho mwema yenye lengo la kufanya mapinduzi baridi au ya moto kuiondoa serikali madarakani ,tumeona maandamano ya aina hio yakitokea Misri / Egypty (maarufu Arab Spring).

Maandamano yao hayakuwa na mwisho mwema.
Yalikuwa ni kama hayo yaliotajwa na Chadema kuipinga serikali iliyopo madarakani yalikuwa ni maandamano yaliyokuwa na lengo moja tu kuipinduwa serikali ndani yake walikuwemo waasi wenye silaha na yalienea nchi nyingi za kiarabu yalianzia Tunisia 2010 .
Maandamano hayo yalifanikiwa kuipindua Serikali ya Tunisia,Algeria Jordan Misri ila Yeman na Libya yalisababisha mtafaruku wa vita vya wenyewe kwa wenyewe hadi leo bado hizo nchi hazijakaa sawa.
Hio ndivyo Historia inavyotuambia ,leo hii viongozi wa Chadema wameonekana majukwaani wakitaka kuirudia historia hio kuanzia hapa Tanzania.

Waliotiwa hatiani wana kesi ya kujibu tusijikite upande mmoja,nasema tu wajiteetee kama kuku anaekaribia kutaga kuwa waliteleza na sio lengo lao.
 
Serikali ya inayoongozwa na Samia Suluhu imeingia mkataba wa bandari Chadema wameingia mkataba wa Maandamno ,wote wamefuata waarabu.
Kuwa uone mambo.
nani amekamata mpini Chadema walilisahau hilo na kuuvaa mkenge. wapo na too much know without knowing nothing of the end.
 
Mwambieni Mama auaye Kwa upanga atauawa Kwa upanga, Mtu mwenye ufahamu hujifunza kutokana na makosa ya waliomtangulia.
Ni kweli Mh rais hajajifunza Kwa jiwe?.
 
mama karuhusu uhuru wa maoni lakini,lakini maoni yanamuelemea.
 
Nenda kawatete mahakamani unafikili police niwajinga waliwaacha mda mrefu wakajisahau na matamshi yao yenye utata. Walikuwa na nia nzuri ila strategy yao haikuwa nzuri kwa afya ya umoja wetu wa kitaifa. Pakitokea civil unrest tutaenda wapi watu wako frustrated na maisha hawajui babdari wala nini kitakachotokea ni looting na uharifu mwingine. Hawa jamaa walijiamini sana mpaka kukosa hekima kwenye matamshi yao.
Na mtakuwa frustrated zaidi pale mtakaposikia hatima ya nchi hii iko mikononi mwa mzungu km zamani isipotokea mkajitambua nyie ni taifa la kwanza kwa unafiki barani afrika katika zama hizi ambazo mataifa mengine yanatafuta kujikomboa toka katika ukoloni mambo leo, eti walio wazalendo wa taifa ndio wanaopewa kesi za uhaini halafu wahaini kwa kusgirikiana na majambazi wa magharibi ndio mnawatukuza ni bora tukamatwe watanganyika wote kwa kuhitaji rasilimali zetu kuliko kuteswa na uoga wa kijinga kisa muungano wa uongo
 
Back
Top Bottom